Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,614
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mshana Jr amekuwa msaada mkubwa kwangu kwenye kujifunza mambo mengi. Nami sasa naona nianze sasa kuwafundisha wengine ..
ULIMWENGU WA 3D NA 4D
Unajua kila mtu anaishi katika sehemu mbili; katika ulimwengu wa 3D na katika ulimwengu wa 4D. D= Dimension. / mwonekano
Katika ulimwengu wa 3D ndio huu unaoniwezesha sasa naandika haya kwenye kompyuta na nikiangalia ninaona jua magari na tunaenda shule kusoma nk. Ni ulimwengu huu ambao umeuzoea siku zote tuna kula na kunywa. Katika ulimwengu huu tunatumia macho mawili na huku tunashangaa kwanini watu wengine wanafanya miujiza wakati sisi wengine hatuwezi? Au kwanini watu wengine wanatabiri wakati sisi hatuwezi?.
Hawa watu wanaweza wakafanya hivyo kwa sababu wanaweza wakatumia jicho la tatu ambalo mtu akiwa mtoto mdogo au mchanga huwa lipo very active. Na kadri anavyozidi kuwa mkubwa jicho hilo hufumbwa na kufanya asiweze kuona tena vitu vilivyo kwenye 4D.
Watu wanafanya mambo hayo ni kwa sababu wanauwezo wa kufumbua jicho la tatu na kuona vitu vilivyo kwenye 4D. Huo uwezo wa kufumbua hilo jicho ndio unaosababisha watu wanafanya miujiza wanatabiri na wanafanya vitu vingi ambavyo havionekani.
Kwa sababu mtu amefumba jicho hilo kwa mda mrefu huwa inamchukua mda kuwa na uwezo wa kulifumbua jicho hilo. Lakini kwa maelekezo maalumu jicho hilo linaweza likafumbuka. Jicho la tatu linakufanya uone ulimwengu mwingine tunaoishi sisi ambao ni mzuri sana. Tofauti na huu ambao umeharibiwa na watu wachache. Mantiki ya sisi kuwepo ni kuufanya ulimwengu huu ufanane na ulimwengu ulio kwenye 4D. Uoga na kuogopeshwa kumewafanya watu wasiweze kabisa kuingia katika ulimwengu huo.
Nitajaribu kueleze jinsi ya kuingia katika ulimwengu huo hatua kwa hatua na ndipo sasa utaanza kujielewa wewe mtu ni wa namna gani? Je! ni nguvu gani uliyo nayo ambayo umefungwa na watu wachache walioweka kanuni zao ili wewe upumbazike.
*Jicho la tatu ndilo linalotufanya tuone vitu kwenye ulimwengu wa 4D*
Kwa sababu ni mda mrefu sana haujawahi kulitumia jicho hilo ni vyema kuanza kufanya mazoezi jinsi ya kulitumia. Tafuta sehemu iliyotulia. ambayo hakuna kelele kelele. Au ikiwezekana jifungie chumbani na uzime taa. Hatua utakazo fanya ni unakaa vizuri mikono yako weka kwenye magoti.
Fumba macho yako haya mawili. Kaa kimya kwa mda wa dakika kama 6 - 10 hivi. Vuta hewa kwa kutumia pua na itoe kwa kutumia mdomo. Fanya hivyo taratibu taratibu. wakati mwingine ukiwa unaanza utasikia kichwa kinauma. Usihofu hiyo ni kawaida.
Anza kutoa sauti kwa taratibu ukisema MEYIIIIIIIIIIIIII, MEYIIIIIIIIIII. Bada ya mda jicho la tatu litaanza kufunguka taratibu. Kwa sababu mda mrefu hujawahi kulifumbua utaona giza giza vitu vitu usivyo vielewa. Fanya hivyo kwa mda wa wiki mbili tayari utakuwa umezoea utaanza kuwa na uwezo sana.
Utaanza kujua vitu vingi sana na kuanza kujielewa sasa wewe ni nani na una nguvu gani. Nitakueleza siri hiyo wanatumia akina nani na inaleta matokeo gani. Hakuna uchawi hapa mtu asikudanganye. Ni wewe tu jinsi ya kujielewa.
Karibu tuujifunze kwa pamoja (theory na practical)
Updates
Je Utambuzi ni nini?
Kujitambua maana yake kukua kimwili, kiakili, kihisia na kiroho kwa njia ambayo itakusaidia wewe na watu wanaokuzunguka. Ni kuachana na mazoea, kuachana na akili ya kupewa (inayokuumiza au inayowaumiza wengine), kuwa na akili yako (isiyokuumiza au isiyowaumiza wengine). Kumbuka, tunapojifunza maarifa haya, hatuzungumzii dini wala sayansi, tunazungumzia maarifa ambayo yako juu ya hivi. Ingawa kuna mahali ambapo dini na sayansi inatumika kama rejea.
Tunajifunza Maarifa haya ya utambuzi ili:
· Yatusaidie kumudu kukabiliana na vikwazo na vurugu za maisha.
· Tuyaone maisha kwamba ni mepesi na siyo mzigo. Tuweze kuyaona maisha katika upande wa pili.
· Tuwe na amani, furaha na ridhiko la kweli katika maisha.
· Tuweze kuishi katika maisha ya uhitaji na siyo utashi.
· Tuweze kufahamu kwamba sisi siyo huu mwili unaoonekana, na hivyo tuishi sisi kama sisi na siyo sisi kama mwili huu unaoonekana.
· Yatuwezeshe kumudu kufanya mambo kama sisi na siyo kama baba, mama, shangazi, mjomba, jamii au watu wengine. Sisi ni kasuku au roboti wa baba/mama au jamii. Jiulize kila unachofanya kama hufanyi kile kile alichokuwa anafanya baba/mama au kama hufanyi kwa ajili ya jamii.
· Tuweze kuishi maisha halisi kwani haya tunayoishi siyo halisi, ni ya bandia.
Tunapata matatizo mengi kwa sababu tunaamini sisi ni huu mwili unaoonekana, tumejifunga sana na huu mwili (tumekuwa wafungwa wa mwili). Ndiyo maana unapofanya jambo baya unasingizia ibilisi. Huyu ibilisi ni nani/nini?
Upo msemo unaosema kuwa “Ibilisi wa mtu ni mtu mwenyewe” Kwa nini? Kwa sababu Ibilisi hawezi kutoka nje yako bali anatoka ndani yako, yaani kila mtu anao uwezo wa kudhibiti mambo mabaya dhidi yake. Kwa hiyo ukitokewa na jambo baya umejitakia, hakuna wa kumlaumu bali ni wewe mwenyewe.
Ebu tumwangalie kwanza mtoto; kwa kawaida mtoto anapozaliwa huwa hana utambuzi, hajui yeye ni nani. Kitu cha kwanza anachokibaini ni vitu vingine (vya nje). Macho hufunuka kuangalia mbele, mikono hushika watu au vitu vingine, masikio husikia watu au vitu vingine, ulimi huonja chakula na pua hunusa watu au vitu vingine. Milango yote mitano ya fahamu hufunguka, yote ikiwa inahusiana na vitu vya nje.
Mtu wa kwanza kumtambua ni mama yake na siyo yeye (hajijui). Baadaye hutambua mwili wake (ambao pia ni nje yake). Mwili huhusiana na dunia hii ya nje. Akiwa na njaa hulia ili anyonyeshwe kuulisha mwili wake, akiumwa hivyo hivyo. Akishiba au kupona,
huusahau mwili wake, hana habari nao tena.
Mama huanza kumwambia yeye ni nani, huanza kumsifu au kumkaripia. Akisifiwa wewe mtoto mzuri, hutabasamu na kujisikia vizuri, huhisi kukubaliwa na kujiona mwenye thamani. Hapa ndipo choyo cha kujipenda huanza (huzaliwa). Choyo (ubinafsi) ni ile tabia ya kutotaka kutoa kitu kumpa mwingine (tabia ya kunyima). Hapa ndipo mtoto
huanza kujitambua kuwa yeye ingawa kujitambua huku ni taswira ya kujitambua, siyo halisi.
Bado hajawa yeye halisi, anachojua ni wengine wanasema nini kuhusu yeye. Lakini kama hakuna anayemjali na kumuonyesha kwamba ana maana, ana thamani hapa napo choyo kingine cha kujipenda huzaliwa, lakini hiki ni choyo cha ubaya; visasi; huzuni; kukataliwa; kujihisi dhaifu, mnyonge na asiye na thamani. nk
Hivyo anaanza mama; baba; dada; wajomba; shangazi; msichana wa kazi; majirani; walimu; marafiki n.k. wote humwambia yeye ni nani; Hapa mtoto huchanganyikiwa kwani maoni kuhusu yeye ni nani huongezeka, huwa tofauti na mengi zaidi kutegemea chanzo yalipotoka.
Kama mtoto angeishi peke yake bila kukutana na watu asingekuwa na choyo cha kujipenda zaidi lakini asingejitambua kikweli (yeye kikweli) angekuwa kama mnyama ambaye hana choyo cha kujipenda. Choyo cha kujipenda zaidi ni hitaji (hitaji la kijamii). Kila kitu kinatuambia sisi ni nani, siyo sisi kujiambia sisi ni nani, hatuwezi kujiambia sisi ni nani kwa sababu hatujui kwamba tupo.
Wahuni, marafiki, na majirani ndiyo wanaokuambia wewe ni nani, hivyo hatua kwa hatua kila mmoja anaboresha choyo chako cha kujipenda zaidi; kila mmoja anajaribu kukirekebisha na kukiboresha choyo chako ili usiwe tatizo kwa jamii. Hivyo wewe ni jamii na siyo wewe kwa sababu kuanzia mama; marafiki; walimu n.k; ndiyo waliokuambia wewe ni nani.
Umefungwa sana na jamii; kiasi kwamba kuwa wewe siyo jambo rahisi kiasi hicho. Unakula kwa sababu wengine wanakula; unavaa suti kwa kwa sababu wengine wanavaa; unakwenda kuzika kwa sababu wengine wanakwenda, unalia msibani kwa sababu wengine wanalia; unakwenda msikitini / kanisani kwa sababu wengine wanakwenda- huwezi tena kuwa wewe kwa sababu ya hicho choyo.
Mfano: mtu akiua mtaani mtu mmoja anaitwa hatari sana; mwingine akaua vitani watu laki moja anaitwa shujaa. Jamii imekubali kuua vitani ni sahihi; mtaani siyo sahihi; jiulize swali hili ili uone jamii ilivyokufunga na hivyo ni ngumu kuwa wewe. Umekuwa jamii tangu kuzaliwa kwako. Kinachokubaliwa na jamii ndiyo sahihi hata kama kinanuka kiasi gani. Hicho ndicho unachotakiwa kuwa kwa sababu wewe ni jamii na siyo wewe.
Hutakiwi kuwa wewe, na ukiwa wewe jamii itakutema mara moja. Ukweli unatakiwa uwe nao wewe na siyo jamii. Lakini bahati mbaya hujawahi kuwa wewe, siku zote umekuwa jamii, hivyo unasikiliza Inasemaje kuhusu wewe na inakutaka uishi vipi. Ukiwa wewe jamii itaona umeasi au umekuwa kichaa.
Jamii haitaki ujitambue (ujue wewe ni nani). Ukijitambua utakoma kuwa jamii na jamii haiko tayari kukupoteza mtumwa wake. Jamii inakutumia kwa faida ya jamii. Ukiwa wewe jamii haiwezi kukutumia itakavyo. Ukifanya jambo zuri unapendwa na kusifiwa; na ukifanya jambo baya unachukiwa na kubezwa. Hii hujenga choyo cha kujipenda zaidi ambacho hutaka kushibishwa kila siku.
Mtu atajitahidi kufanya kile ambacho jamii inampangia ili kushibisha choyo alichopewa na jamii husika. Atataka gari na nyumba kwa sababu jamii imemwambia ni vya maana na vinampa thamani siyo kwa sababu yeye anavitaka. Atataka digrii, mke mzuri, utajiri, umaarufu yote ikiwa ni choyo alichopewa na jamii.
Kila siku tunatafuta sisi ni akina nani kupitia kwa watu wengine, wakituona kututambua, kutusifia ndipo tunahisi kuwa sisi. Jamii inayumba kila siku kuhusu kipi ni kipi na hivyo na sisi tunayumba kila siku kwa sababu sisi ni jamii. Kumbuka wakati unazaliwa ulishakuwa wewe na uwewe wako bado unao. Lakini kwa sababu umepewa uwewe mwingine na jamii ndiyo maana kuchanyikiwa na kujuta ni kwingi sana.
Ni hadi hapo utakapovua uwewe uliopewa na jamii na kubaki na uwewe uliozaliwa nao (kuwa wewe halisi), ndipo kuchanganyikiwa na kujuta kutaisha. Inawezekana!!!
Binadamu anahangaika sana na maisha. Anatafuta mambo ya nje (gari, pesa, mke mzuri, mume anayejali, elimu n.k.) ili yampe nafuu (furaha, amani na ridhiko). Lakini, anapoyapata anajikuta hayampi nafuu badala yake yanampa maumivu.
Mambo ya nje hayawezi kutupa nafuu hadi tuingie ndani yetu (ni wapi huko?). Tutapata jibu kwa kadri tunavyoendelea kujifunza maarifa haya vizuri zaidi, na hatimaye tutajijua sisi kama sisi na siyo sisi kama mwili huu unaoonekana, hisia, mawazo (akili) au roho. Ni vema kutazama miili (nyumba zetu) hiyo kwani ndiyo ambayo itatusaidia kujua hasa ni wapi tuendako kwenye maisha haya na pengine kujua maisha haya yana maana gani kwetu. Hii inaweza kutupunguzia mizunguko na mahangaiko ambayo kiukweli hayana maana.