Umeshawahi kutoa rushwa?

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Leo nimesikia kuwa huko Uchina kuna mtu alianzisha blog yake ambayo aliwataka watu wachangie na kuandika kama wametoa rushwa na ni kwa nani. Hata hivyo, baada ya muda blog hiyo ilifungwa kwa vile majina ya wakubwa wengi yaliwekwa hadharani.

Ingekuwa ni jambo zuri pia na sis kuweka hadharani watu wote wanaopokea rushwa ili kutoa huduma kwa wananchi. Mimi nilishawahi kuombwa rushwa ili gari langu litoke haraka bandarini, ama sivyo ningekutana na vizingiti vingi. Nadhani ni wengi wetu yametukuta haya.
 
Kama unamiliki gari, nina hakika huwezi pitisha mwezi bila kutoa rushwa kwa askari wa usalama barabarani.
 
Ahh mie nilitakiwa safiri gafla bin vuu sasa ubalozini wakawa wananisumbua yellow card na siku zimeisha, nilienda pale mnazi mmoja nikakutana na nesi fulani na polisi sijui wa kuzuia rushwa haha hahha wao ndo walinipa card na kuniambia andika jina lako upesi weka hela hapo mezani uondoke hahah hahha nilifanya huyoo nikatimua na sindano sikuchoma na foleni niliiikata :bange:
 
nilitaka kupata viza,kuna fomu ya polisi kujaza mambo ya kwamba sio mhalifu,,safari ndani ya wiki nikaambiwa nije kuchukua baada ya wiki 3 aah nikazama mfukoni kutoa rushwa kesho yake tu nikapata fomu,huyoo nikapaa.........
 
Back
Top Bottom