Msanii wa R&B Ben Pol amewasifia
wasanii wenzake wa Bongoflava
kuwa wana uwezo mkubwa kuliko
hata wasanii wa nchi zilizoendelea
kama Marekani kwa uwezo wao wa
kufanya kazi nyingi zikiwemo utunzi
na kuimba wao wenyewe.
Kupitia Twitter Ben Pol ambaye
mwaka jana na mwaka huu amehit
na ngoma kama Pete na Yatakwisha
amesema, wasanii wa Bongo tuna
vipaji vya hali ya juu, mtu unafanya
kila kitu mwenyewe na bado
unaweza kutunga na kutoa Hits, hii
hata R.kelly hawezi.
Ameongeza kuwa kutokana na
mazingira ya muziki wa kibongo
msanii hujisimamia mwenyewe
anapotaka kurekodi, kushoot video
ama kujiandaa na show ilhali
wasanii wakubwa mfano wa
Marekani huwa na watu
wanaosimamia mambo hayo.
Amesisitiza kuwa msanii hulazimika
kufanya kila kitu kwasababu hawezi
kumudu kuajiri watu wa kusimamia
mambo hayo. Sasa watu hawataki
kulipa vizuri, mwishowe
tunashindwa kutoa ajira kwa
wenzetu wenye utaalam fulani
fulani wa marketing n.k.
Wasanii wengi wakubwa katika nchi
zilizoendelea huandikiwa nyimbo
zao (mashairi na melody) na watu
maalum (songwriters) ambao
hutafutwa na record label husika
kwa kazi hiyo na wao huingia tu
studio kurekodi tofauti na wasanii
wengi wa Tanzania (na kwingineko
Afrika) ambao hutunga na kuimba
wenyewe.