Umesema kweli shemeji. Nakumbuka marehemu babu yangu alikuwa mkali, ikitokea akaona tumetupa hata tonge moja fimbo zake sio za kawaida!!!!Nyumbani chakula hakimwagwi kamwe, nakumbuka enzi hizo watoto, ukipigwa ugali ukabaki, mtaula baadae au wakati wa kusonga ugali mwingine ule utatangulizwa kwenye maji mnaongezea unga kigogo.
Kama ni mihogo, italowekwa kwenye maji ili isiharibike na mtaimaliza tu, ole wako ukamatwe umemwaga chakula.
Na wakati niko Boarding tulikuwa na sera ya The Share Provided Must be Finished, hii mpaka leo naendelea kuitumia.
Hetu ni nyika, zaidi nee mbure na ngokoro hahahahahah kana kishumba cha mimanga hahahahavhishumba vha itendera
Kweli mkuu pia inasaidia pale unapoenda kuishi mazingira tofauti yenye aina tofauti ya watuThe way mama yako alivyokueleza matumizi bora ya misosi ndivyo ninavyowaelekeza wanangu. Namshukuru Mungu tunajiweza kiuchumi, ila hii haimaanishi kwamba tuwe tunafuja chakula kwa kuwa tu "KIPO". No way. Huwa nawaelekeza wanangu kwamba wapakue chakula kile wanachoweza kula bila kusaza chakula "KINGI". Pale mnapokwenda kumwaga kwenye debe la taka unakutana na watu walilala njaa, wakiona mmemwaga huwa inawauma sana. Unakuta mtu kapakua sahani imejaa mpaka pa kuweka kipaja cha kuku hakuna, then anakula robo ya alichopakua. Inakera sana.