Umepata mchumba mwathirika utawaeleza wazazi ukweli?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,792
Habari za leo wapendwa,

Kama wanasayansi wanavyosema UKIMWI unaweza kudhibitiwa na ARV, sasa umepata mwenza amekwambia ukweli kuhusu afya yake, umegundua ni Zaidi ya miaka mitatu sasa anatumia dawa. Wote mmepata ushauri nasaha na mmekubaliana kuoana.

Kuna mzazi kweli atakaeridhia mtoto wake aoe/aolewe na mwathirika? Au hili utaamua kufa nalo rohoni iwe siri yenu wana ndoa?
 
Lengo la kuwaambia ni nini?
 
Ninadhani ni rahisi kuwaambia wazazi unabadili dini kuliko kuwaambia unajilipua na mwathirika.
Yah swala la dini watapiga kelele mwisho wakuelewa ila la Ukimwi yaan wajue mtoto wao unajipelka mdomon mwa mamba mapema hvyo haiwezekan
 
Labda iwe siri tu.
Sidhani Kama kuna mzazi anaweza kuelewa kwa kweli.
Japo mimi najua unaweza kumkimbia mwenye HIV. Na kesho ukakuta na mwathirika na asikwambie kwamba kaathirika. Akakuambukiza
..Mimi Kama mimi ,
Naishi nae nae bila wazazi kujua tu. Kama kuna upendo wa kweli
 
Umwambie mzazi kuwa unajilipua!!! Hii kwa mzazi wangu nimjuavyo lazma akupeleke maabara kwanza kucheki kama dish halijacheza.
 
Sababu gani zilizompelekea yeye kupata ukimwi?! Na kwa nn asubirie nshampenda ndo anambie hali yake?!

Wengine hapa kumwambia tu mzazi mwanaume alikua na mtoto huko nje unauma meno unamfichia siri yake..itakua ukimwi!!! Wazazi hawatajua labda waote usingizini.

Ishu ni Mimi kukubali kuishi nae.
 
Mmmh..........inahitaji ujasiri sana................................nani yuko willing tayari kujikaanga kwa mafuta yake...!!!!!!!!!
 
Haha, ila watu mna roho ngumu jamani

Yaani mi mtu Kama ana ukimwi hata ale makopo kumi ya ARV hapo hapo siwezi kupiga kavu aisee

Tatizo unaweza kumpenda mtu ukaoana nae ivo ivi,akakuambukiza afu akaja tu kukuzingua huko mbeleni,binadamu hatuna dogo

Sorry for the negativity, and being out of topic for that case
 
Back
Top Bottom