Ulaya, Marekani na China wateja wakubwa wa mafuta ya Afrika

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
pipeline.jpg

CHINA imeungana na Marekani na Ulaya kama mteja mkubwa wa mafuta na gesi kutoka Afrika, FikraPevu inaripoti.

Takwimu zinaonyesha kwamba, kiwango cha mafuta ambacho China inanunua kutoka Afrika kimeendelea kukua huku kile cha Marekani kikipungua hasa katika kipindi cha kati ya mwaka 2007 na 2011.

Mchanganuo unaonyesha kwamba, katika mwaka 2011 asilimia 23 ya mafuta yaliyosafirishwa kutoka Afrika yaliuzwa Marekani tofauti na mwaka 2007 ambapo taifa hilo lilinua asilimia 30 ya mafuta hayo, wakati China ilinunua asilimia 14 likiwa ni ongezeko la asilimia 4 kulinganisha ni kiwango cha mwaka 2007.
ZAIDI...
 
Back
Top Bottom