Umakini na njia mbadala unahitajika, mkataba wa EPA huwenda ukaivunja jumuiya ya Afrika Mashariki

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wadau

Salaam Jf

Nimefikiri na kuwaza kwa sauti ya chini sana, nimewaza kwelikweli na sijakosea kuwaza kwa baadae.

Katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Daresalaam juzi juzi kwa

malengo ya kujadili mkataba mustakabali wa EPA sambamba na kumkabidhi uwenyekiti Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, katika mkutano huo kwa jina la Mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulistahili kuhudhuriwa na Marais wenyewe kutokana na umuhimu wake kimaamuzi wakae meza moja wakiangaliana machomacho kutoa ya moyoni mwao na ni walakini ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais Dr Magufuli wakati nchi nyingine zilituma wawakilishi kama Mawaziri na Makamo Rais mfano Mh Ruto kutoka Kenya, nchi zilizotuma wawakilishi ni Rwanda, Kenya, Sudani Kusini na Burundi walituma wawakilishi, kwa kuzingatia umuhimu wa mkutano ule katika kuamua kama watasaini mkataba wa mahusiano ya kibiashara kati jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya yaani EPA au laa, Aidha kwa kuwa mkutano uliopita tayari nchi za Rwanda na Kenya zilisaini mkataba huo kinyume na makubaliano ya jumuiya ya Afrika Mashariki ingekua ni bora nchi zote wanachama wangekataa kusaini mkataba huo nyonyaji kuliko kuwa na nchi kigeugeu, vilevile kuna habari kwamba nchi za Ulaya zipo tayari kuandaa mkataba mpya wa kufanya biashara na nchi zilizosaini mkataba huo,vile vile machomacho na maombi ya nchi ya Somalia kutaka kujiunga na jumuiya yetu Afrika Mashiriki wote tunajua hali ya usalama usio imara nchini Somalia hususani maeneo ya kiuchumi na kisiasa, ninauliza hivi ni kweli wenzetu tupo nao pamoja kwenye njia moja? au kuna mkono mrefu mchafu wa nusu msafi nusu mchafu? ukizingatia Tanzania imetangaza kuwa ya viwanda, ninavyojua Jumuiya yoyote ya nchi duniani huwa na lengo na maslahi yanayofanana, wajuvi wa mambo ya mahusiano ya kimataifa, uchumi na biashara tufungueni macho mtoe njia mbadala na salama.
 
Wadau

Salaam Jf

Nimefikiri na kuwaza kwa sauti ya chini sana, nimewaza kwelikweli na sijakosea kuwaza kwa baadae.

Katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Daresalaam juzi juzi kwa malengo ya kujadili mkataba mustakabali wa EPA sambamba na kumkabidhi uwenyekiti Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, katika mkutano huo kwa jina la Mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulistahili kuhudhuriwa na Marais wenyewe kutokana na umuhimu wake kimaamuzi wakae meza moja wakiangaliana machomacho kutoa ya moyoni mwao, walakini ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais Dr Magufuli wakati nchi nyingine zilituma wawakilishi kama Mawaziri na Makamo Rais, nchi zilizotuma wawakilishi ni Rwanda, Kenya, Sudani Kusini na Burundi walituma wawakilishi, kwa kuzingatia umuhimu wa mkutano ule katika kuamua kama watasaini mkataba wa mahusiano ya kibiashara kati jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya yaani EPA au laa, Aidha kwa kuwa mkutano uliopita tayari nchi za Rwanda na Kenya zilisaini mkataba huo kinyume na makubaliano ya jumuiya ya Afrika Mashariki, vilevile kuna habari kwamba nchi za Ulaya zipo tayari kuandaa mkataba mpya wa kufanya biashara na nchi zilizosaini mkataba huo,vile vile machomacho na maombi ya nchi ya Somalia kutaka kujiunga na jumuiya yetu Afrika Mashiriki wote tunajua hali ya usalama usio imara nchini Somalia hususani maeneo ya kiuchumi na kisiasa, ninauliza hivi ni kweli wenzetu tupo nao pamoja kwenye njia moja? au kuna mkono mrefu mchafu wa nusu msafi nusu mchafu? ukizingatia Tanzania imetangaza kuwa ya viwanda, ninavyojua Jumuiya yoyote ya nchi duniani huwa na lengo na maslahi yanayofanana, wajuvi wa mambo ya mahusiano ya kimataifa, uchumi na biashara tufungueni macho mtoe njia mbadala na salama.
Ni bora kuwa kama uingereza walivyojitoa jumuiya ya ulaya, ukawa huru kufunga mikataba na nchi ambayo/ambazo una nafasi ya kunufaika kiuchumi, na kubaki na mipaka iliyo salama. Wenzetu waliosaini awali walishaona fursa za kunufaika na mkataba wa EPA, kwetu sisi EPA ni kutibua habari zote za kuendeleza viwanda, na kuicha Tanzania ikiwa siyo salama. Kwa hili mimi nasimama na Rais wangu.
 
Wakati nyie mkiendelea na ima msaini au msisaini, mkumbuke kuwa AGOA nayo extension yake ni hadi 2025, baada ya hapo ni "reciprocal trade. Every But Arms (EBA) nayo mashakani. GSP ndio hivyo ishafanyiwa mabadiliko. Tanzania needs to be smart enough to feal with with EPA.
 
Kwanza EPA haina chochote kipya kwa nchi kama Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan. Kama LDC countries wanapata favorable treatment under WTO kwenye soko la Ulaya without reciprocity. Lakini Kenya is a developing country, kwahiyo hizo favor hazipati.

Kufa kwa EAC sio tatizo, maana Tanzania anafanya Biashara sana na nchi za SADC kuliko nchi za EAC. Tuna ukubwa wa eneo more than the combined other partner states of EAC, we have the highest population more than any country in the EAC., therefore the impact of the collapse of EAC are not so major kwa Tanzania.

Kuhusu EU, japo kuwa tunaexport kwenda Ulaya some primary products, still our major trading partners sio EU, it is China and India. and kwa kenya, Kuna maua anaexport kwenda EU ndo hayo yanampa tabu sana.

The truth is, the deal has very minimimal benefits for LDC, kutokana na fact kwamba, tatizo kubwa ambalo nchi kama za africa zinashindwa kuexport na kucompite kwenye masoko makubwa kama EU, sio mambo ya tariffs, (GSP and GOA). TATIZO NI STANDARD. Starndard za EU ni kubwa sana, na ndio njia wanayotumia kuprotect soko lao, EVERYONE Knows this, lakini ukisoma mkataba wa EPA hayo mambo ni kama Zero.

Swala la Tanzania kutokusaini EPA ndani ya EAC lisiwe nongwa sana, maana hata kwenye SADC, EU alisaini mkataba na baadhi ya member tu, and Tanzania hakujoin kusaini na bado SADC inaendelea.
 
Nashangaa sana,china wamefuta kodi kwa bidhaa 300 toka Tanzania na zote zinauzika huko.
Tatizo hatuna waziri wa viwanda na biashara wala kilimo,haya mambo ya jumuiya ni kiini mcho tu,walitaka ardhi walipoona haiwezekani wakaamua kusaini kivyao
 
Ni bora kuwa kama uingereza walivyojitoa jumuiya ya ulaya, ukawa huru kufunga mikataba na nchi ambayo/ambazo una nafasi ya kunufaika kiuchumi, na kubaki na mipaka iliyo salama. Wenzetu waliosaini awali walishaona fursa za kunufaika na mkataba wa EPA, kwetu sisi EPA ni kutibua habari zote za kuendeleza viwanda, na kuicha Tanzania ikiwa siyo salama. Kwa hili mimi nasimama na Rais wangu.
Well said, hata Norway walishituka mapema, hata kujiunga hawa kujiunga! MAMA TANZANIA AMEAMKA MILELE!
 
Kwanza EPA haina chochote kipya kwa nchi kama Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan. Kama LDC countries wanapata favorable treatment under WTO kwenye soko la Ulaya without reciprocity. Lakini Kenya is a developing country, kwahiyo hizo favor hazipati.

Kufa kwa EAC sio tatizo, maana Tanzania anafanya Biashara sana na nchi za SADC kuliko nchi za EAC. Tuna ukubwa wa eneo more than the combined other partner states of EAC, we have the highest population more than any country in the EAC., therefore the impact of the collapse of EAC are not so major kwa Tanzania.

Kuhusu EU, japo kuwa tunaexport kwenda Ulaya some primary products, still our major trading partners sio EU, it is China and India. and kwa kenya, Kuna maua anaexport kwenda EU ndo hayo yanampa tabu sana.

The truth is, the deal has very minimimal benefits for LDC, kutokana na fact kwamba, tatizo kubwa ambalo nchi kama za africa zinashindwa kuexport na kucompite kwenye masoko makubwa kama EU, sio mambo ya tariffs, (GSP and GOA). TATIZO NI STANDARD. Starndard za EU ni kubwa sana, na ndio njia wanayotumia kuprotect soko lao, EVERYONE Knows this, lakini ukisoma mkataba wa EPA hayo mambo ni kama Zero.

Swala la Tanzania kutokusaini EPA ndani ya EAC lisiwe nongwa sana, maana hata kwenye SADC, EU alisaini mkataba na baadhi ya member tu, and Tanzania hakujoin kusaini na bado SADC inaendelea.
Nasimama kinyume na roho za wasomi kama wewe mnaowaza ujinga wa kuuziwa bidhaa feki za kichina na kukataa bidhaa imara za EU kwa kisingizio cha kuua viwanda!!!Mbona hata sasa tunatumia kila kitu mchina?Hadi toothpicks ni mchina!Tunanunua minguo haina kiwango,siku tatu tu imechuja tena kwa bei mbaya!Nimenunua viatu kwa sh.laki moja na nusu na sasa ni miezi sita tu soli imekatika na hii ni product ya China!Leo ninyi wasomi mnataka kutuletea ujuaji wa kijinga kijinga tukose bidhaa za kiwango?Unadhani watu wanatafuta mitumba ya nini?Ni kutafuta kitu imara kuliko hii ni fake yenu ya China ingawa na mitumba nayo imeanza kuja feki toka China.Jiangalieni sana na elimu zenu za kichina,mnatu bore sana!!!!
 
Nani kakuzuia kununua bidhaa "imara za EU.?". mbona zipo madukani tu boss,, sema hela huna tu ahahha. The number one trading partner of USA is china, The number two trading partner of Germany, Russia and EU in general is China. India and EU are now negetotiating a trade deal with china, the ASEAN community is also finalizing agreement with china. a single agreement with china, you have accesses to a market with 1 billion people. By the way unaelewa hata maana ya trading partner? it is a two way traffic. Do you want bidhaa Imara kutoka EU? unadhani watu wanaonunua vits na kuacha BMW hawajua kuwa BMW ni imara kuliko vitz? Wananuna because that is what they can afford. Hicho kiatu cha laki moja na nusu kilicho isha ndani ya miezi sita, wajanja wamekuingiza mjini ahahahhaha, yaani usikute huko china wamekichkua sawa na shillingi 2000 za kitanzania. Swala la bidhaa feki kutoka china ni kulingana na uwezo wako wa kuafford vitu. hata iPhones are assembled in china.

China hana limitation kubwa ya standard kama EU, ndo maana it is easy to export to china kuliko kuexport EU.
 
Kwanza EPA haina chochote kipya kwa nchi kama Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi and South Sudan. Kama LDC countries wanapata favorable treatment under WTO kwenye soko la Ulaya without reciprocity. Lakini Kenya is a developing country, kwahiyo hizo favor hazipati.

Kufa kwa EAC sio tatizo, maana Tanzania anafanya Biashara sana na nchi za SADC kuliko nchi za EAC. Tuna ukubwa wa eneo more than the combined other partner states of EAC, we have the highest population more than any country in the EAC., therefore the impact of the collapse of EAC are not so major kwa Tanzania.

Kuhusu EU, japo kuwa tunaexport kwenda Ulaya some primary products, still our major trading partners sio EU, it is China and India. and kwa kenya, Kuna maua anaexport kwenda EU ndo hayo yanampa tabu sana.

The truth is, the deal has very minimimal benefits for LDC, kutokana na fact kwamba, tatizo kubwa ambalo nchi kama za africa zinashindwa kuexport na kucompite kwenye masoko makubwa kama EU, sio mambo ya tariffs, (GSP and GOA). TATIZO NI STANDARD. Starndard za EU ni kubwa sana, na ndio njia wanayotumia kuprotect soko lao, EVERYONE Knows this, lakini ukisoma mkataba wa EPA hayo mambo ni kama Zero.

Swala la Tanzania kutokusaini EPA ndani ya EAC lisiwe nongwa sana, maana hata kwenye SADC, EU alisaini mkataba na baadhi ya member tu, and Tanzania hakujoin kusaini na bado SADC inaendelea.

Mkuu sijaelewa hapo kwenye nchi kama Tanzania Kuwa LDC na kenya kuwa developing country..

Nadhani ni vema ukatofautisha faida na hasara za kutoshirikiana na EU kibiashara kupitia EPA na zile za kutokuwa mwanachama wa EAC.. Unachanganya vitu viwili kwa pamoja!
 
UN ndo anatoa list ya nchi ambazo ni LDC, kwenye hiyo list Kenya hayupo, with the meaning kwamba ameshagraduate na kuwa developing country. Kwa EAC nchi zote ni LDC isipokuwa Kenya tu.
Kama LDC, Tanzania anapata favor, “Everything but Arms” (EBA) initiative, pia hii ipo kwenye nchi kama Australia China, India, Republic of Korea, etc. hii kitu haina reciprocity.

Dunia ya leo, the number one obstacle ya trade, are Technical Barriers and Standards, and EU ndo njia kubwa anayotumia kuprotect market yao. Ukisoma EPA, out of 600 pages, wanasema in issues regarding standards, member states will negotiate in future.

Kuhusu kuchanganya na EAC,, soma vizuri mada husika, inaongelea kuhusu kutokusaini EPA na kuvunjika kwa EAC. ndo maana nikasema hata tusiposaini EPA and EAC ikavunjika, there is less to loose.
 
China watu wake ni zaidi ya 1.3 billion, tukijipanga vizuri soko la china litatutoa, kenya wao wamesha stukia issue hii. Sisi ambao china ni marafiki wa kihistoria tutajivutavuta weee! kenya watatuovateki. Lazima viongozi wetu wajue china si ile ya kijamaa tena wao sasa wanangalia fedha mbele mengine baadaye. Hatuna jinsi kama taifa lazima tujipendekeze kwa china. Hili na lisema, nilishangaa kidogo pale tunapo omba SA watusaidie huko BRICS. Hivi BRICS mwenye sauti kwa kutumia mantiki si China? Sasa sisi tumfikie china au urusi for that matter kwa kupitia kumuomba SA. SA hawa tulio wakomboa juzi kati hapa. Tujirekebishe/tujisahihishe.

Na washawasha!

Nashangaa sana,china wamefuta kodi kwa bidhaa 300 toka Tanzania na zote zinauzika huko.
Tatizo hatuna waziri wa viwanda na biashara wala kilimo,haya mambo ya jumuiya ni kiini mcho tu,walitaka ardhi walipoona haiwezekani wakaamua kusaini kivyao
 
China watu wake ni zaidi ya 1.3 billion, tukijipanga vizuri soko la china litatutoa, kenya wao wamesha stukia issue hii. Sisi ambao china ni marafiki wa kihistoria tutajivutavuta weee! kenya watatuovateki. Lazima viongozi wetu wajue china si ile ya kijamaa tena wao sasa wanangalia fedha mbele mengine baadaye. Hatuna jinsi kama taifa lazima tujipendekeze kwa china. Hili na lisema, nilishangaa kidogo pale tunapo omba SA watusaidie huko BRICS. Hivi BRICS mwenye sauti kwa kutumia mantiki si China? Sasa sisi tumfikie china au urusi for that matter kwa kupitia kumuomba SA. SA hawa tulio wakomboa juzi kati hapa. Tujirekebishe/tujisahihishe.

Na washawasha!
Tutarudi tu China,ni suala la muda
 
UN ndo anatoa list ya nchi ambazo ni LDC, kwenye hiyo list Kenya hayupo, with the meaning kwamba ameshagraduate na kuwa developing country. Kwa EAC nchi zote ni LDC isipokuwa Kenya tu.
Kama LDC, Tanzania anapata favor, “Everything but Arms” (EBA) initiative, pia hii ipo kwenye nchi kama Australia China, India, Republic of Korea, etc. hii kitu haina reciprocity.

Dunia ya leo, the number one obstacle ya trade, are Technical Barriers and Standards, and EU ndo njia kubwa anayotumia kuprotect market yao. Ukisoma EPA, out of 600 pages, wanasema in issues regarding standards, member states will negotiate in future.

Kuhusu kuchanganya na EAC,, soma vizuri mada husika, inaongelea kuhusu kutokusaini EPA na kuvunjika kwa EAC. ndo maana nikasema hata tusiposaini EPA and EAC ikavunjika, there is less to loose.

Asante kwa majibu mkuu. Nadhani kuwa developing country siyo mbadala wa LDC.

Hilo la pili labda nijaribu lugha ya logic:

1.Kutosaini EPA kutaivunja EAC=Hii ni sperculation ya mtoa mada

2. Kwa kusaini EPA bila marekebisho Tanzania inapata hasara - Nakubaliana na hii hoja

3. Kwa kukataa kusaini EPA Tanzania haipotezi chochote (inawezekana sana kuwa hivyo ila wakati utasema. ipo haja ya kulitazama hili si tu kiuchumi ila pia kidiplomasia n.k)

4. Kwa kujitoa EAC kwa sababu yoyote Tanzania haipotezi chochote kwa sababu tuna idadi kubwa zaidi ya watu- Seriously? (Sitaki kuamini kwamba hatuna maslahi yoyote kwenye EAC)

5. Hasara ya kusaini EPA ni kubwa kuliko faida ya kubakia EAC- Sina hakika

6. Kwa kujitoa EAC kwa sababu ya kutosaini EPA Tanzania haipotezi chochote (inategemea mjumuisho wa 1-5)

Wewe umeenda moja kwa moja kwenye 6!
 
Wadau

Salaam Jf

Nimefikiri na kuwaza kwa sauti ya chini sana, nimewaza kwelikweli na sijakosea kuwaza kwa baadae.

Katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Daresalaam juzi juzi kwa malengo ya kujadili mkataba mustakabali wa EPA sambamba na kumkabidhi uwenyekiti Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, katika mkutano huo kwa jina la Mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ulistahili kuhudhuriwa na Marais wenyewe kutokana na umuhimu wake kimaamuzi wakae meza moja wakiangaliana machomacho kutoa ya moyoni mwao, walakini ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni na Mwenyeji wake Rais Dr Magufuli wakati nchi nyingine zilituma wawakilishi kama Mawaziri na Makamo Rais mfano Mh Ruto kutoka Kenya, nchi zilizotuma wawakilishi ni Rwanda, Kenya, Sudani Kusini na Burundi walituma wawakilishi, kwa kuzingatia umuhimu wa mkutano ule katika kuamua kama watasaini mkataba wa mahusiano ya kibiashara kati jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Ulaya yaani EPA au laa, Aidha kwa kuwa mkutano uliopita tayari nchi za Rwanda na Kenya zilisaini mkataba huo kinyume na makubaliano ya jumuiya ya Afrika Mashariki, vilevile kuna habari kwamba nchi za Ulaya zipo tayari kuandaa mkataba mpya wa kufanya biashara na nchi zilizosaini mkataba huo,vile vile machomacho na maombi ya nchi ya Somalia kutaka kujiunga na jumuiya yetu Afrika Mashiriki wote tunajua hali ya usalama usio imara nchini Somalia hususani maeneo ya kiuchumi na kisiasa, ninauliza hivi ni kweli wenzetu tupo nao pamoja kwenye njia moja? au kuna mkono mrefu mchafu wa nusu msafi nusu mchafu? ukizingatia Tanzania imetangaza kuwa ya viwanda, ninavyojua Jumuiya yoyote ya nchi duniani huwa na lengo na maslahi yanayofanana, wajuvi wa mambo ya mahusiano ya kimataifa, uchumi na biashara tufungueni macho mtoe njia mbadala na salama.
EPA ni utapeli wa wakoloni
Full stop!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Na kuhusu Somalia kuwa mwanachama wa EAC binafsi nasema Hapana "No"
Wasituletee balaa
 
Nashangaa sana,china wamefuta kodi kwa bidhaa 300 toka Tanzania na zote zinauzika huko.
Tatizo hatuna waziri wa viwanda na biashara wala kilimo,haya mambo ya jumuiya ni kiini mcho tu,walitaka ardhi walipoona haiwezekani wakaamua kusaini kivyao
Umesema ukweli mtupu, kwanza Tanzania ingejitoa tu kwenye hilo shirikisho la EAC ibaki na SADC tu maana ndio kwenye nchi rafiki wa Tanzania sio nchi hizo maslahi.
 
Waziri wa viwanda Waziri wa fedha na Waziri wa kilimo hawajajua usevikibi maana inahitaji muda sana ni kama paka na panya uvunguni warudi nyumbani kwelikweli
 
Back
Top Bottom