Ukweli usipowekwa wazi utekaji uko palepale

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,506
661
Kwa yaliyotokea leo ni dhahiri kuwa wasanii wahusika ndio wanachochea saaaana kuendelea kuwepo kwa matukio ya wasanii na wengine kutekwa, kupigwa na kupotezwa lakini cha ajabu utasikia maisha yangu yapo matatani.
Mtu umetekwa umepigwa hujafanya kosa badala ya kuja hadharani na kusema ukweli wa tukio hata kama umepewa hela au kutishwa kwa nini usiseme ukweli ili jamii ijue na ikomeshe hii tabia. Huyo mtekaji hatathubutu tena kufanya upuuzi wake akitajwa jina. Hata kukuumiza ukimtaja hataweza jamii itakuwa inajua nani kakuumiza.
Sasa Roma kusema swala lipo polisi haina maana. Ipo polisi sawa lakini nini kilitokea? Kuficha kwake ndio kutaka kesho mimi na wewe tutekwe sasa. Anachangia utekaji pia
 
Katishwa huyu Mkuu katishwa sana. Hayuko huru tena ndani ya nchi yake. Tuombe Mungu labda mawakili wake wataweza kumshawishi aseme yaliyojiri tena bila woga hata kama hawafahamu waliomteka.
 
Kaongea anachokijua sasa nyie povu la nn??
ombeeni bas na nyie mtekwe ili mje kusema icho mnachoamin kuwa wanakificha!
mbuzi nyie!!!!!
 
mkuu muonee huruma maana usemecho ni kweli ila katamalizwa faster ka roma cha watu

pale alipo anataman kweli kusema ukweli ila ndo ivyo hawezi
 
Kwa yaliyotokea leo ni dhahiri kuwa wasanii wahusika ndio wanachochea saaaana kuendelea kuwepo kwa matukio ya wasanii na wengine kutekwa, kupigwa na kupotezwa lakini cha ajabu utasikia maisha yangu yapo matatani.
Mtu umetekwa umepigwa hujafanya kosa badala ya kuja hadharani na kusema ukweli wa tukio hata kama umepewa hela au kutishwa kwa nini usiseme ukweli ili jamii ijue na ikomeshe hii tabia. Huyo mtekaji hatathubutu tena kufanya upuuzi wake akitajwa jina. Hata kukuumiza ukimtaja hataweza jamii itakuwa inajua nani kakuumiza.
Sasa Roma kusema swala lipo polisi haina maana. Ipo polisi sawa lakini nini kilitokea? Kuficha kwake ndio kutaka kesho mimi na wewe tutekwe sasa. Anachangia utekaji pia
Itakuwa vyema jitokeze hadharani ulizungumze ili ukamatwe ukiachiwa uje useme ukweli ili utuokoe na sisi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom