sinajinasasa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 2,988
- 4,145
Habari wana JF!
Naomba wenye akili na ufahamu waje hapa tuijadili hii pasaka ya uongo.
Pasaka ipo kwenye biblia, na ilianza kuadhimishwa na wana wa Israel enzi hizo. Katika biblia pasaka huadhimishwa tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka, ili uhakikishe soma kitabu cha Kutoka 12:2,6. 13:10. Huu mwezi wa kwanza ni mwezi wa Abibu, ni mwezi kwenye kalenda ya kiebrania. Pasaka hufanyika siku ya sita ya juma, tarehe 14 ya mwezi wa Abibu kila mwaka! It is a Must! Rejea fungu lile la Kutoka 13:10. Kwa maelezo mengine ni kuwa Pasaka hufanyika siku ya sita ya JUMA (ambayo inaitwa siku ya maandalio ), tena tarehe inayofanana ya 14/01… kila mwaka.
SWALI KUU KWA WENYE AKILI?
Kwa nini Pasaka hii tunayoiadhimisha kila mwaka hufanyika siku ya sita (ijumaa kuu) lakini tarehe tofauti ya mwezi? Agizo la biblia ni tarehe 14 mwezi wa kwanza ambayo hiyo tarehe huwa inakuwa ni siku ya sita ( Maandalio ) Kwa nini leo tarehe huwa tofauti bali siku ni ile ile?
Jibu ni kuwa pasaka hii inaadhimishwa kinyume na tarehe aliyoiagiza Mungu kwa waisraeli zama hizo.
Kwa vile hawa wanaotengeneza kalenda hii tunayoitumia kalenda yao ni tofauti na ile waliyoitumia waisraeli. Ukitumia calendar ile ya Waebrania , lazima pasaka itadondokea tarehe na siku ile ile.
Na kama waebrania tarehe ile ya pasaka ilikuwa ni maandalio ambayo ni siku ya sita, basi siku iliyofuata ni siku ya saba, ambayo ni sabato. Basi kwa lugha nyingine kalenda hii ya leo imeficha kitu MUHIMU.
Watu wengi leo hawana ufahamu wa kalenda, wanadhani hii tunayoitumia ndiyo waliyoitumia Waebrania. Yesu alimwambia mwanamke (asiyekuwa Myahudi)”Ninyi mnaabudu msichokijua;….kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi” Yohana 4:22. Kwa kuwa wayahudi wamebeba siri za wokovu, wapagani walioishika na kuitawala dunia wamefanya juhudi za kuwaangamiza wayahudi, ili kuhakikisha hakuna Ukweli kujulikana.
Kwa ushahidi rejea historia za wayahud,i Holocaust, Kuanzishwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, yaani Israel imetengenezwa kama Scapegoat, yaani mbuzi wa kafara (rejea historia ya mbuzi wa kafara kwenye biblia), yaani kosa anafanya mtu mwingine ila lawama zote inabebeshwa Israel kama ndo anasababisha. Wayahudi wameenea kila kona ya dunia wakibadilisha ID zao ili wasijulikane maana ni risk kwao. Hivyo kweli inafichwa.
KWA NINI KALENDA ILIBADILISHWA?
Danieli 7:25 inasema “……..naye ataazimu kubadili majira na sheria……” kwa kiingereza …and think to change times and laws….
Majira/times ni nini?
Kalenda imebadilishwa kutoka ile ya Kiebrania inayotumia JUA na Mwezi (Soma Mwanzo 1:14) kwenda kalenda hii ya JUA yaani Solar calendar, na kubadili saa za kawaida 12 za siku (soma Yohana 11:9) kwenda 24 za siku.
Kubadilisha kalenda maana yake ni kupoteza siku, majuma, miezi na miaka ya kweli.
Ibada ya kweli imejengwa kwenye misingi ya kalenda. Mfano biblia inasema siku ya saba ni Sabato, watu siku hiyo inatakiwa waache kazi wapumzike wamwabudu Muumbaji wao. Hivyo unapobadilisha Kalenda unapoteza usahihi wa siku hizo, hivyo hata sikukuu za kweli kama Pasaka huwezi kuipata kama unatumia kalenda ya Jua pekee, ndo maana tarehe za pasaka zinatofautiana mwaka kwa mwaka kwa sababu ya ubovu wa kalenda ya kipagani ya JUA.
SABATO ya kweli ya siku ya saba nayo imepotea, soma Maombolezo 2:6….Amezisahauzisha katika Sayuni, sikuu kuu za makini na Sabato,……. .Kwa vile watu walibadili kalenda aliyowaagiza watu wake waitumie kwa ajili ya ibada zao za Sabato ya siku ya saba na Sikukuu makini kama Pasaka nk, hivyo bwana amezisahauzisha , watu hawajui . Hata muda wa kuanza sabato umepotezwa, leo waumini waaminifu wanaodhani wanatunza sabato ya kweli hudhani sabato huanza jua linapozama siku ya ijumaa na kuisha jumamosi jua linapozama. Ni kwamba, aliyebadili kalenda na times amefanikiwa kubadilisha hata waumini hawafahamu usahihi siku inaanza muda gani, je inaanza jioni au saa sita usiku au asubuhi watu wamevurugwa. Evidence za kwenye biblia na kalenda ya kiyahudi siku inaanza jua linapochomoza na kuisha jua linapozama. Hivyo kwa waebrania hawakuwa na sabato ya masaa 24, ni masaa 12 ya jua tu.
HITIMISHO
Hawa jamaa wenye kalenda, ambapo hata wewe msomaji hujui mwakani pasaka itakuwa tarehe ngapi hadi uone kalenda ya ukutani, wamefanikiwa kuudanganya ulimwengu kwa kuuficha ukweli wa Sabato ya siku ya saba kwa kuifanya kuwa Jumamosi.
Katika biblia hakuna sehemu ambayo inasema jumamosi ni siku ya saba hivyo ni sabato. Bali kuna siku ya kwanza, pili….na saba ni Sabato. Wamefanya ubunifu kwenye kalenda yao feki na hivyo ku insert Sabato yao feki yaani Jumamosi, kiasi kwamba kwa msomaji wa juu juu, atakuambia kama Ijumaa kuu ni maandalio basi automatically jumamosi itakuwa siku ya saba hivyo ni sabato na jumapili Yesu alifufuka ambayo ni siku ya kwanza ya juma. Ukiwa huna ufahamu wa kalenda lazima upotee. Ndo maana kote katika biblia wayahudi walikuwa wana sherehe za miandamo ya mwezi kila mwezi, hii iliwezesha kutopoteza sequence ya ibada zao/zetu.
Katika haya mambo, wapo wahubiri makini ambao sijui kama wana uhakika wanamfanyia kazi ibilisi, kwa kuwashutumu wayahudi na kuwalaani kwa sheria zao na amri zao kumi kama ni wamelaaniwa. Hata Sabato ambayo ni ishara ya watu wa Mungu na wengineo.
Hivyo watu watambue kuwa SABATO NI SIKU YA SABA na siyo JUMAMOSI kwa vile Jumamosi ni siku ya kwanza kwa kalenda waliyoitumia waarabu, na Saturday ni siku ya saba kwa kalenda ya jua hii ambayo ni Gregolian. Na kwa vile ukweli unatoka kwa Waebrania, vivyo hivyo hata sabato ya kweli lazima ipatikane kutoka kwa kalenda ya kiebrania, ambayo bahati mbaya kalenda hiyo ilipigwa marufuku katika Roman Empire kwa vile ilikuwa inapingana na State official calendar, kwamba hawa wanaenda kazini hawa ni ibada nk.
Japokuwa watu wengi hawapo tayari kuupokea ukweli, ukweli utazidi kushinda na walioko gizani hawataki kuja kwenye mwanga. Kama kuna mtu ana hoja ya utetezi au atatofautiana na mimi. Karibu sana.