Umegaji Selous unufaishe taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umegaji Selous unufaishe taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gwaje, Jul 7, 2012.

 1. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Umegaji Selous unufaishe taifa
  NA MWANDISHI MAALUM
  6th July 2012
  Maoni
  Serikali ya Tanzania imo katika furaha kubwa baada ya Kamati ya Urithi wa Dunia inyo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kukubali kumegwa kwa eneo la pori la akiba la Selous baada ya kuwako kwa harakati nyingi za kitaifa na kimataifa za kushawishi hatua hizo.

  Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kiasi cha km za mraba 200 zitamegwa kutoka pori hilo lenye km za mrada 50,000 ili kuruhusu uchimbaji wa urani ambayo inadaiwa kuwako nyingi mno katika eneo hilo la kusini mwa Tanzania.

  Eneo hilo linadaiwa kuwa limekwisha kuvutia kampuni ya uchimbaji urani ambayo inatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 400 sawa na Sh. bilioni 640, mradi utakoifanya Tanzania kupata mapato ya Sh. bilioni 8 kwa mwaka wakati wachimbaji watajipatia kiasi cha Sh. bilioni 320, jambo linalopokewa kwa furaha kubwa kwamba mapato ya serikali yataongezeka na hivyo kujenga uwezo wa kutunza pori la Selous.

  Furaha ya serikali inatokana pia na kufikiwa kwa mwisho wa harakati wa wanaharakati wa mazingira ambao wamekuwa wakiukataa mpango wa kuchimba urani katika eneo hilo ambalo ni moja ya urithi wa dunia, lakini zaidi sana kuona kwamba walau kilio chake kimesikika kwamba nia siyo kuharibu urithi huo ila ni kuona taifa likinufaika na rasilimali iliyoko bila kuathiri urithi huo.

  Tunaelewa furaha ya serikali nasi tungependa kuipongeza kwa kufanikiwa kupata fursa hiyo ya kuendesha mradi wa uchimbaji urani katika eneo hilo, tunasema hivyo kwa sababu kwanza serikali imeheshimu na kufuata taratibu za makubaliano ya kimataifa juu ya utumiaji wa rasilimali ambazo zimo kwenye maeneo ambayo ni urithi wa dunia.

  Hii inajenga heshima ya taifa katika jumuiya ya kimataifa kwamba inaaminika na kufuata sheria na kanuni husika.

  Hata hivyo tungependa kutoa angalizo mapema juu ya uchimbaji wa urani katika eneo hili, mbali ya changamoto za kuendelea kulinda mazingira na kuhifadhi eneo la pori la Selous, bado kuna changamoto moja kubwa juu ya mustakabali wa taifa hili katika kuvuna rasilimali zake.

  Uzoefu uliopo unaonyesha kuwa pamoja na taifa hili kufungua milango katika uwekezaji mkubwa wa uchimbaji wa madini ya aina zote, dhahabu na hata vito, bado taifa halijanufaika sawasawa na uwekezaji huo kwa sababu mbalimbali.

  Miongoni mwa sababu kuu ambazo zinatajwa kuwa changamoto kubwa ya kuikwamisha nchi na wananchi wake wasinufaike na matunda ya rasilimali hizi zinapovunwa, ni uwepo wa mikataba mibaya ambayo kimsingi hailengi kuinufaisha nchi isipokuwa kuiacha katika ukiwa.

  Kelele nyingi zimepigwa juu ya mikataba hii, kilio kikiwa ni kutaka ipitiwe upya ili taifa linufaike na neema hii ambayo watu wake wamepewa na muumba.

  Kwamba rasilimali hizi zinakwisha siyo jambo geni, lakini kinachosumbua watu ni kwamba uhamishaji wa rasilimali hizo kwenda kuendeleza wengine na kuacha taifa katika ukiwa ule ule siyo jambo linalofurahiwa na wengi.

  Ni kwa kutambua ukweli huu tunauliza swali la kichokozi kwa wahusika wote wanaoshangilia uamuzi huu, kwamba sasa eneo la Selous linamegwa ili kuruhusu uchimbaji wa urani wanajua kuwa habari itakuwa ni kama ile ile ya uchimbaji wa dhahabu, tanzanite na hata gesi asilia?

  Ndiyo maana sisi tunasema kuwa furaha hizi za wizara zingekuwa na maana zaidi kwa taifa hili kama tungejipanga vizuri katika kuhakikisha kwamba taifa linanufaika kwa kiwango cha juu katika uvunaji wa rasilimali hizi.

  Ni ukweli usiopingika kwamba hadi sasa kama taifa hatuwezi kutamba kwamba tunanufaika ipasavyo na uvunaji wa rasilimali hizi.

  Itakuwa ni kupoteza muda na wakati kama uwekezaji katika eneo hilo utagharimu Sh. bilioni 640 huku wawekezaji wakinufaika kwa kiasi cha Sh. bilioni 320, huku taifa likiambulia Sh. bilioni 8 tu kwa mwaka.

  Hapa hakuna kile kinachoitwa kwa kimombo equitable sharing of benefits, yaani unufaikaji wa haki. Bila kufanya hivyo, taifa hili halina sababu yoyote ya maana kuendelea kuvuna rasilimali hizi tulizopewa kwa neema na muumba wetu.
  Kama mtaji wa uwekezaji ni bilion 640 kwanini tusiwekeze wenyewe?
   
Loading...