Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286

1
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu mkia wa singa, mrefu kama farasi,
Hatembei kwa kuringa, haruki kibelewasi,
Ya’ni si kama kinyonga, huenda kwa mwendo kasi
Mwanangu siye nyumbu siye.
2
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu sifaye ujinga, ulio pita kiasi,
Mahala pana majanga, hatari hato ihisi,
Mwenziwe apigwe panga, hakimbii hana wasi,
Mwanangu siye nyumbu siye.
3
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu hufata mkumbo, kuhoji yeye hawezi,
Mwisho hufanya utumbo, vituko na upuuzi,
Ndipo kaitwa mtambo, bila mtu hajiwezi,
Mwanangu siye nyumbu siye.
4
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu ana mengi mambo, istizai utalazi,
Kukurupuka hajambo, amemzidi mkizi,
Avuliwa bila chambo, kumpata hana kazi,
Mwanangu siye nyumbu.
5
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu hata wawe kundi, simba ana wasumbua,
Wingi wao si ushindi, mwanangu hilo tambua,
Kupigana si mafundi, mikwara wana ijua,
Mwanangu siye nyumbu siye.
6
Mama mama, sorole nyumbu nyama yetu.
Mwanangu siye nyumbu siye,
Nyumbu haishi ndindindi, fukuza kwa kutimua,
Umbwambie humpendi, hawazi na kuwazua,
Vile siku hazigandi, hilo hataki lijua
Mwanangu siye nyumbu siye.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatsapp 0622845394 Morogoro