Ukweli unaouma usiodhuru

mmmuhumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2017
Posts
493
Reaction score
480
Mwanaume mmoja mwenye miaka sabini na nane(78), akiwa na miaka (24) akilibahatika kuwa na mchumba na baada ya mwaka akafunga naye ndoa. Baada ya miaka mitano alibahatika kuwa na mtoto mmoja wa kiume ambaye amekuwa ni furaha na kuwajenga kuwa na upendo yeye na mkewe.

Ikiwa sasa ni miaka hamsini na nne (54) tokea wafunge ndoa, hawakubahatika kupata mtoto mwingine zaidi ya huyu mmoja. Kwa mapenzi na hali ya maisha, huyu mwanaume alikuwa ni mjasiriamali, akiwa na miaka arobaini aliukata na kuwa na maisha bora. Aliweza kuwa na kampuni ya usafirishaji na miradi mingine midogo ambayo yeye na mkewe walisaidiana kuijenga.

Akiwa na miaka sitini na mbili (62), alipata ajali iliyompa dosari mwilini na hivyo akawa hawezi kutembea zaidi ya kusukumwa katika kiti. Miradi yote alimwachia mtoto wake na kwa malezi aliyompa, hakika aliisimamia vyema. Baba na mama walijivunia kuwa na mtoto huyu.

Baada ya mwaka mmoja wa ajali, mke wake alianza kuumwa na katika kufatilia matibabu aliambiwa ni kansa na imeshamshambulia mno hivyo wakati wowote huenda akapoteza maisha. Siku moja akiwa nguvu zimemuishia, alipokuja mwanaye alimtuma kaniitie baba yako. Kijana alienda na kumleta baba yake akiwa kwenye kiti na mama akaomba awapishe.

Mke aliongea kwa kulia, "Mume wangu, nasikitika nakuacha ikiwa bado nakuhitaji na unanihitaji pia, lakini maumivu nayoyahisi mwilini mwangu, sina wa kumpa zaidi ya Mungu, naamini ipo siku utasimama tena na utawalea vyema watoto wetu ila upo ukweli mchungu nataka uujue.

Sihitaji kufa na kukuacha katika upofu na mimi kuingia kaburini na hii dhambi, mtoto tuliyenaye si wa kwako, ni mtoto wa marehemu kaka yako, wewe hukuwa na uwezo wa kunipa mimba".

Mume alishtuka na mke aliendelea kuzungumza, "Tulipoenda kupima siku ile mimi na wewe na ukapata simu ya dharura, majibu yalipokuja niliona hilo ila kwa mapenzi yangu sikupenda kukupoteza, nilivumilia matusi yako ya mimi kuniita mgumba.

Hatimaye nilifanya uamuzi wa kumuwekea kaka yako dawa ya usingizi na alipolala mimi nilimtumia na mpaka amekufa hakujua kama anamtoto huyu wala kujua kama aliwahi kuniingilia. Mume wangu najua upo kwenye kiti huwezi kusimama, lakini huyu mtoto wewe ndiyo baba yake umemlea na ndiyo miguu yako na muendesha miradi yote na anatulea bila kutuchoka. Kunisamehe ni wewe na kuificha au kuitoa siri hii ni wewe, nakupenda mume wangu".

Baba aliumia, lakini muda siyi mrefu mkewe alikata roho, baba alishtushwa na kimya cha mkewe, aliita kwa nguvu jina la mkewe, lakini kimya hakuitika, mwisho kwa uchungu alijikuta amesimama na kumkumbatia mke pale kitandani na kumuita lakini hakuitika.

Mwanae aliporudi alishangaa kuona baba amesimama na analia huku amemshika mama yake, alisogea na kujua mama ameshafariki, baba alimkumbatia mwanawe na kuzidi kulia pamoja na mwanawe.

Baada ya mazishi baba alimsamehe mkewe na alizidi kumpenda mtoto kama mwanawe wa kumzaa na kuificha siri ile.

#imarika na mmmuhumba
Kwa ushauri katika mahusiano, kupata maneno matamu ya mapenzi na mahaba (love sms) pamoja na elimu ya mahusiano.
Mawasiliano 0624 440 454
Tiktok@mmmuhumba

 
Wanawake wengi sana hua wanakufa na hii siri moyoni. Hawasemi!
 
Mtu akipewa dawa ya usingizi anao uwezo wa kusimamisha dyudyu na kufanya tendo kikamilifu? Madaktari nisaidieni
 
Mtu akipewa dawa ya usingizi anao uwezo wa kusimamisha dyudyu na kufanya tendo kikamilifu? Madaktari nisaidieni
Anaweza kusimamisha na ikatumika vyema tu na mtumiaji, dawa ya usingizi (tafsida hiyo). Bila yeye kutambua ni kinaendelea. Kilevi uamsha metaboliki mwilini.
Kikubwa manii ipatikane..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…