Ule utafiti unawahusu na wanasiasa pia?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,559
Ule utafiti kwamba kwenye kila watanzania watano mmojawapo ni kichaa unawahusu pia na wanasiasa? Wabunge wapo zaidi ya mia tatu, ukigawanya kwa tano unapata makundi zaidi ya sitini ya watu watano watano. Kama utatifiti ule unawahusu watanzania na kwa kuwa na wabunge nao ni watanzania, basi bila shaka bungeni tunao wabunge vichaa zaidi ya sitini, ni kina nani hao?

Kwenye baraza la mawaziri je. kwenye Halmashauri za miji, Manispaa na majiji? Kwenye vyama vya siasa nako hali ikoje? Au ule utafiti unawahusu wauza mkaa na kina mama ntilie na wauza vitumbua peke yao wanasiasa hawahusiki? Nauliza tu?
 
Back
Top Bottom