Umeme Hutumika Zaidi Sauti ya Redio Ifunguliwapo Kubwa zaidi au La?

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
234
218
Katika kusikiliza redio, kunaweza kutokea swali kwamba je, umeme hutumika zaidi ikiwa redio itafunguliwa kwa sauti kubwa zaidi? Mtu anaweza kujibu kwamba hakuna hata haja ya kujadili jambo kama ilo, kwani redio hutoa sauti kutokana na umeme, hivyo ni dhairi umeme utatumika zaidi redio ikifunguliwa kwa sauti kubwa zaidi. Mfano wake ni kuwashwa kwa tanuri. Moto huwa mkubwa zaidi ikiwa makaa ya mawe yatazidishwa.
Ufafanuzi huo unaoonekana ni sahii lakini siyo kamili kwa jumla. Ukweli ni kwamba: Sauti ya redio na kutumika kwa umeme hutegemea aina ya ya redio. Mpaka hivi sasa kuna aina mbalimbali za redio. Aina moja ni redio ya vali za umeme yaani electron tube, na aina nyingine ni redio itunmiayo transista. Kwa redio itumiayo vali za umeme bila ya kujali ufunguliaji wa sauti kubwa au ndogo, umeme unaotumika ni sawasawa. Hii ni kwa sababu gani? Hii inatokana kwamba umeme unaotumika katika redio hiyo hasa unatumika kuwasha tu ncha- hasi ya vali ya umeme. Wakati ifunguliwapo redio umeme hupaswa uwe wa kiwango fulani, la sivyo, redio haitafanya kazi barabara. Ukifungulia redio kwa sauti ya chini kidogo, hupunguzi utumiaji wa umeme, ila umeme hautabadilika kuwa sauti ili kusikia redioni, badala yake utabadilika kuwa ujoto na kupotea tu (sauti ikiwa kubwa, umeme mwingi utapotea na kiasi kidogo tu kitabadilika kuwa sauti).
Kuhusu redio ya transista itumiayo transista moja, mbili au tatu, utumiaji wake wa umeme hauhusiani na ukubwa wa sauti. Redio kama hiii ina vikuza sauti mbili ya masafa ya chini yaani low frequency ambayo husukuma kipaza sauti na inaitwa njia ya umeme ya kutolea sauti kwa kusukuma. Tabia ya njia hiii ni kwamba sauti ikiwa ya chini, umeme utumikao katika kikuza sauti unakuwa mdogo na sauti ikiwa kubwa, Umeme utatumika zaidi.
 
vipi na kwa upande wa magari ni mwendo upi unakula mafuta sana kuendesha kwa spidi kubwa au kundesha polepole
 
Back
Top Bottom