Ukwepaji Kodi Kwa Kubadili Majina Ya Makampuni

mwana2009

New Member
Aug 10, 2008
4
1
Habari zenu mabibi na mabwana.
leo katika uchunguza wa kina kirefu kama ilivyoada nimefanikiwa kugundua makampuni makubwa yanayokwepa kulipa kodi ya serikali kwa kubadili majina ya makampuni yao kwa kile walichokisema eti kampuni imeuzwa.

Si kweli kwamba makampuni hayo huwa yanauzwa na kama yanauzwa basi itakuwa kila mtu anaanzisha kamapuni yake na akiisha nufaika na kupata mapato ya kutosha basi huuza kampuni kwa kukimbia kulipa kodi ya serikali na kuanzisha kampuni nyingine.

Je kwanini serikali isiwe inafanya kwamba wewe umenunua kampuni hiyo na unataka kuanza upya basi itabidi ulipe deni la hapo nyuma la mwenzio kabla hajakuuzia ili hela zisipotee na kama hutolipa basi usiruhusiwe kufanya biasha mpaka aliyekuuzia amalize deni lake .

Mfano mzuri ni kwa watu wa umeme pamoja na kampuni ya maji tanzania dawasco, yaani kama umehamia kwenye nyumba na ilikuwa inadaiwa maji na umeme basi utatakiwa kulipa kodi ya mwenzio then ndi ulipe ya kwako ili uweze kupata maji laasivyo wanakukatia maji / umeme mpaka hela zilipwe na hawajali nani alikuwa anakaa hapo mwanzo sababu wao haiwahusu.

Mfano mwingine mzuri ni kwenye mamampni ya simu kama vile hapo awali tulikuwa na kampuni inaitwa MOBITEL na yenyewe ikauzwa (feki) ikawa BUZZ nayenyewe ikauzwa (feki) ikawa TIGO sasa sijui ikitoka tigo sijui wataita NG`OMBE au nini maana hata hatuelewi.

Kampuni nyingine ilikuwa inaitwa CELTEL ikabadilishwa juzi tu kwa kukwepa kodi kama kawaida ya makampuni na sasa inaitwa ZAIN jamani sasa sisi wananchi tutapelekwa kama viroba mpaka lini kwani hili serikali hailioni au kuna mikono ya wakubwa humu na wenyewe wanaponea humu humu ?

Then kuna ile ilikuwa inaitwa SHERATON HOTEL daH hii ndio siipatii picture kabisa sababu zile ndio huwa zinaingiza hela kutokana na wageni wengi wanalala mule haswa wazungu ambao wanaiingizia serikali mapato yaani wanakuja kama watalii hivi, sasa kikubwa zaidi ilikuwa SHERATON ikabadilishwa tena kisanii ikajakuwa ROYAL PARM na sasa ni MOV N PEAK dah jamani serikali hii ni ya wapi jamani mbona swala dogo hili hata mtoto wa darasa la saba anaweza kuligundua ? inamaana hamuoni huu ufisadi wa makampuni ?

Na haswa usanii huu unafanywa na watu kutoka nnje kama vile wahindi na waharabu inamaana hadi leo bado tunatawaliwa ? inamaana hatuna maamuzi yetu binafsi na serikali yetu? inamaana RAIS na Mawaziri wake wote wameshindwa kuona hilo jambo ? tunaomba ushilikiano wenu kama serikali au mpaka siku tuchinjane wenyewe kwa wenyewe ndio tupeane haki zetu kama ilivyokuwa huko ruanda na burundi ?

Yaani hii nchi sijui inaelekea wapi hata ukienda kwenye migodi mambo ni yale yale tu wachimbaji wadogo wadogo wananyanyaswa na makampuni mageni kutoka nnje na kulipwa ujira mdogo nao kila wakisha maliza mashimo yale kuyachimba na kumaliza kilichopo wanavunja mkataba na ku sign mkataba mwingine kwa kubadili jina la kampuni na kuanzisha mgodi mwingine .Sasa wananchi tunafaidika nini na madini yetu ? maana hakuna tofauti kati ya enzi za baba wa taifa mwil JULIUS KAMBARAGE NYERERE yeye hakuruhusu madini ya chimbwe alikuwa na maana yake sio mjinga yule alikuwa anataka nchi iendelee kwanza ili tuweze pata wasomi na vyombo maalumu kwaajili ya kuchimbia hayo madini lakini walipoiingia viongozi feki madarakani wametuletea maafa makubwa na siju yataisha lini .

Sasa ndugu wanachi tujadiliane na tuweze kuona hili swala linafikia wapi na wanaofanya ufisadi huu waondolewe makalakani na tuweze kupata viongozi bola watakao wezeshsa nchii hii kufika mahala pazuri na kuwa na msimamo na nchi yetu sio kuongozwa na watu toka taifa lingine especial wahindi.

NAOMBA COMMENTS ZETU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom