Ulisha wahi ingizwa mjini (Kutapeliwa)

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Eleza ilikuaje.
Mimi nilitapeliwa dumu zima la mafuta ya kupikia ambayo mdingi aliniagiza nikayachukue kwa rafiki yake mmoja kibamba. Sasa nilivyofika nayo k.koo, ndio mchezo ulichezeka hapo. Nakumbuka nilikuwa form two

Jamaa wa toroli alikuja niomba anibebee kwa jero. Sasa ikawa kuvuka barabara, jamaa akavuka fasta, ile anavuka tu ikaja gari ya mnazi mmoja ikapaki katikati yangu, mpaka kuja kugeuka gari nivuke jamaa simuoni tenaa.

Mziki ikawa nitamwelezaje Mzee mana mzee ni mkali vibaya. Nilivyofika Om nikamwambia gari imepata ajali, polisi wameipeleka kituo cha polisi pale Usalama hivyo tumeambiwa kila mtu akachukue vitu vyake kesho, akasema ayaa tutaenda wote

Sasa usiku ukawa unakaribia huku nikijiuliza hiyo kesho itakuwaje. Ikanibidi kidume nimweleze ukweli, kuwa nimetapelia.

Mdingi alinijibu ayaa. Dah sikuamini yani mana nilijua nakufa siku hiyoo

Mpaka leo sijawahi tapeliwa kabisa.
 
Sijawahi tapeliwa kiihivyo labda tu jamaa zangu ambao nafahamiana nao vizuri anakukopa then hakulipi... hizo kwangu ni nyingi sana.
 
Na unjanja wangu wote niliwahi kuuziwa ALL STAR uozo kwa elfu 8 maeneo ya msimbazi street, nilivyofika home kufungua mfuko nilijicheka wiki nzima maana ni utapeliwa wa kitambo ambao nimekuwa nikiona wengi sasa sijui mimi nilijisahau vipi.
 
Niliuziwa net nikiwa b.bar pale sinza kufika nyumban naifungua kalikuwa kadogo balaa labda kitanda cha mtoto mchanga
 
Mimi jamaa leo kaniuzia FLASH YA SAMSUNG 64GB(ikiwa packaged) sh. Elfu 10 tu... alivyoondoka tu Nikashtuka huenda kanitapeli ila nikacheki baadae kitu OG.
 
Nilitapeliwa kkoo, nimenunua viatu kufika nyumbani vyote vya kulia, mara ya pili nikanunua suruali nilivyofika home nikakutana na dekio ama kweli mjini chuo kikuu
 
Ogopa wale wanaojifanya wanauza vitu kwa mnada.
Usithubutu kusimama.utalizwa mpaka hela ya futari
niliuziwa flash feke mkuu moja 10,000
Nikicheki kwenye computa inasoma 64GB lkn haiingizi hata mziki wa 10m.

Alafu kwa hasira nilinunua nyingi ili nikaziuzee

dah
 
Nilibadilishana na mshikaj flani hivi iPhone. Nikampa iPhone 5s Og yeye akanipa iphone 7 plus fake. Nakumbuka nilicheka sana kwa hasira. Ila ile iPhone nikajakuifunga iCloud lost mode siku ile ile.
 
hahahha
alie uza cheni ya dhahabu fake, kapokea ela fake
 
Back
Top Bottom