Ulevi noumaaaa

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,402
Reaction score
12,794
Jamaaa kapoteza mali zoote na akawa masikini wa kutupwa sababu ya ulevi. Siku moja akapita karibu na dampo na kuona chupa za bia..Kwa hasira akachukua ya kwanza na kuipasua akisema " kwa sababu yako nimeachana na mke wangu!"
Akapasua ya pili akisema " Kwa sababu yako nimeshindwa kusomesha wanangu!"
Akapasua ya tatu kwa hasira akisema " kwa sababu yako nimefukuzwa kazi!"
Akapasua ya nne akisema," Kwa sababu yako nimeuza mali mali zangu zote hadi nikafilisika!..
Akachukua ya tano akakuta haijafunguliwa imejaa bia,akaiweka pembeni akisema " Kwanza huu ugomvi haukuhusu,tutaongea baadaye kwanza unaonekana huna tabia mbaya km wenzako!
 
Lol huyo mlev mbona kama namjua vile haha mapombe hayo saafi atajifunza

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ahaaaa we jamaa umetisha kinoma kaka.kwa hiyo ugomvi unazihusu tupu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…