KILIVITE
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 1,302
- 556
Tatizo la umeme na maji Tanzania limekuwa kero kubwa sana.Serikali ya CCM imekuwa ikitoa ahadi nyingi zisizotekelezeka kutatua ukosefu wa umeme na maji.
Magufuli ana ahidi kujenga viwanda vingi kila Wilaya sasa najiuliza viwanda hivyo vitatumia nishati gani?.Viwanda vingi vinahitaji maji pia.Kila maeneo mjini na Vijijini hakuna maji na hakuna umeme.
Nina amini hakuna maendeleo yatakayopatikana kama hakutakuwa na umeme na maji.Naomba bila kinyongo kila mchangiaji aseme ukubwa wa tatizo la maji na umeme eneo alipo.
Naanza mimi mwenyewe,hapa nilipo Kata ya Mlowa,Makambako Njombe,Kukatika kwa umeme mara kwa mara kumeathiri maendeleo kwa kiasi kikubwa.
Upatikanaji wa maji ni mgumu.Tunalazimika kuamka saa kumi alfajiri kufuata maji kilometa 8.Umeme na maji imeshakuwa kero ambayo CCM imeshindwa kutatua.
Mimi nimeamua kuipiga chini CCM Oktoba 25,2015.Nitampa kura yangu LOWASSA.Wewe je?