Umasikini hautakwisha kama mfumo huu wa elimu utaendelea katika nchi zetu za africa hususani Tanzani

Joselela

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
5,919
7,624
Pamoja na mambo yote yanayofanywa na serikali za africa hususani Tanzania bado umasiki upo kwa kiwango kikubwa..
Katika uzi huu nitaizungumzia Tanzania sana...

Ili umasikini uweze kupungua ni lazima mifumo ya serikali yetu ubadilike..
Mfumo uliopo sasa umeegemea kwamba mwanafunzi ataanza darasa la awali hadi darasa la saba atakaeshinda katika hatua hii ataendelea na elimu ya upili,yaani kidato cha kwanza hadi nne na atakaeshinda ataendelea na elimu ya upili wa juu yaan kidato cha tano hadi sita,pia atakaeshinda ataendelea na elimu ya juu...

Sasa tujiulize umasiki utpunguaje kama lengo la elimu ni kupunguza umasikini sio kufika chuo kikuu.

Saivi utakuta watu wengi wamesoma hadi kufikia elimu ya juu kabisa lakini bado ni masikini,sijui tatizo hapa ni nini?

Na yule alie shindwa utakuta anamafanikio kuliko huyo,kwanini??

Sababu kuu za maswali hayo juu ni..
1.Elimu yetu inafundisha kwamba anaefaulu ndie alifanikiwa na ndie atakaefanikiwa kimaisha.(haya ni matabaka yanayojengwa katika elimu yetu mapema) ndio unakuta mwanafunzi anakata tamaa ya kujifunza...

2.mfumo mbovu wa kuandaa walimu.
Mfumo huu uliopo sasa wakuchukua wenye viwango fulani kwenda kusoma ualimu nikosa kubwa sana,hasa mfumo huu unaotumiwa na serkali kuchagua wanafunzi wa kujinga na taaluma hii adhimu ya ualimu.

3.Mitaala mibovu kwa maana ya kwamba mitaala yetu imejikita kwa asilimia 85 katika ufaulu wa masomo darasani..
Kimsimgi wanafunzi watakao pata elimu watakuwa na uwezo mdogo wa kufanya kwa vitendo mfano mtu anapata degree ya computer science lakini hawezi kutengeneza hata viruses n.k mtu anasoma kilimo anashindwa hats kuanda bustani yake ya matunda kisa wamesoma elimu ya nadharia tuu...

4.Sekta ya elimu imefanywa kama ni sekta ya viwanda na biashara sio huduma..hapa namaanisha kwamba sekta ya elimu imekuwa kama biashara ya korosho au mpungu sio huduma,mbali na elimu bure ya sasa bado gharama ni kubwa za elimu.
Mfano upatikanaji wa vitabu vya kujifunzia na kufundishia.

5.Serikali kutopanga fedha maalumu za mafunzo kwa vitendo na utafit kwa sekta zote kama ilivyo kwa upande wa madaktari.

6.Matumizi ya kodi za wananchi ovyo...
Kwamaana ya kwamba utakuta mtu ni afisa usalama,mkuu wa wilaya,waziri yena hadi wa ulinzi analindwa kwani nchi hii kuna vita??,viongozi wanatembelea magari ya kifahali wakati huo huo vitabu mashuleni hakuna bado posho wakati kule mitaani wananchi wanamsubiri mwanafunzi arudi shule ili wale kiporo kilichobaki jana usiku.

6.Maslahi madogo ya walimu hili pia ni tatizo kubwa sana.,tujaribu kuwapa walimu wetu posho kama anazopata mkuu wa wilaya uone kama kuna mwanafunzi atashindwa kujua kusoma au atakae shindwa...Najua kulinga na elimu wanayopata walimu wetu vyuoni inatosha kabisa lakini wanakuja kuvunjika moyo katika mishahara ingawaje elimu ni wito..

Fikiria mwalimu au wewe kiongozi unaweza enda kufanya ziara ya ghafla bila chochote kupata asubuhi na ukirudi mchana pia hivo hivo,kimsingi hii ni hali halisi ya walimu wetu ndio maana mwalimu anaamua kuza ubuyu,bagia n.k shuleni ili angalau apate pesa ya kutimiza mahitaji yake wakati akisubiri kakipande kadogo ka keki ingawa yeye ndio mtengenezaji while hana haki ya kugawa.

7.Sheria mbovu zilizopo kwa viongozi hivyo kuingilia taaluma hii adhimu ya ualimu.kawaida idara ya ukaguzi ndio inatakiwa kushughurikia matatizo yaliyopo katika shule zetu na kupeleka serkali kuu...
Hapa ndio sioni umuhimu wa idara ya elimu ya mkoa na idara yaukaguzi mkoa badala yake zinaishia kuanda mitihani ya mock ya mkoa(mtihani wa utamirifu basi)..sasa sijui mnaandae wakati hamfuatlii matatizo yaliopo shuleni na kudhibiti ipasavyo badala yake mnawaachia wakuu wa wilaya na mikoa kuja kuriporti kwenu si ndio hivyo..lakini wakuu hawa pia wamezifisha kiherehere,nyinyi shughulikieni wale waliopo chini yenu sio una shuka moja kwa moja kumtumbua mkuu wa shule alagu anaacha hizo idara tajwa hapo juu..

8.Udhibiti wa masuala ya utawazi hususani simu za mikononi kwa wanafunzi na walimu na baadhi ya vituo vya television.
Kimsingi walimu wetu mnachati mno hata katikati ya kipindi.hivi ukitumiwa sms inayohusu mapenzi katikati ya kipindi cha dakika 40-80 unaweza kumudu kufundisha..
Mfano ulikuwa umemtongoza mtu awe mvula au msichana akaja kukutumia sms wakati ww upo katika kipindi bila yeye kufahama akakutmia nimekubali,itakuaje yani utaweza kufundisha kweli au concentration yote si itahamia huko,hapo nimetolea kwenye ishu ya mapenzi tu ila kuna mambo mengi yanayoweza kuinterfere shughuli ya ufundishaji.

So my take here,simu zote iwe kwenye idara yoyote ya serkali zikusanywe kwa mkuu wa hiyo ofisi sio kwa secretary au mkuu wa idara au mwalimu wa taaluma.

Kuhusu television nivyema kuundwe chombo kitakacho simamia na kuhusika na maadhui ya vipindi kwa kuwa vipindi vingi havina maana katika maisha ya watu wote ikiwemo wanafunzi...
Tunaka vipindi ambavyo watu wanadive kwenye maji wanafanya utafiti ilikuaamsha hali za wanafunzi kusoma au kupenda hicho kitu hivyo kuongeza bidii katika masomo sio kuonesha vitu vya ajabu vijana wanaita ubuyu na ushilawadu"

Mwisho.
Nadhani mtu yoyote mwenye akili sawasawa na aliesoma maelezo machache hapo juu anaweza kupata njia ya kutokomeza matatizo yaliyopo mbali na hayo machache tu yakiyoguswa ili kutokomeza umasikimi kwa njia sahihi ya elimu.

`Mtu yeyote mwenye elimu atafanikiwa lakini sio kwa kiwango cha kupata mafanikio makubwa lakini inawezekana endapo atatumia watu wenye elimu katika shughuli zake zilizo halali si vinginevyo`~joselela.

Karibuni kwa mchango zaidi matusi mwisho baharini.
[HASHTAG]#seeingisbelieving[/HASHTAG] [HASHTAG]#comeclose2017[/HASHTAG]
 
Mkuu nakubaliana na we kabisa yan elimu yetu IPO more theoretical kuliko practical nafikiri ni kaz ya serikal kubadili mfumo mzim wa elimu yetu nakuweka special class kwa kila mwanafunzi anayetaka kujifunza masuala mbalimbali mf.sayansi,arts,biashara,michezo more practical kama wenzetu wa ulaya nafikir kwa kufanya hivyo tutapata wataalamu ktk sekta mbalimbali.
 
Maadhimisho ya siku ya walimu na hali ya elimu kiujumla.
 
Huuu mfumo wa elimu utaisha endapo sisi tunaoutumia saizi tutauacha, unless otherwise yanapita sikio la kwanza yanatokea sikio la pili, maisha yanaendelea
 
walimu wa kitanzania ni sawa na mtu ambae ulikuta anapigwa kama mlevi hajui hata kurusha ngumi halafu unaenda kujuinga chuo cha karate unakuta huyo mtu ndio master. hapo ndipo utaposhangaa mwalimu anawahamasishaje wanafunzi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha elimu itakufanya uwe na mafanikio wakati yeye mwalimu hana mafanikio. tafadhali serikali wafanyeni walimu wae na maisha mazuri iwe rahisi kwao kuhamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii wazungu wanaita role model.
 
Kwa Mfumo Hu Wa Elimu Ni Ngum Kutokomeza Umaskn,koz elimu itolewayo inamapungufu meng,km vle ni nadharia zaid,mrundkano wa maxomo kwa mwanafunz mmoja,vfaa vya kujfunzia na kufundshia ni duni,serikal kutoxamin wahtmu wa koz mbalimbali,elimu ye2 inafundsha kuajiriwa zaid,huduma mbovu kwa wawezeshaj,km makaz,maj,umeme,mishahara,nawasilisha,,
 
Tuache kwa njia ipi mkuu unless otherwise tuwepo kwenye system ingawa tayari wapo waliotumia huu mfumo na wanatambua kuwa ni mbovu wapo kwenye system wanazunguka tu kwenye viti na chai kwa round table ya mikutano wenyewe wanafanya restaurants kwa office.

Nadhani kazi kubwa tu wahamasishe walioshika mpini wabadili muelekeo jembe laweza kata kizazi Chao pia.
Huuu mfumo wa elimu utaisha endapo sisi tunaoutumia saizi tutauacha, unless otherwise yanapita sikio la kwanza yanatokea sikio la pili, maisha yanaendelea
 
Kwa Mfumo Hu Wa Elimu Ni Ngum Kutokomeza Umaskn,koz elimu itolewayo inamapungufu meng,km vle ni nadharia zaid,mrundkano wa maxomo kwa mwanafunz mmoja,vfaa vya kujfunzia na kufundshia ni duni,serikal kutoxamin wahtmu wa koz mbalimbali,elimu ye2 inafundsha kuajiriwa zaid,huduma mbovu kwa wawezeshaj,km makaz,maj,umeme,mishahara,nawasilisha,,
Nadhani wanatambua ila wanafanya makusudi kutoelimisha na kuwapa elimu masikini ili waendeleee kutawala wajinga waliokosa Elimu bora.

Mtaji wa mwanasiasa na siasa chafu ni ujinga.

#LofaMimi
 
walimu wa kitanzania ni sawa na mtu ambae ulikuta anapigwa kama mlevi hajui hata kurusha ngumi halafu unaenda kujuinga chuo cha karate unakuta huyo mtu ndio master. hapo ndipo utaposhangaa mwalimu anawahamasishaje wanafunzi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha elimu itakufanya uwe na mafanikio wakati yeye mwalimu hana mafanikio. tafadhali serikali wafanyeni walimu wae na maisha mazuri iwe rahisi kwao kuhamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii wazungu wanaita role model.
Ni ushauri mzuri kabisa mkuu walimu wawe role mode.

Mwaka 2017 nilikuwa sehemu fulani hivi nilienda mahali nilikuta walimu wanne wanatumia ofisi moja kwa pamoja kama makazi yao tena ofisi yenyewe ipo katikati ya darasa la kwanza na darasa la nne mbele ni sehemu ya parade bafu ya kuogea ni ofisi nyingine ambayo bado haijaisha na haina milango, mlango ni kujibana kwenye kona au kufunga shuka mlangoni uwe ndio mlango.

Muda mwingine walimu hawa wanasema wanaamka usiku sana kabla wanafunzi hawajafika ili waweze kuoga.

Huo ni mfano tu wa shule moja ambayo mazingira yake siyo kijijini sana ila ni katika mji mdogo unaokuwa kwa kasi.

Je tutegemee wanafunzi kumuheshimu walimu wao?

Hii ndio sababu ya wao wanafunzi kukataa kusomea hii taaluma kwa sababu wanafanya reasoning kati ya mwalimu na kada zingine.

Mwalimu anamaisha duni kuliko balozi wa nyumba kumi.
 
Back
Top Bottom