Fortilo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 5,013
- 15,633
Mambo yanayoendelea bungeni wala sio mageni, hasa kwa mustakabali wa upinzani wa nchi hii, zaid sana wala hayatishi.
Baadhi yetu, ni mambo tulioyatarajia, ila ushirikiano wa Upinzani na CCM hasa Chadema kwenye mambo ya kitaifa, hasa ya kuleta mshikamano na utengano wa kitaifa ni kama Chadema wanapona haraka sana majeraha yao.
Sitaki kuongelea kabisa mambo haya
1. Chadema na upinzani walivyoshiriki juzi kumpigia Kikwete makofi Bungeni wakasahau namna alivyowahenyesha Soweto, Iringa, Morogoro, Escrow, Ugaidi, n.k
2. Chadema na upinzani walivomuhurumia Nape na kumuita Shujaa wakati akizozana na mabosi wake... haraka sana wakasahau ishu ya Bunge live, Goli la mkono, na matusi yasiomithilika dhidi ya wagombea wao wa nafasi mbali mbali hasa ya urais.
3. Sitaki pia kuzungumzia ushirikiano wa dhati kabisa wa CDM na upinzani waliokuwa wanamuonesha Rais wakati akitembelea maeneo yao.. hadi alipoanza kuwalambisha dawa ndipo wakatia adabu, Boniface Jacob, Mbunge wa CUF lindi/Mtwara? Anakumbuka vizuri.
4. Kushirikiana nao hata linapokuja suala la kupigia kura wagombea wa CCM wenye chuki za dhati dhidi yao... hata juzi EALA upinzani ulipiga kura za kuliunganisha taifa.. lakini walipotoka.
5. Chadema na upinzani walivyoshiriki kusifia utendaji wa Rais , kabla hawajaambiwa 'kwenye serikali yangu sichagui mpinzani hata mmoja" wakabaki wanaduwaa......
Kwa uchache kuhusu kigingi cha mhimili wa Bunge, Spika Job Ndungai...
Chadema wamesahau kuwa Job Ndungai ni mwana CCM, tena ili uchaguliwe uwe Spika, uCCM wako unahitajika uwe beyond reasonable doubt... and yes.... here he is.....(Kumbuka ya Sitta bunge la kumi)
Chadema waliokuwa wanasema Ndungai ataliunganisha bunge, wakasahau kabisa uccm wa Ndungai.
Kwa Ndungai ishu za kupendelea CCM hazikuanza leo....
1.Ndungai ndie huyo huyo alieamuru Polisi kuingia bungeni kuwatoa kwa nguvu kina Tundu Lissu na Joseph Mbilinyi..... hawakumbuki.
2. Ni huyo huyo alieamuru mijadala mingi sana ifungwe kwa maslahi ya chama chake toka akiwa Naibu wa Spika kwenye bunge la Kumi.
3. List ni ndefu.....
Chadema hao hao, ndio walikuwa mstari wa mbele kumuombea dua apone haraka(Kitu ambacho si kibaya hata kidogo) arudi aendelee na kazi yake ya kuliunganisha bunge(Nashangaa sana, amuunganishe nani na nani)
Yapo mambo mengine hadi unakasirika , unaweza sema labda upinzani hamna, wote ni wale wale au labda kuna kitu.. kumbe ni kuwa na kumbukumbu fupi au kuwa na moyo wa kulipenda taifa zaidi ( kumbe wenzenu wanawaumiza kisiasa )
CHADEMA NA UPINZANI WANA LA KUJIFUNZA KWENYE CHAMA DOLA, NALO NI HILI.
Waache siasa za kusahau, CCM Hawasahau baya, ukishawatenda wao wanakutenda zaidi... wazungu wanasema " where it hurt the most" na kwa taarifa yao tu, CCM wana chuki za kudumu.
i/ Imagine mtu kama Lau Masha... CCM wanakumbuka kuwa aliwatosa mwaka 2015, hivyo watamkomoa tu asipate kitu.
ii/Mtu kama Sophia Simba.. wamekuja kumtosa miaka miwili baada ya uchaguzi tena kwa aibu.
iii/Mtu kama Makongoro Nyerere.. walimchoka tu, basi
iv/Mtu kama CHADEMA yenyewe.. wameamua waivimbie tu, liwalo na liwe....
Ila nyie sijui kwanini hamuelewi hii tune...?
Nimewawekea verse, mshindwe tena kuimba.
Wasalaam,