HAbari mtaalam ikikupendeza tupatie na elimu ya MRI.
Wacha nikujibu mm.
MRI( magnetic resonance imaging) hutumia nguvu ya usumaku kutengeza picha.
1. Mwili wa mwanadamu una organ( ubongo, ini, Figo n.k) ndani ya organi kuna tissue na ndani ya tissue kuna cells na ndani ya cells kuna maji n.k
Kama umesoma physics vizuri kuna hii kitu..
Palipo na umeme kuna usumaku pia..
(
jiulize kwa nn mtu anapigwa shots ya umeme? Maana ake na yy ana umeme ndani yake.)
Sasa kwenye maji yaliyo ndani ya cell kuna hydrogen proton ambazo zinazunguka (spin) na hivyo zinakua na usumaku ndani yake..
Na kila organ au sehemu ya mwili ina idadi tofauti ya cell hivyo itakua na kiwango tofauti cha maji na vile vile kiwango tofauti cha hydrogen.
Hizi hydrogen proton huwa zina rotate kwenye position fulani naturally tu...
Sasa
1. Mwilini kuna usumaku
2. Machine ina sumaku
Nn kinafanya picha itokee?
Machine ya MRI hutuma taarifa za usumaku kuja kwenye mwili wa mwanadamu. Usumaku huu hupelekea ule usumaku wa mwili kulalia upande fulani(flip)
Halafu baadae kila sehemu ya mwili kutokana na kiwango chake cha hydrogen itakua inarudi kwenye position yake ya ku spin ya mwanzo kabla haijapata ile sumaku kutoka kwa machine..
Wakati zinarudi kuna kifaa kinaitwa coil hiki ndo huwa kinatuma taarifa na huwa kinapokea taarifa kutoka kwa hydrogen proton zinazorudi kwenye position zao za mwanzo...
Sasa Machine ina uwezo wa kubadili taarifa za usumaku zinazorudi kutoka kwenye mwili na kuwa picha...
Kukiwa na shida labda uvimbe kwenye organ fulani labda ini. idadi ya cell huongozeka, maji yanaongezeka..
Sasa sehemu hii ha uvimbe itakua na sifa tofauti ya cell za ini zilizo nzima..
Hivyo pich itakayokuja sehemu ya uvimbe itaonekana tofauti...
Mwisho kabsa..
MRI ni nzuri kwenye vipimo vinavyohusisha sehemu laini ya nyama( soft tissue)
Kama vile uvimbe, kuangalia ubongo, ini , uti wa mgongo, sehemu za joints..
Huku x ray na CT scan ni nzuri kwenye mifupa
Kuna vitu vingi saana nimejibu japo kwa uchache
Asanteni.