Nakumbuka ilikua siku ya jumatatu nilipoanza kuziona dalili za kwanza za kifo chake,Baada ya kumaliza kupika nilikua na kawaida yakupumzika sebuleni nikimsubiri atoke kazini, kila jioni muda kama huu ilikua ni ngumu kwangu kuyazuia mawazo yangu yasitoroke na kukumbuka siku ya kwanza nilipokutana naye,sikukutana naye kisimani kama Yakob alivyokutana na
Raheli na wala sikukutana naye Shuleni au Chuoni sehemu ambayo mapenzi ya wengi uanzia, nilikutana naye hatua chache kutoka nyumbani kwangu upenuni mwa Nyumba aliyokua amejibanza akisubiria Mvua iishe aendelee na Safari yake,Mvua ilikua kubwa huku ikiambatana na Baridi kali nisingeweza kuendelea na safari japo nilikua nimebakiza hatua chache nifike kwangu na hivyo ilinibidi na mimi nijibanze pembeni yake.
Kila manyunyu yaliyokua yanadondoka na kulibamiza bati tulilokua chini yake yalikua yakitengeneza kelele ambayo ilikua ngumu kwa sauti yoyote kusikika vizuri labda kama ingebidi kupayuka kama mwendewazimu,na kati yetu hakuna aliyekua anataka kuonekana kwa mwenzake mwendawazimu,ilikua ni baada ya mvua kupungua na dalili kuonyesha haitachukua muda kukoma kabisa ndipo aliniuliza =Bado una safari ndefu sana?
-Aliuliza huku meno yake yakitoa sauti ya kugongana na vitu kama moshi vikitoka mdomoni mwake vyote vikiashilia kua Baridi ilikua kali na ilimuingia sawa sawa –Hapana mi tayari nimefika nakaa hapo mbele tu.Nilijibu huku nikinyanyua mkono kumuonyesha kitendo kilichoifanya blauzi yangu iliyoloana igandie kwenye Ziwa langu la kulia na hata nilipoushusha mkono iliendelea kugandia na kufanya taswira ya ziwa langu kuonekana na chuchu kujichora.
Ilikua ni mpaka pale nilipoaga kuendelea na Safari yangu ndipo niligundua kua alikua akiniangalia kwa kuibia jambo ambalo lilinifanye kuwaza kama alikua akiangalia kifuani kwangu pia.-Dada yangu naweza kupata Namba yako?Aliongea kwa sauti iliyotoka kinyonge kama Mtoto anayemuomba Mama wa kambo Hela ya matumizi ,sauti ambayo ililainisha Moyo wangu na kunifanya niende kinyume na sheria ya kamwe kutompa namba yangu ya simu mtu nisiye mfahamu vizuri.
Kitendo cha kumpa Namba yangu ya simu kilipelekea mimi na yeye kua wapenzi miezi miwili baadaye ,tumeona mvua nyingi kama zile tukiwa pamoja,kisha Masika yakaja na kufanya Ardhi kuwa ya kijani na Miti kustawi tukiwa pamoja na baadaye kiangazi kikaja na kupukutisha chini majani na kuifanya Ardhi kua nyekundu na mbaya kama imetupiwa laana tukiwa pamoja.
Katika kipindi chote hicho tumekua wenye furaha ingawa kuna vipindi tuliumizana na kuapa kwamba tumeachana na kisha siku mbili tukarudiana.Miaka miwili baadaye tulisimama altareni na huyu Padri mwenye miwani na sauti ya taratibu akasema kuanzia leo kwa mamlaka niliyopewa na kanisani nawatangaza nyie kua ni mume na mke.
Mwaka moja sasa tu Mume na Mke,na Jioni muda kama huu nikiwa nimevaa nightdress yenye kuonyesha maungo yangu kwa mbali nipo sebulen nikimsubiri arudi toka kazini nimpokee na kumtua mizigo kisha nimvulishe nguo na kumuelekeza bafuni na kisha baadae nimkaribishe chakula mezani.
Giza litakapozidi na kua tororo tutafunga milango na madirisha na kisha kuzima taa,tutajitupia kitandani kama tulivyozaliwa nitamkumbatia kwa mikono yangu miwili tena kwa nguvu sana kama mtoto anavyomkumbatia mdoli anayehofiwa kupokonywa,kwenye mikono yake,a uchovu,maudhi na kadhia zote alizozikusanya siku nzima zitayeyuka kama nailoni kwenye tanuru la moto na kisha tutaseleleka taratibu kwenye usingizi mzito na kuiaga siku.