Ukweli 'Muhimu' kuhusu suala la umaarufu!

Ukweli 'Muhimu' kuhusu suala la umaarufu!

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,146
Reaction score
3,460
UKWELI 'MUHIMU' KUHUSU SUALA LA UMAARUFU!

Umaarufu ni mchanganyiko wa mambo au vitu kama vitano hivi.

1. Kipaji halisi (talent)
2. Muonekano wako na ujitunzaji wako binafsi
3. Kujiamini (confidence energy)
4. Kuwa na mtandao (connections)
5. Uwepo wako mitandaoni (visibility)

Ukiwa na sifa au vitu hivyo vitano, basi unaweza kufanya MANIPULATION OF ENERGY kwa ajili ya umaarufu na baada ya muda ukajikuta umekuwa maarufu sana sio tu Tanzania, bali East Africa kwa ujumla and beyond.

Kama huna hayo mambo 5 niliyoorodhesha hapo juu, my friend, achana na dawa!

Hakuna dawa itakayochukua nafasi ya vitu hivi.

Umaarufu unabebwa na kipaji (talent) ulicho nacho!

Je, una kipaji gani?

Watu wa nyota za Samaki, Simba, Punda, Ng'ombe, Mizani (kwa uchache); wengi wao wana vipaji vya asili vya sanaa (sanaa inamfanya mtu kuwa maarufu kwa urahisi)

Kwa Upande wa Kiroho, labda niongelee suala la Energy na Chakras.

Kwa msanii kama mwanamitindo, kwa mfano, chakra 3 ni muhimu sana kuhakikisha ziko active and balanced.
(a) Sacral Chakra
Nimefundisha wanafunzi wangu wanaosoma mada ya mwezi Februari (Chakra Awakening) kwamba Sacral Chakra inahusiana na ubunifu, mvuto wa kimwili na sexual energy.

Ikiwa active, mtu anakuwa na mvuto wa asili.
Ikiwa blocked, mtu anakuwa na aibu kupita kiasi, hofu ya kuonekana.

Unaweza kuiamsha na kuifanya iwe active kwa:
  • Kuwa na mazoea ya kucheza (dancing)
  • Kusikiliza muziki
  • Kuvaa mavazi ya rangi ya machungwa (🍊) mara kwa mara.
  • Kunywa maji mengi
  • Kujikubali
  • Kufanya Yoga, mantra husika na mudra ya kuiamsha (mlisoma mada hii ongezeeni tafadhali, mengine nimewaachia nyie makusudi)

(b) Chakra nyingine ambayo inatakiwa kuwa active ni Solar Plexus Chakra.

Hii chakra ikiwa active:
- Inakupa nguvu ya kujiamini (power ya ndani)
Kumbuka msanii bila hii power/ energy, hawezi kuhudumu.
- Ikiwa active hii chakra msanii anakuwa na 'stage presence' kali sana (kuteka/ kumiliki jukwaa)

Hii chakra ikiwa blocked, msanii anaogopa auditions (wengi ndio hujikuta kwenye uraibu wa kutumia drugs, pombe kali, shisha nk. ili kuamsha mzuka😃)

Hii chakra unaweza kuiponya kwa:
1. Kufanya mazoezi ya tumbo (yapi? Wale mliosoma mada hii yataje)

2. Kujisemea maneno mazuri ya uthibitisho (positive affirmations)
TOENI MIFANO.

3. Kujifunza kuzungumza mbele ya watu
MLIOSOMA HII MADA TIA NYONGEZA HAPO👆👆👆

(c) Chakra nyingine ambayo kwa msanii inatakiwa kuwa very active ni Throat Chakra.

Hii chakra ni muhimu sana iwe balanced kwa msanii (hasa kama anaimba au kuongea)
Achana na kina Isaiah Febu wanaochora katuni kama ki- 🐁
😃😃😃

Throat Chakra inatawala sauti na mawasiliano.

Aidha, ukishajiridhisha kwamba hizo chakra ziko very active, ndipo unaweza kutumia nyenzo kama mafusho, mafuta, vito (Crystals)vya Mvuto na Umaarufu kama:
✓ Citrine (jiwe la mafanikio na kujiamini)
✓ Carnelian (jiwe la mvuto na ubunifu)
✓ Tiger’s Eye (jiwe la ujasiri na mvuto mkubwa)

Ukishakuwa mtumiaji wa mawe hayo na mengine niliyoorodhesha hapo juu, sasa unatakiwa kuanza kufanya au kuwekeza kwenye:

👉🏼 Kujenga 'Personal Brand' yaani
kuamua wewe unataka kuwa nani? Kuwa msanii wa aina gani (Classy model)

👉🏼 Kuwa na 'street vibe' yako, vitu kama fashion hivi ili uweze kuwa na identity (utambulisho) ya peke yako. Usifananie wengine. Ujitofautishe.

👉🏼 Zingatia sana matumizi ya mitandao especially Instagram & TikTok , weka picha zako au video zako zenye ubora wa hali ya juu, sio zile umepiga na Infinix yako 😃😃 na ujitahidi kuwa consistent mitandano (angalau posts 3–5 kwa wiki), huku ukiweka na zile reels za ubunifu, hashtags nk.

👉🏼 Kama kutatokea mashindano fulani yanayohusiana na aina ya sanaa unayofanya, jitahidi sana kushiriki kikamilifu ili kuongeza 'exposure' yako kwenye jamii.

👉🏼Tafuta Mentor wako (mtafute msanii au model - mtu anayefanya sanaa kama yako, lakini aliyefanikiwa, ili akuelekeze kwenye baadhi ya vitu)

👉🏼 Kuwa na nidhamu ya kazi, kula na kulala vizuri, fanya mazoezi, zingatia 'skincare' (tunza ngozi yako na mwonekano wako kwa ujumla), soma sana kuhusiana na 'industry' ya sanaa na yanayofanana na hayo.

Note: Hata hivyo, umaarufu sio tu kuwa na mvuto, bali pia kuwa na uwezo wa kuvumilia kukataliwa, nguvu ya akili (usiwe kilaza ukategemea mafusho na uchawi mwingine mwingine, utaishia kuoga na mjini huendi😂😂😂)

Assignment:

Andika ndoto yako inayohusu aina ya sanaa yako (uanamitindo, uigizaji, muziki, dancing, kuchora etc) kisha iwekee timeline ya kama miaka 2 au 3 hivi huku ukifanyia kazi yote niliyoelekeza hapo juu na matokeo kwako yatakuwa ni uhakika.

NI KITU GANI KAMA MSANII UMEKIELEWA.

Dondosha comment yako hapo chini.

Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ (PhD),
Mtafiti na Mkufunzi wa masuala ya kiroho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom