Umasikini ni miongoni mwa vyanzo au sababu za kuporomoka kwa maadili Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,102
4,228
Pamoja na uwepo wa sababu nyingi ambazo zimeonesha kuwa ndizo zinazosababisha maadili kuporomoka Nchini hatupaswi kusahau kwamba Umasikini nao unachangia kwa kiasi kikubwa mno katika kuharibu maadili yetu na ninapouzungumzia umasikini nagusia kuanzia ngazi ya Taifa hadi mtu binafsi.

Taifa linalopambana kuutokomeza umasikini na likafnikiwa kwa kiwango chochote kile moja kwa moja huwa linapiga hatua katika kuweza kujisimamia kimaadili.

Ipo haja ya kupambana na umasikini wa kila namna kwa kuwa ndiyo unaozaa neno umasikini na hali ya umasikini ili tuweze kufikia hatua ya kujiuliza maadili yetu ni yapi"our national ethos".

Asili"nature"na Jamii au malezi"nurture"zinaweza zikaitwa sababu Mama na Baba katika maadili ya Mtu yeyote yule lakini sababu hizo ukijumlisha n umasikini tunapata janga la kimaadili.
 
nauliza kwa mtoa mada na wengine:
1. mataifa tajiri kama Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na mengine ndo yanaongoza kwa maadili mazuri? na nchi maskini ndo zinaongoza kwa maadili mabovu?
2. watu matajiri na maskini nani ana maadili mazuri kuliko wengine?
 
Mkuu umehit utosi wangu kwa hakika. Jamaa ajitahidi tu akujibu ili mjadala uendelee
 
Ukiwa maskini wa kipato hapohapo we ni jizi,changu,jambazi ndo utaonekana hukulelewa ktk maadili mazuri.
 
Pamoja na uwepo wa sababu nyingi ambazo zimeonesha kuwa ndizo zinazosababisha maadili kuporomoka Nchini hatupaswi kusahau kwamba Umasikini nao unachangia kwa kiasi kikubwa mno katika kuharibu maadili yetu na ninapouzungumzia umasikini nagusia kuanzia ngazi ya Taifa hadi mtu binafsi.

Taifa linalopambana kuutokomeza umasikini na likafnikiwa kwa kiwango chochote kile moja kwa moja huwa linapiga hatua katika kuweza kujisimamia kimaadili.

Ipo haja ya kupambana na umasikini wa kila namna kwa kuwa ndiyo unaozaa neno umasikini na hali ya umasikini ili tuweze kufikia hatua ya kujiuliza maadili yetu ni yapi"our national ethos".

Asili"nature"na Jamii au malezi"nurture"zinaweza zikaitwa sababu Mama na Baba katika maadili ya Mtu yeyote yule lakini sababu hizo ukijumlisha n umasikini tunapata janga la kimaadili.
Eleza maadili gani yanayochagizwa na umaskini?
 
MTV Bongo sikutaka kufanya ulinganisho kwa kuwa maadili yanatofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine "moral relativism"
Na simaanishi kwamba mataifa tajiri yana madili mazuri kuliko Mataifa masikini kwa kuwa ubora au uzuri wa maadili unategemeana na jamii pamoja na miiko yake na inaeleweka kuwa jamii hazifanani.
Lengo langu ni kutaka kutambua kuwa umasikini unachangia jamii kukosa nguvu hata ya kuisimamia miiko yake na hivyo kutoa mwanya kwa mambo yasiyowiana na miiko ya jamii kuingia au kuingizwa kiurahisi mno
 
Back
Top Bottom