Hebu tupe mbinu(mbuni) sisi wanachuo ambao pamoja na kutokwenda club ili kusave pesa bado tunashindia mihogo na hatuna kitu
We really need your 2019 tactics mkuu[emoji120][emoji120]
Masikini watoto wa wakulima mnawaiga watoto wa vibopa kuishi ?
Ishi maisha yako achana na mambo ya eti lazima niwe na code kali
Achana na simu za gharama ukiwa na PC basi kiswaswadu ndiyo habari ya mjini.
Oya wewe bado huna hela hizo laki tano na kumi zisikutoe akili kwa hiyo miezi miwili unayoipokea achana na habari za kupanga chumba eti unajipanga na maisha .Maisha gani hayo ? Wakati mkimaliza vitu mnauza ili mpate nauli kurudi vijijini kwenu?
Pambana upate hosteli ili uwe na uhakika wa kulala kwani wamama wauza vyakula vya buku huwajui ? Kale huko achana na habari za chipsi yai maana hata kwenu hukuwahi kula hivyo.
Oya dogo , laki mbili ni kubwa sana kwa wewe kula miezi miwili kabla ya bumu lingine na pia kulipia hizo hosteli kila mwezi elfu thelathini ambavyo mkishare ni kumi na tano
Dogo wewe mjini ni wa kuja hivyo tuliza akili achana na motivational speaker et tafuta biashara uanza wewe dogo pambana kutunza hicho kidogo kwanza mpaka kiwe kikubwa walau.
Dogo najua una hamu ya kugegedana , bwana mdogo achana na ushenzi wa kuwa na maslay queen tafuta kabinti kashamba kama wewe ambako mtaendana hata siku ukikatoa out basi elfu mbili iwatoshe kunywa soda na kurudi magetoni akupe mzigo.
Dogo hapo ni shule sio kwenye ajira ule upuuzi wako wa kuwatumia ndugu zako hela acha mara moja , Maana bumu likikata hawajawahi kukutumia hata nusu ya ulichowahi kutuma.
Bwana mdogo sio kila mwanafunz ni mwanafunzi hivyo acha shobo na usiowajua sio kila mtu awe rafiki yako .
Dogo ulikuja kusoma au kushindana kuvaa na kwenda bar au Play station Games?
Piga kitabu bwana mdogo kilichokuleta ni hicho tu sio hayo maigizo.
Dogo mambo ni mengi mda ni mchache niache nikawachome sindano wanakijiji ila nikusisitize ukitakata ufanikishe lengo la kuitunza hela anza na kutizama majengo mazuri yote mjini jiulize ni nani pale kwenu analo ikiwa hamna basi jua kwenu ni masikini wa kutupwa acha kuiga pambana uondoe laana ya ukoo wenu.
Pole nimeandika haraka niko na wamama labour na pia nisamehe kwa lugha ngumu ni haraka tu ila mimi ni mstaarabu.
Natanguliza shukrani.