Umenikimbia mpenzi

kwamtoro

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,930
2,000
 1. Kipi kilokukimbiza?, natamani kukijua
  mahaba nimetimiza, kadiri nilivyojua
  mpenzi umeniponza, moyoni ninaugua
  kidonda nakiuguza, sijui lini tapoa.


 1. Nateseka na giza, mawazo yanisumbua
  maswali najiuliza, kipi nilokukosea?
  baadae najikaza, kuishukuru kadhia
  mola ataniliwaza, naye atanisaidia.. 1. Mapenzi yalinawiri, raha nikajiskia
  leo nini kimejiri?, mbona unanisusia
  tuliiweka dhamiri, tutahimili udhia
  leo bila tahayuri, mwenzio wanikimbia


 1. Vingi vimeniponyoka, wala mimi sikujali
  wengi wamenitoroka, ikawa kwangu sahali
  wewe nikikukumbuka, ninapata idhilali
  ahadi uliiweka , leo hii hunijali.?
Nakuombea salama, nikimbie utoweke!


 1. usije ukalalama, baadae ukumbuke
  nuru yangu umezima, niachie niteseke
  rabi tanipa salama, wala nisiadhirike


 1. Moyo wangu nilikupa, tena nikakuridhia
  leo hii wanilipa , unyonge bila hatia
  penzi umeshalitupa, kwengine waelekea
  mimi waniacha kapa, bila kunihurumia 1. Ahsante nashukuru, nami nimeyakubali
  madhali sikukudhuru, nenda potelea mbali
  mola nitamdhukuru, anipe wangu asali
  yaILAHI YA KAHARU, nipe moyo nihimili.


 1. Nalia ninaumia, leo hii sina hali
  wajua nateketea, penzi letu kulijali
  mwenzangu wafurahia, umenitwisha jabali
  nami nimelipokea, nifanye mie jahili. 1. Dunia yazunguka, waswahili wamesema
  wewe utanikumbuka, si hiyari ni lazima
  kwa wema nilikuweka, kwa maradhi na uzima
  leo hii watoweka , kwa mabaya wanisema


 1. Nenda "usotabirika", iko siku nitapona
  kweli nimefadhaika, kwani nilipenda sana
  leo umefarijika, mwenzio ninasonona
  kuna siku nitacheka, tena sio mbali sana. 1. Mola wangu nisitiri, unipe subira njema
  unilinde YA QAHARI, unipe kilicho chema
  uniepushe athari, ya kupenda aso mwema
  uniongoze JALALI , uwe namimi daima.
 
Top Bottom