Umaskini chanzo cha kuuza dawa bila cheti cha daktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaskini chanzo cha kuuza dawa bila cheti cha daktari

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mjadala umeanza katika maeneo tofauti kufuatia kuchapishwa kwa matokeo ya utafiti kuhusu ununuzi wa dawa zinazohitaji cheti cha daktari, ulioonyesha kiwango cha maelekezo hayo kutofuatwa.

  Kimsingi utafiti huo ulionyesha kuwa kuuziwa dawa zinazohitaji cheti cha daktari bila kuwa nacho ni jambo la kawaida zaidi katika maeneo yenye kipato cha chini, na ni nadra zaidi katika maeneo yenye kipato cha juu. Huo ndiyo msingi wa hali hiyo, lakini inaelekea mjadala haulekezi hisia huko, ila katika taaluma.

  Siyo tu kuwa wanaojadili suala hilo wanaweka kando suala la umaskini, bali pia kuna kiwingu cha kuona ni mazingira gani ambako dawa zinanunuliwa, na inawezekana utafiti huo haukufikia kina cha kutosha kuhusu suala hilo.

  Mara nyingi dawa zinanunuliwa kwa mtu kufahamu ugonjwa, akawa anahitaji dawa kwa haraka na hana fedha za kutosha kuanza kwenda hospitali kwanza au zahanati binafsi, achukue vipimo halafu ndipo anunue dawa. Hiyo inaweza kugharimu shilingi elfu tano kabla ya kununuliwa dawa.

  Ikiwa mgonjwa ana shilingi elfu tatu au nne za kuweza kununua dawa, wanachosema wakinzani wa kununua dawa bila cheti cha daktari ni kuwa akae tu na ugonjwa ukizidi si ajabu akafa, lakini kwa hali yoyote kanuni hiyo isivunjwe.

  Si hoja yenye maana kwa mtu anayeumwa na anataka dawa, au jamaa zake, au ni mtoto ameugua na wazazi hawana fedha za kupata vipimo kwanza kabla ya kununua dawa. Ina maana kwamba katika mazingira hayo ni lazima dawa itafutwe kwanza, na akihitaji zaidi, vipimo vipatikane.

  Mara nyingi ndivyo inavyokuwa katika masuala ya kununua dawa na kutafuta vipimo, kama katika usemi wa matangazo ya ‘dawa baridi’ unaoelekeza kuwa ‘maumivu yakizidi mwone daktari,’ ila pale unapohitaji tu dawa baridi hakuna haja ya kumwona daktari.

  Ni wazi kuwa mtu akiwa na ugonjwa unaohitaji dawa isiyo ‘baridi’ na hana fedha za kutosha atakachofanya si kupima na kurudi nyumbani kukaa, ila kununua dawa.

  Baada ya kupata ‘dozi’ moja, inayotazamiwa kuondoa ugonjwa, akiwa bado hajisikii vizuri au hana hakika ya kupona, hapo kwa jumla atahitaji kupata ushauri wa daktari kwani kwa vyovyote hataendelea kubahatisha.

  Pale mtu anapoona hajapona vizuri ni tofauti na pale ugonjwa unapolipuka akashindwa hata kuketi, kulala au kufanya kazi za kawaida ambapo katika hali hiyo ni lazima apate dawa kwa haraka.

  Anapokuwa ameshapata dozi, hali yake itakuwa haina haraka kama mwanzo, na kwa njia hiyo anakuwa na fursa zaidi katika kupanga fedha za kupata vipimo na ushauri kamili wa daktari kwa sababu anazo dalili za ugonjwa lakini hauenei haraka mwilini. Ni kama mtu anayetaka kujua vizuri afya yake, kama amepona au hapana.

  Kwa upande mwingine muuza dawa hawezi kukataa kata kata kuuza chochote bila cheti cha daktari kama wakazi wa eneo hilo kwa jumla ni maskini, kwani anaweza kusababisha maafa.

  Isitoshe anaweza kugombana na watu akose uhusiano unaohitajiwa katika kuendesha biashara, hivyo atatoa ushauri anaoweza au unaopasa kuhusu matumizi ya dawa.

  Na ndiyo maana sheria inahitaji muuza dawa awe pia ni mtaalamu, kwa vile siyo kila kitu kitategemea cheti cha daktari, yeye awe na uwezo tu wa kukisoma, basi.

  Haya ndiyo mambo ambayo tunadhani Serikali yetu na wataalamu wa afya wanapaswa kuyatizama kwa macho mawili ili kuwasaidia wananchi hasa wa kipato cha chini ambao hujikuta wakichukua maamuzi kinyume na taratibu za kitabibu na hivyo kuhatarisha maisha yao.

  Na la msingi zaidi ni serikali kuhakikisha kuwa hali ya umasikini waliyo nayo wananchi wengi inatokomezwa ili hali hatarishi kama hizo za watu kujitibu bila ushauri wa daktari ufikie kikomo.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa dr. Inaitwa vicious cycle. Mgonjwa hana uwezo wa kumudu kulipia consultation, mwenye dawa anataka hela hamuachii asie na prescription, mkaguzi wa dawa akikuta hii hali hana ubavu wa kumuwajibisha muuza dawa manake kawekwa kibindoni. Baada ya usubi kuonekana, daktari hana hata interest ya kazi na hajali kuuliza chanzo cha tatizo.

  Hivi unajua kuna pharmacies nyingi tu mitaani zinauzwa na mahousigal?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Hakuna Serikali (Polisi) kuwakamata hao Ma House girl?au nchi haina Serikali?Viongozi wamelifumbia macho hilo tatizo la Uuzwaji wa Dawa Kiholela? King'asti
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Askari ndo anakamilisha vicious cycle. Akikuta housigelo si ndo anachukua elfu ishirini akalipie mwanae matibabu ama ada ya shule?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...