kuhusu wale jamaa wa boti waliopotea nakuzama na kufanikiwa kupona mtu mmoja wale jamaa kile kifo cha kujitakia sababu yule aliepona ndio aliwaambia baada ya kuzama wakati wanazama walibahatika kuvaa life jacket ile boti ikaenda chini sasa wao wakabaki wanaelea ndipo yule nahodha akawaambia itabidi tuogelee huku tukifata maji muelekeo wake wale jamaa wengine walikataa ikabidi kila mtu aogelee kivyake isipokuwa yule nahodha aliogelea kwa kufuata maji ndio pona yake yeye aliokotwa kisiwa cha koma akiwa mzima maana aliogelea mpaka ufukweni alipofika kalala hapo hapo mpaka maji yalipokuwa yanajaa ndo yakamuamsha ndo akapandisha juu ndio akapewa huduma ya kwanza nayo ni uji ila wale wengine wenziwe alozama nao hakuna alopona akiwemo mzungu ndio mwenye safari
Ndio hivyo mkuu.Sure inaumiza sana me nilikuja kuona tu mitandaoni ikiwa kama mwezi ushapita so sad.
Umemuuliza swali zuri sana, ngoja arudi kutupa majibu ya kauli hii.Lakini kiongozi,,,Mimi ni BAHARIA,,, na sio mvuvi ,,samahani kwa swali langu,,tunaposoma somo la PERSONAL SURVIVE TECHNIQUES... wanasema inapotokea ajali,,haswa mkiwa na life jackets,,mnapaswa kukaa eneo la ajali ili muweze kupatiwa msaada,,,tena muwe kikundi.,,kuliko kuogelea na kutoka eneo la ajali.....sasa naomba kukuuliza,,hao waliokufa umesema walijitakia,,je kwanini iwe walijitakia?
Umemuuliza swali zuri sana, ngoja arudi kutupa majibu ya kauli hii.
Kwanza kabisa Maji hayana Rangi,,Kwann yale maji ya bahari ni blue?
Ebwana eh ambari vp ushawahi kuigumia
Mm nli bahatika kukutana nayo kilwa ila jamaa walishindwa iuza hapa wa kaenda iuza mombasa
Hebu wape elimu wadau humu kuhusu hiyo kitu
Ova
Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
ni kweli tena ntaleta kisa chake hapa kuna siku wakati tunatega samaki kwa bahati mbaya mtoto wa chongoe alinasa balaa alivyokuja mama yake sitasahau maishaniHalafu Mkuu nasikia kuna samaki anaitwa Chongoe ni mkubwa kama nyumba ni kweli?
Siku akipata muda...😂😂😂Ni lini mwanadamu atai explore Bahari yote?
uko deep sana mpaka huwa nakuogopa kusoma text zako. gombea hata uenyekiti wa kijiji mkataUkishawahi kufika kwenye kile kisiwa karibu na Nyamisati ilipozama meli kubwa ya kivita ya wajerumani?
Jr
nikweli la kurogana la kawaida sana lipo tasi huvuliwa kama samaji wengine wanavyovuliwa kuhusu kondo la nyuma sina hakika ila nia za ushirikina watu hutumia katika uvuvi wengine huua hata mvuvi mwenzao ili wapate samaki (wakojani)chongoe hicho kisa cha chongoe mwana na mama yake nakisubiri. Lakini pia, maajabu ya baharini japo kisa kimoja. Nasikia pia wamiliki wa boti mara nyingi huhusika na ajali kwa ajili ya kurogana ili kurudishana nyuma. Pia kukumbushia swali la mdau mmoja namna tasi anavyovuliwa maana mm hupenda tasi ss kusikia huvulia kwa kondo la nyuma la mama au maiti naanza kujifikiria mara mbili.
Wale jamaa waliozama na kuto patikana sehem waliozama maji yalikuwa yana muelekeo wa kwenda namaanisha visiwa vya koma mapanya mpaka nje ya buyuni kabisa na ndio maana wale watafutaji walikuwa na vifaa tu ila ujuzi wa utafutaji hawawana
Viumbe gani, mzeeMimi nishajishugulisha na uvuvi wa jongooo
Katika harakati zangu sijawahi kuthibitisha kuhusu nguva, licha ya kukutana na vitu na viumbe wengine kutoka baharini
Ova
Iwe bojo.Bahari kwa kihaya inaitwaje?
Habari zenu waungwana,
Leo nipo hapa kwa ajili ya maswali ambayo yanahusu mambo ya bahari tu. Mimi ni nahodha wa majahazi ya mizigo Mafia, Kisiju, Kilwa, Nyamisati na Koma.
Uliza swali linalohusu maeneo hayo pia kuhusu safari na vimbwanga vya baharini.
Karibuni.