Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 55,027
Baada ya rais John Magufuli kuchaguliwa na kushika madaraka katika awamu ya tano aliteuwa wakuu wa wizara mbali mbali hapa nchini kila wizara ikipewa waziri wake.
Baada ya kuapishwa kwa mawaziri hao kila mmoja alianza kukimbiza upepo katika wizara yake wapo ambao hawakuisha kuandikwa katika magazeti na vyombo vya habari hapa nchini.
Kadri muda ulivyozidi kwenda kasi hiyo naona inazidi kushuka na wale mawaziri ni mara chache sana kuwasikia wakifanya ziara za ghafla kama pale awali wakati wizara zao zikiwa mbichi, Wizara ya Afya, Nishati na Madini, Elimu, na baadhi ya wizara ni moja kati ya wizara ambazo zilikuwa hazilazi damu kuandikwa katika front page ya magazeti hapa nchini.
Kilichofanya kuandika uzi huu ni kuona ukimya wa wale wazari na manaibu waliokuwa na matamko kipindi kile, kusimamisha watu, kufungia mageti wafanyakazi wachelewaji na mara nyingine fukuza fukuza yao.
Najiuliza na ninawaza kwa sauti ile nguvu ya soda ninayosikia ndio hii iliyotumika toka kuapishwa kwao na kuisha kabla ya safari?
Mbona baadhi yao wapo kimya hata kwenye vyombo vya habari nini dhima ya ukimya wao kwa kipindi chote hicho?
Mbona baadhi ya wizara hazijawahi hata kusikika zipo kama hazipo je hawa walioteuliwa wanafanya kazi chini kwa chini au ni kutotaka waonekane wapo kazini?
Au kuna mtu anahusika na huu ukimya wa ziara za ghafla ambazo hapo awali zilikuwepo kwa viongozi mbali mbali wa serikali?
Mbona yale matamko ya mawaziri kusimamisha simamisha watendaji wa chini yamepungua?
Maswali ni mengi ila ni wasaa wa kujadili ni nini kipo nyuma ya pazia hili ambalo zamani lilionesha kuwa na weupe uliotuwezesha sisi walala hoi kuona uchafu uliokuwa umejificha.
Kunani "ile kasi na utendaji baada ya viapo imeenda wapi?