Hadi imefikia hatua Israel inatuma watoto wa kike kuishughulikia Iran ni dharau kubwa sana hii.
Lingekuwa ni balaa zito mno wangetumwa wale wazee wa kazi walionyakua helikopta ya Rais wa Iran, kumtegea bomu chini ya kitanda kiongozi wa Hamas akiwa Iran, Kuwahangaisha kina Yahya kutupia vijiti drone, n.k. ilibidi mabinti wapewe nafasi kupunguza uzito wa mashambulizi.
Jeshi la Israel liliingia na kutoka Iran bila ndege yake hata moja kuguswa, shambulio lilikuwa la awamu tatu kwa idadi ya ndege jumla ya 100, Awamu ya kwanza zilitumwa takribani ndege 35 kuichakaza mifumo ya ulinzi wa anga ambayo kwa kiasi kikubwa ni mitambo ya S 300 ilinunuliwa urusi, baada ya hapo anga likawa wazi, Israel waliingia na kuvilipua viwanda vya drones na makombora
Kuna zile video zinasambaa Ndege za Israel zinatamba kwenye anga la jij kuu la Tehran, Mifumo ya ulinzi imejiwasha inapiga hewa utadhani fataki, Lile sio jambo la kushangilia, Ni matusi makubwa sana yale kwa Iran, Jeshi la Iran liliogopa kutumia marubani wao wapigane na ndege za Israael wamejificha wanategemea mifumo ambayo haikuweza kudungua ndege za Israel, marubani wa wangeamua kufanya chochote Tehran hakuna ambacho kingewazuia.
IRAN IMEKIRI:
- Idadi ya askari wake waliouawa imeongezeka 2 hadi 4
- Mifumo ya ulinzi wa anga imeteketezwa
- Viwanda cha makombora vimelipuliwa
- Viwanda cha drones vimelipuliwa