Ukweli wa gas Mtwara

Ukweli wa gas Mtwara

haters

New Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
4
Reaction score
9
KWA NINI WANANCHI WA KUSINI WANAPINGA GESI ISITOKE
Kupinga gesi isitoke mtwara kwanza ieleweke,wanaopinga si wananchi wa mtwara pekee yao bali ni wananchi wote wa mikoa ya kusini kwa sababu zifuatazo
1. Mkataba mzima wa mradi huu, mpaka sasa si viongozi wa kusini tu inavyoonekana hata mawaziri husika hawajui na kama wanajua basi wasibitishe hilo , ndiyo maana hata cha kuwaeleza wananchi mpaka sasa hawana.
Mkataba wenyewe kuanzia majadiliano mpaka mradi kukamilika unaonakana umefanywa ndani ya miezi 20 tu na unafanywa na viongozi ambao wamebakisha miaka 2 kumaliza muda wao, wanataka kila kitu kikamilike kabla wao hawajatoka madarakani hii inaonyesha wazi kunakitu ambacho wanalazimisha cha maslai yao binafsi na si Taifa.

2. Wananchi wa kusini walipata mateso makubwa, zaidi ya miaka 40 wameishi bila umeme,maji ya tabu, miaka 51 ya uhuru mpaka leo barabara haijakamilika ianakuwaje mradi huu mkubwa zaidi inabidi ukamilike ndani yamiezi 18 tu, Tanzania wote ni ndugu na ni wamoja, ilikuwa kusini ni mikoa ya adhabu kwa wafanyakazi wa serikali ambao walikuwa wanafanya makosa katika mikoa mingine ya Tanzania,mikoa 25 ya zamani ya Tanzania yote ilikuwa imeungwa kwenye gridi ya taifa na walikuwa wanapata umeme kwa masaa 24 kasoro mikoa ya kusini mpaka leo bado ilchosababisha viwanda vingi kufa na maisha kuwa magumu sana mpaka ikawa adhabu ya dunia ndiyo maana waliokuwa wanakosea makazini wanapelekwa huko kwa adhabu.
Gas ndiyo ikawa tumaini lao pekee, lakini leo gesi inahamishwa hata jiwe la msingi la kiwanda hata kimoja au mradi wowote bado ndiyo maana wanagoma.

3. Tanzania sisi bado hakuna ulazima wa kukopa zaidi ya tilioni 2 kupeleka gesi Dar, July 2004 gesi ilianza kuingia Dar 51.2 Mmscf/d toka Songosongo , August 2008 vilikamilika visima viwili vya gesi pale Songosongo na kuongezeka kwa gesi Dar mpaka kufikia 90 Mm scf/d lakini tangu 2004 mpaka leo gesi hiyo kwa viwandani na matumizi mengine inayotumika 10 Mmscf/d ya 90 Mmscf/d ya gas inayozalishwa na songosongo kwa hiyo ukiondoa la umeme Dar na Tanzania kwa ujumla bado hakuna ulazima wa kukopa kiasi hiki cha pesa ambacho serikali kupitia TPDC katika mikutano yao ya kuchangia sera ya gesi imekili pindi mradi huu utakapoanza gharama za umeme zitaongezeka maradufu ina maana kupandishwa bili za umeme kwa viwanda vingine vyote vinavyotumia nishati ya umeme Tanzania na wananchi wengine ili tulilipe deni hilo.

4. Tanzania ilifanikiwa kupata wawekezaji wengi wakubwa kwa kuwa waliambiwa njooni muwekeze Tanzania, njooni mwekeze kusini kwa kuwa kuna bandari ya asili yenye kina kirefu , kiwanja kikubwa cha ndege, gesi nyingi, uranium, makaa ya mawe,chuma n.k, Wawekezaji waliokuwa wanakuja kuwekeza si kama walikuwa wanaangalia masoko ya Tanzania, na miradi iliyokuwa inawekezwa mingi ni mikubwa sana kama kiwanda cha mbolea cha wamarekani, Dangote n.k, Wao walikuwa na masoko yao tayari South Afrika, Angola n.k hata BG gesi yao tayari wana soko india ,wawekezaji walikuja kufuata huku malighafi na bandari na eneo yani mazingira mazima ya kusini.
Hawa wawekezaji hawakufuata Dar wala Bagamoyo na wangeweza kuekeza nchi yoyote ila walifuata kusini kwa ajili ya fursa zilizopo kule.
Nachokuambia kitendo cha kuondoa gesi mpaka sasa wawekezaji wengi wameondoa imani na Tanzania na miradi mingi ambayo tayari menejimenti zilikuwa zimeshaanza tayari wameshaondoka.
Hii gesi kutotoka Mtwara kwa sasa ni faida kwa Tanzania mzima siyo kusini mambo bado kabisa haijafika muda wa kukopa pesa nyingi na kwenda huko kwa hili la mkataba wa miezi 18 kukamilika kwani kabla ya miaka miwili ya kumaliza muda wao inatupasa tufikiri kuwa huu mkataba una lengo la kuwanufaisha wachache kabla ya kuondoka madarakani.

NOTE:
Baaydhi ya vyombo vya habari kama gazeti la uhuru linapotosha watanzania na kusema wanaogoma ni wachache , si Mtwara tu kusini yote wanagoma na kwa hilo halina itikadi ya vyama, huyu Ghasia waliomtaja wanamuunga mkono si kweli na kwa hili hata wanakijiji wa kijiji chake hawamtaki kabisa hata kumuona. Vyombo vya habari njooni kusini mutasibitisha hilo.
28/12/2012 waziri mwenye dhamana alikuwa anojiwa na Channel 5 anawadanganya watanzania gharama za umeme zitapungua wakati TPDC katika mikutano yao yote wanasema zitaongezeka maradufu, kuna vyombo vya habari kama clous wanaropoka , hawajafika,hawajaona mikataba na hakika wao walienda siku ya uzinduzi tu pale kinyerezi, hawajui lolote kuhusu hii gesi, jaribuni kufanya uchunguzi mnaondoa imani kwa wasikilizaji.

Kwa hili vyovyote mtakavyofanya mwisho wa siku ukweli utajulikana tu.
Watanzania wote tuungane tuwe wamoja tusikubali keki ya Taifa wale wajanja wachache.
Kwa kuthibitisha keki ya taifa inataka kuliwa na wajanja wachache katika gazeti la daily news la 05 july 2012 waliripoti kuwa wawekezaji wawili wanakwenda kwenda kuwekeza kiwanda cha mbolea ya Urea wakimnukuu kutoka Dodoma muheshimiwa Adam Malima,na kiwanda hiki kingekuwa kikubwa kusini mwa bara la Afrika na wangeuza mbolea katika nchi za Malawi,Zambia,msumbiji,Rwanda,Burundi,kenta,Uganda<Drc,visiwa vya comorona sudani lakini ikatokea taarifa katika mtandao wa jamii wa forum kuwa Rostam Azizi akishirikiana na Mawaziri anatuhumiwa kukwamisha kiwanda chambolea kisijengwekwa sababuwao wanapata mabilioni kwa kuagiza mbolea toka nje ya nchi na kuiuzia serikali,huu nimfano tu wa watu wachache wanavyoiyumbisha nchi kwa maslai yao binafsi,
Pia kulikuwa na kampuni binafsi ya umoja light kusambaza umeme katika mikoa ya mtwara,lindi na Ruvuma lakini serekali ilipinga kwakuwa kampuni ya rostam azizi ndiyo wanatenda ya kusambaza mafuta katika magenereta ya kuzalishia umeme katika sehemu zinazotumia mitambo ya mafuta katika mikoa hiyo
 
Tafuta katuni ya kipanya ya leo jumapili gazeti la mwananchi,ina majibu yako yote.
 
mtwara kuchele..........mama ghasia, kule naumbu kiukweli hawamtaki, na mengine uliyosema ni kweli...for now, nipo mtwara...hadi tarehe 02/01/2013...naandaa article ya suala hilo...and kwa haraka haraka, uliyoyasema ni kweli.....big up new guy.............
 
Kiukweli Kama ni kuitafuna nchi basi viongozi wa CCM wameitafuna vya kutosha tena bila aibu na hao waliokuwa wakiwaona wajinga, hawajitambui, wamelala leo wameshtuka na kudai haki zao hongereni sanaa watu wa kusini ........kip it up
 
Muachage basi kuvaa hayo manguo ya kijani na kuwapokea kwa ngoma, wamezoea kuwafanyia hivyo tangu zamani.Chadema walishawashtuaga tangu zamani na walishawaonyesha namna kujikomboa.Hata Korosho zimewanufaisha watu wengine ambao hata hawajui mti wake unafananaje!Msikubali Gas iwalaani.

Adui mkubwa no 1 wa maendeleo ni CCM
 
Kosa ni pale "MJINGA ANAPO JITAMBUA". Hapo ndipo shughuli pevu inapo anza. Hii ngoma ndiyo kwanza mbichi. Si tunajuwa jinsi Mmmakonde akizinda anavyo chachamaa!!!! UCHITEME WALA UCHIMUMUNYE". CCM lazima wataicheza SINDIMBA kama sio KIKOCHA!!!!!
 
Acha kina prof Muhongo wachukulie isue kirahisi rahisi kwa kudanganywa na magazeti ya uhuru na mzalendo
 
Ningeshangaa kama nisingekuona kweye uzi huu.
ninachojiuliza hadi sasa kama Temeke wamegundua gas nyingi hili bomba linalojengwa kutoka mtwara hadi dar la nini?
nadhani kuna watu wameshakula 10% hapo, hapa lazime kieleweke.

Mwanzo nlikuwa naunga mkono ujenzi wa hili bomba but gas ya Temeke inatosha kwa watu wa dar na viwanda vyake.
serikali sasa iweke wazi, kwanza katika nchi zenye mafuta lazima wananchi wanashirikiswa kuhusu utafiti na uchimbaji
na pia wananchi wanaelezwa hatua ambazo mwombaji wa leseni anapaswa kuzingatia kama Impact assesement, uwezo kifedha wa mwomba leseni, ajira za wazawa katika mradi wake nk.

Pili lazima kuwe na sheria inayoweka wazi wiwango vya kodi atakavolipa mwomba leseni, hivi hatujui
kwa sasa kama ni processing industry ijengwe mtwara,watu watapata ajira huko hata za mama ntilie
na ukuli kwenye processing industry ya gas nk

MTWARA NA KUSINI MSIKUBALI KUIBIWA GESI YENU,HAMJASHIRIKISHWA,MAAMUZI MMEFANYIWA NA WATU WENGINE TOFAUTI KWA MASLAHI YAO NA ADVANCE ZAO NDIO HIZO ZIMESHAWEKWA BANK ZA USWIZI.
aluta continue.

thank you,na umeeleweka mkuu

gesi kuhamishwa pande za kusini shughuli itakua pevu sana
 
Tena radio Clouds tulidhani ni redio ya wajanja kumbe imegeuka KICHEFUCHEFU,watangaze udaku wao tu, mambo ya Wanamtwara wasiingilie kwa kuongea utumbo maana NO RESEARCH NO RIGHT KUPAYUKA.Huyo Ghasia anajifahamu kuwa alishakataliwa siku ya mkutano wa Kinana na MAGAMBAS wenzao,so hana chake tena aendelee kuunga miradi ya Bagamoyo maana anajua shoga yake ndiye alitoa pande kwa msela akaletwa pale.Yote kwa yote vijana wameanza mafunzo ya kutengeneza vilipuzi ili tugeuke Nile Delta,CHOKOZA MAKONDE WEYEE!!!!
 
Acha kina prof Muhongo wachukulie isue kirahisi rahisi kwa kudanganywa na magazeti ya uhuru na mzalendo

MSIMAMO WA WANAMTWARA UNATAKIWA UUNGWE MKONO NA WATANZANIA WOTE WENYE UZALENDO.

1. Tunajua kuwa hilo bomba linalotakiwa kujengwa litamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja, je gesi itakayosafirishwa inamilikiwa na akina nani, kwa asilimia ngapi kila mmoja?

2. Swali hili linatokana na ukweli kuwa maliasili zote zinazovunwa humu Tanzania hazimilikiwi na Serikali wala Watanzania. Dhahabu huko Geita, Kahama, North Mara n.k. tunazisikia tu zikibebwa na helikopta bila kuambiwa zinakokwenda!

3. Watafutaji wa hii gesi wamekwisha lipa zaidi ya TShs. 300 bilioni kwenye akaunti binafsi za viongozi waliowasaidia kuwapa vitalu vya KUTAFUTA hiyo gesi hata kabla gesi yenyewe haijapatikana, je baada ya kupatikana, gesi hiyo ni yetu WATANZANIA au ni kama dhahabu za Geita, Kahama na North Mara ambako Watanzania wanaambulia kupigwa risasi na Polisi wa Tanzania huku mali asili za nchi zikivunwa na WAGENI usiku na mchana?

4. Watu wa Mtwara wasionekane kuwa wanataka kujibagua kwa kudai kufaidika na maliasili za nchi hii. Kinachotakiwa ni sisi WATANZANIA WENYE UZALENDO kuwaunga mkono na kuuliza hizo maliasili zetu kama dhahabu zinazochimbwa kila kukicha zinatunufaisha kwa kiwango gani.

5. Miaka ya nyuma kidogo, WILAYA YA MAHENGE ilisikika sana kwa kutoa madini aina ya RUBY; Tujiulize, hizo RUBY baada ya kuwakaribisha WAVUNAJI (Serikali huwaita WAWEKEZAJI) kutoka Thailand, Mahenge na Tanzania kwa ujumla ilifaidika vipi? Kilichobaki kula ni mashimo ambayo wala hayakusazishwa, na WANANCHI WA MAHENGE, ambao ndio WALIOKUWA WANAJUA KINACHOFANYIKA walikaa kimya; JE HUO NDIO UZALENDO TUNAOTAKA NA WANAMTWARA WAUIGE? WAKAE KIMYA HUKU MALI ASILI ZA NCHI ZIKIVUNWA BILA WATANZANIA KUFAIDIKA NAZO?

5. Kinachozungumzwa hapa SIYO KUKATAA kupeleka gesi Dar es Salaam kuendesha mitambo ya KUZALISHA UMEME , Swali ni kuwa hao TANESCO watakuwa wanamlipa nani watakapokuwa wananunua hiyo gesi ya MTWARA?

6. Watawalipa WATANZANIA wenye gesi yao au watawalipa hao WAVUNAJI ambao wamekwisha MILIKISHWA GESI YA WATANZANIA baada ya KUINUNUA kwa kuwalipa WATAWALA/VIONGOZI zaidi ya Shilingi bilioni 300 katika akaunti zao binafsi huko Uswisi?

7. WATANZANIA TUUNGANE KWA NGUVU MOJA NA WANAMTWARA KUKOMBOA MALI ASILI ZETU
 
Gesi kuja Dar itakuja tu,tuache ushabiki
 
Gesi kuja Dar itakuja tu,tuache ushabiki

What will happen to this pipeline when more gas is discovered near Dar. We know that natural gas has already been discovered in Mkuranga and it is likely there will be even more gas discoveries in Temeke and other Coastal areas near DAR. Will the Government then send this Mkuranga/Temeke gas to Mtwara?

The Government should stop this Pipeline project and carefully analyze all the options. I believe the decision on the Mtwara pipeline is being rushed through with dire consequences to the Nation. Tafadhalini CCM tuwekeni UZALENDO mbele rather than MATUMBO yetu.
 
duh! kumbe watu wanaifanyia maandamano mali asili ambayo imeibiwa tayari....
 
ningeshangaa kama nisingekuona kweye uzi huu.
Ninachojiuliza hadi sasa kama temeke wamegundua gas nyingi hili bomba linalojengwa kutoka mtwara hadi dar la nini?
Nadhani kuna watu wameshakula 10% hapo, hapa lazime kieleweke.

Mwanzo nlikuwa naunga mkono ujenzi wa hili bomba but gas ya temeke inatosha kwa watu wa dar na viwanda vyake.
Serikali sasa iweke wazi, kwanza katika nchi zenye mafuta lazima wananchi wanashirikiswa kuhusu utafiti na uchimbaji
na pia wananchi wanaelezwa hatua ambazo mwombaji wa leseni anapaswa kuzingatia kama impact assesement, uwezo kifedha wa mwomba leseni, ajira za wazawa katika mradi wake nk.

Pili lazima kuwe na sheria inayoweka wazi wiwango vya kodi atakavolipa mwomba leseni, hivi hatujui
kwa sasa kama ni processing industry ijengwe mtwara,watu watapata ajira huko hata za mama ntilie
na ukuli kwenye processing industry ya gas nk

mtwara na kusini msikubali kuibiwa gesi yenu,hamjashirikishwa,maamuzi mmefanyiwa na watu wengine tofauti kwa maslahi yao na advance zao ndio hizo zimeshawekwa bank za uswizi.
Aluta continue.



thank you lokisa

imekaa poa sana analysis yako
 
Ajabu nyingine ni kuwa gesi hiyo itaweza kuuzwa hapa TZ kwa wateja mbalimbali kwa kutumia sarafu ya Merikani (dola), kama inavyofanyika kwa ile inayopatikana Songosongo!
 
Gesi kuja Dar itakuja tu,tuache ushabiki

Hakuna sababu inayokubalika kuhamisha rasilimali na kunyima watu haki yao ya kiucgumi hata kama ni kulipia madawa ya kulevya ya mtoto wa mkulu yalitokamatwa Hongkong najiunga na varangati hili kwa hali na mali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom