jirani27
Member
- Apr 15, 2014
- 56
- 15
Huwa naamini mkoa wa Ruvuma ni moja ya sehemu iliyobarikiwa kwa rasilimali mbali mbali kama ardhi yenye rutuba, madini na ziwa, na pia mbuga ya wanyama. Kinachonichosha katika mji huu ni ukosefu wa viwanda unaosababishwa na kutokuwa na umeme wa uhakika, huwa sielewi ni kwa nini hadi leo gridi ya taifa bado haijaufikia mji huu hadi sasa tunatumia umeme wa generator. Sijajua wahusika ni nini hasa tatizo katika mji (Manispaa) kama huu kukosa umeme wa uhakika?
Swala la pili ni hili la miundombinu hasa ya maji na barabara. Wametupimia viwanja karibia miaka miwili iliyopita, cha ajabu ni kwamba hatuoni dalili zozote hata za kupitisha greda kwa ajiri ya kutengeneza barabara za mitaani achilia mbali kuweka miundo mbinu ya maji, mfano mji unakojengwa kwa sasa, mkuzo . Sielewi, ni kwamba budget zenu ni finyu au uwalakin mahali?
Mwenye ujuzi na haya ya manispaa wa Songea naomba atujuze nini hasa tatizo?