Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,197
- 7,533
Wakuu, moja ya tatizo ambalo limetuumiza, linatuumiza na litatuumiza sana kama hatutabadilika; ni kwamba hakuna anayetaka kuwa mkweli kwenye siasa zetu, na kama wapo wanaoamua kuwa wakweli, ni wachache sana na hawapati uungwaji mkono.
Mtu yoyote anayefuatilia kwa ukaribu atakubaliana kwamba, Tanzania tumekuwa na utaratibu mtu hatetei kitu kwa kuwa ni kizuri au kukemea kitu kwa kuwa ni kibaya bali kwa sababu kinamnufaisha je yeye au kundi lake. Kwa mfano;
Unakuta mtu anasema hadharani bila hata wasiwasi, hawa watu sio wakwetu mkiweza wafanyieni vurugu, na hakuna anaye kemea. Sasa subiri huyo anayesema hayo siku awe muhanga utaona atakavyoongea point hutaamini kama ni yeye.
Haya, unakuta mwingine naye anaongea point kweli leo ila ukiangalia unakuta ni muhanga. sasa ngoja atoke kwenye kundi la wahanga utaona atakavyowageuka wahanga wenzake.
Unaweza ukakuta mtu anatetea ujinga mpaka unashangaa huyu jamaa vipi, lakini sio kwamba hajui kwamba anatetea ujinga; bali ananufaika na anachotetea kwa wakati husika. Sasa subiri siku awe muhanga na aanze kuumizwa na kundi analotetea utaona atakavyoanza kujenga hoja madhubuti zilizojaa ukweli mtupu lakini sasa sio kwamba sasa anajenga hoja na kuongea ukweli kwa kuwa anaona ni wajibu kufanya hivyo, bali kwa kuwa ameshakuwa muhanga.
Kwa upande mwingine, unakuta mwingine anajenga hoja nzuri sana zenye ukweli mtupu ila wakati anajenga hoja hizo, anajitetea dhidi ya dhulma anayofanyiwa (ambapo unakuta kweli anadhulumiwa). Sasa siku na yeye akiwa upande wa mdhulumuji au akipata nafasi ya kudhulumu au kufanya 'the same error' aliyokuwa anaikemea kwa hoja nzuri na ukweli mtupu, atafanya kituko hakuna atakayeamini. Akiulizwa atajibu jibu rahisi tu! Siasa mchezo mchafu. Hivi kwa utaratibu huo, ni kwa vipi tunaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote la maana?
Hali hii husababisha zoezi zima la kuondoa au kuzuia uovu usitokee kuwa gumu sana karibu kila mahali. Husababisha hata wanaodai kuwa wanakabiliana na uovu nao wasiaminike. Husababisha pia watu ambao ni waungwana na wana nia njema kweli ama waogope au washindwe kushiriki kwenye siasa lakini chaajabu hata wanapojaribu huwa hawapati uungwaji mkono nao ni wepesi kukata tamaa isivyo kawaida.
Ikumbukwe, kwa kadiri watu wema, wenye uelewa au maono positive wanavyoshindwa kushiriki kwenye siasa kwa sababu yoyote ile, ndivyo uwezekano wa kuwa na siasa zenye utata unavyoonezeka na hali hiyo katika hatua yake ya juu kabisa hatutaacha kutafutana.
Nini tufanye: Ni muhimu kila mtu bila kujali chama chake akajitahidi kuwa mkweli. Kwenye tatizo aseme ukweli na kwenye jambo zuri aseme ukweli bila kujali nani anafanya au nani anafanyiwa nani mnufaika au nani anaumia. Lakini wananchi nao wajenge tabia ya kukemea uovu wowote wanaouona bila kujali mfanyaji ni nani na mwathirika ni nani.
Tukiendelea na utaratibu wa kutokuwa wa kweli, na kila kitu tunaangalia kwa jicho la wao na sisi, mimi na wao nk. Mwisho wake hautakuwa mzuri bila kujali chama kipi ni kipi na madhara yake hayatachagua