Ulinzi na usalama: Teknolojia rahisi inavyofanya kazi kwa urahisi

Safety and Security

New Member
Mar 8, 2016
1
0
Umejenga mwenyewe nyumba nzuri, katika mandhari nzuri unayoweza kuona Bahari ya Hindi. Lakini jijini Dar es Salaam pia ni mahali ambapo uhalifu unazidi kukua siku hadi siku. Unaamua kuimarisha ulinzi kwa kuweka magrili katika milango na madirisha yote nyumbani kwako.

expandable-barrier-application-slide-1-jpg.328481

Unahisi uko salama sasa kutokana na hatua uliyochukua kuongeza ulinzi, hadi pale unapokumbuka kuwa kuna ajali zingine zaweza kutokea na ulinzi uliojiwekea ukakuponza. Unawaza, ''Hivi moto ukizuka ghafla na ninahitaji kutoka haraka itakuwaje?''.

Je, wajua kuwa kuna aina za grili zinazoweza kukunjwa? Aina hii ya magrili ni yale ambayo yanakupa ulinzi imara wakati unapouhitaji, lakini yanaweza kukunjwa au kuwekwa kando wakati huhitaji ulinzi wake, mfano pale unapotaka kutizama uzuri wa mandhari iliyokuzunguka au wakati wa hatari unapotaka kutoka haraka.

expandable-barrier-application-slide-2-jpg.328482

expandable-barrier-application-slide-3-jpg.328483

Haya, sasa umeweza kutatua tatizo la grili kukuzuia utakapotaka kujiokoa na ajali mathalani ya moto. Lakini unawaza tena, “Hawa jamaa siku hizi wanatumia njia mbalimbali kuvunja makufuli. Wanatumia mashoka na zana nyingine nzito, na kila kukicha wanabuni namna mpya za kutuingilia majumbani mwetu, madukani na hata katika maghala”

Unafahamu kuwa kufuli aina ya MUL-T-LOCK ni zenye ubora wa hali ya juu? Ni aina ya kufuli zisizovunjwa kirahisi. Unafahamu kuwa MUL-T-LOCK pia wanakupa aina za kufuli zilizounganishwa na mfumo wa GSM/GPS (mfumo wa kutambua eneo ulipo) zinazofanya kazi kwa msaada wa satellite?

eseries-padlock-high-security-sliding-bolt-sbe10_jpg-jpg-p0x0-q85-m400x0-framenumber-1-jpg.328484

cseries-padlock-series_jpg-jpg-p0x0-q85-m1020x420-framenumber-1-jpg.328487

watchlock_with-cliq-key_jpg-jpg-p0x0-q85-m204x140-framenumber-1-jpg.328485
watchlock_mtl-side-bottom-view_jpg-jpg-p0x0-q85-m204x140-framenumber-1-jpg.328486

Ubora wa kufuli hizi hauwezi kulinganishwa na kufuli aina zingine hata kidogo. Jinsi watu watakavyozidi kutambua umuhimu wa kufuli hizi, ndipo tutakapozidi kukandamiza mipango ya wahalifu kuchukua vitu vyetu vya thamani.

“Sababu ya kuwepo kwa bidhaa hizi ni kuhakikisha kuwa wewe pamoja na vyote unavyovithamini mpo salama usalimini. Si hayo tu, bali pia kufanya hivyo kwa ubunifu na ufanisi wa hali ya juu kabisa. Teknolojia hii inakua kwa kasi nchini Tanzania, huku sisi tukiwa tunaongoza katika kuzisambaza bidhaa zinazotokana nayo.”

“Tunategemea kwamba katika miaka ya mbeleni, elimu juu ya usalama itazidi kukua na kukubalika nchini”, haya ni maneno ya Mufaddal Jariwalla, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji katika kampuni ya Safety and Security Centre Tanzania, wasambazaji wa grili hizi za pekee na kufuli zenye ubora wa hali ya juu.

Uhalifu upo katika mitaa yetu kila siku. Badala ya kujuta na kusema “endapo wangekuwa na magrili” au “endapo wangetumia kufuli bora”, ni vema tuchukue maamuzi sasa kabla hatujachelewa. Kama wahenga walivyosema, “Kinga ni bora kuliko tiba”.
 
Attachments

  • Expandable-Barrier-Application-Slide-1.jpg
    Expandable-Barrier-Application-Slide-1.jpg
    81.7 KB · Views: 505
  • Expandable-Barrier-Application-Slide-2.jpg
    Expandable-Barrier-Application-Slide-2.jpg
    79.8 KB · Views: 295
  • Expandable-Barrier-Application-Slide-3.jpg
    Expandable-Barrier-Application-Slide-3.jpg
    79.1 KB · Views: 297
  • E‑Series Padlock High Security Sliding Bolt - SBE10_jpg.jpg@p0x0-q85-M400x0-FrameNumber(1).jpg
    E‑Series Padlock High Security Sliding Bolt - SBE10_jpg.jpg@p0x0-q85-M400x0-FrameNumber(1).jpg
    11.2 KB · Views: 255
  • WatchLock®_with CLIQ key_jpg.JPG@p0x0-q85-M204x140-FrameNumber(1).jpg
    WatchLock®_with CLIQ key_jpg.JPG@p0x0-q85-M204x140-FrameNumber(1).jpg
    4.7 KB · Views: 237
  • WatchLock®_MTL side bottom view_jpg.JPG@p0x0-q85-M204x140-FrameNumber(1).jpg
    WatchLock®_MTL side bottom view_jpg.JPG@p0x0-q85-M204x140-FrameNumber(1).jpg
    3.9 KB · Views: 244
  • C‑Series Padlock Series_jpg.jpg@p0x0-q85-M1020x420-FrameNumber(1).jpg
    C‑Series Padlock Series_jpg.jpg@p0x0-q85-M1020x420-FrameNumber(1).jpg
    22.2 KB · Views: 272
Umejenga mwenyewe nyumba nzuri, katika mandhari nzuri unayoweza kuona Bahari ya Hindi. Lakini jijini Dar es Salaam pia ni mahali ambapo uhalifu unazidi kukua siku hadi siku. Unaamua kuimarisha ulinzi kwa kuweka magrili katika milango na madirisha yote nyumbani kwako.

Unahisi uko salama sasa kutokana na hatua uliyochukua kuongeza ulinzi, hadi pale unapokumbuka kuwa kuna ajali zingine zaweza kutokea na ulinzi uliojiwekea ukakuponza. Unawaza, ''Hivi moto ukizuka ghafla na ninahitaji kutoka haraka itakuwaje?''.

Je, wajua kuwa kuna aina za grili zinazoweza kukunjwa? Aina hii ya magrili ni yale ambayo yanakupa ulinzi imara wakati unapouhitaji, lakini yanaweza kukunjwa au kuwekwa kando wakati huhitaji ulinzi wake, mfano pale unapotaka kutizama uzuri wa mandhari iliyokuzunguka au wakati wa hatari unapotaka kutoka haraka.

Haya, sasa umeweza kutatua tatizo la grili kukuzuia utakapotaka kujiokoa na ajali mathalani ya moto. Lakini unawaza tena, “Hawa jamaa siku hizi wanatumia njia mbalimbali kuvunja makufuli. Wanatumia mashoka na zana nyingine nzito, na kila kukicha wanabuni namna mpya za kutuingilia majumbani mwetu, madukani na hata katika maghala”

Unafahamu kuwa kufuli aina ya MUL-T-LOCK ni zenye ubora wa hali ya juu? Ni aina ya kufuli zisizovunjwa kirahisi. Unafahamu kuwa MUL-T-LOCK pia wanakupa aina za kufuli zilizounganishwa na mfumo wa GSM/GPS (mfumo wa kutambua eneo ulipo) zinazofanya kazi kwa msaada wa satellite?

Ubora wa kufuli hizi hauwezi kulinganishwa na kufuli aina zingine hata kidogo. Jinsi watu watakavyozidi kutambua umuhimu wa kufuli hizi, ndipo tutakapozidi kukandamiza mipango ya wahalifu kuchukua vitu vyetu vya thamani.

“Sababu ya kuwepo kwa bidhaa hizi ni kuhakikisha kuwa wewe pamoja na vyote unavyovithamini mpo salama usalimini. Si hayo tu, bali pia kufanya hivyo kwa ubunifu na ufanisi wa hali ya juu kabisa. Teknolojia hii inakua kwa kasi nchini Tanzania, huku sisi tukiwa tunaongoza katika kuzisambaza bidhaa zinazotokana nayo.”

“Tunategemea kwamba katika miaka ya mbeleni, elimu juu ya usalama itazidi kukua na kukubalika nchini”, haya ni maneno ya Mufaddal Jariwalla, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji katika kampuni ya Safety and Security Centre Tanzania, wasambazaji wa grili hizi za pekee na kufuli zenye ubora wa hali ya juu.

Uhalifu upo katika mitaa yetu kila siku. Badala ya kujuta na kusema “endapo wangekuwa na magrili” au “endapo wangetumia kufuli bora”, ni vema tuchukue maamuzi sasa kabla hatujachelewa. Kama wahenga walivyosema, “Kinga ni bora kuliko tiba”.
Staili nzuri sana ya kutangaza biashara!
 
biashara matangazo ni kweli lakini ingekuwa bora zaidi ukaweka na picha tuzione
 
Hahaha! Vipi mkuu mbona washangaa? Umeona vitu hivyo!?
Lakini haya magrill kama sio ya 'kichina' yanaonekana ni madude flani hivi amazing!Lol
Tehe tehe...nimebaki nakodoa macho tu mkuu Kama pimbi ndani ya box.
 
Back
Top Bottom