Ukweli mtupu

Ukweli mtupu

MADIBA MANDELA

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
503
Reaction score
398
WALIOPATA ZIRO WANA VITU VINGINE HATUKUVIPIMA.

Na Thadei Ole Mushi.

Picha ya kwanza hapo ni ya Charles Msonde katibu wa baraza la mitihani Tanzania.

Huyu Jana katoka kutupa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na katuambia kuwa ufaulu umeongezeka.

Kwangu Mimi ufaulu ulioongezeka ninautafsiri kama idadi ya wanafunzi wenye uwezo wa kukariri umeongezeka na unaongezeka mwaka hadi mwaka.

Maana yake ni kuwa Msonde amemaliza kazi Moja tu ya kupima nani mwenye uwezo wa kukariri masomo kuanzia Saba na kuendelea.

Kuna usemi maarufu sana unaifananisha Elimu yetu na mtihani waliopewa wanyama wa kukwea mti. Hapa lazma nyani atafaulu huku tembo na Samaki lazma wapate sifuri.

TWENDE SAWA HAPA.

Nyerere alipoanzisha falsafa ya "Education for Self reliance" alikuwa amelenga kila mhitimu katika ngazi yotote ya Elimu Tanzania aweze kutumia maarifa aliyoyapata kujitegemea.

Ndio maana katika Shule zetu tulifundisha michepuo mbalimbali ya Kilimo, Ususi, uchoraji, ufugaji nk. Hii ililenga kuwa mhitimu anapomaliza std seven au form four aweze kujitegemea.

Mwl Nyerere hakuishia hapo akajenga vyuo vya kati ambavyo vilifundisha kwa vitendo, vilikuwa havina haja ya kusibiri mtu aliyemaliza form six ndio aje chuo hapana hata wa Darasa la Saba alijiunga na taifa lilipata mafundi wazuri na watu wabobezi katika fani mbalimbali walioweza kujitegemea.

Vyuo hivi tukavibadilisha tukavifanya vyuo vikuu na vingine tukaviua kabisa. Sasa vyuo hivi vinapokea waliomaliza PCM form six na tunajidai tunazalisha Mainjinia kama Injinia Bwire....

Nakurudisha kwenye hoja:-

Matokeo ya Jana ni mwendelezo tu wa kupima uwezo wa kukariri, kuna watu waliokuja na talent zao mbalimbali mashuleni ambazo tumeziua na hazikuendelezwa huo ndio mfumo wetu wa Elimu ulivyo.

Yaani tunapozaliwa kila mtu anakuja na Talent yake kwa mfumo wa Elimu wa Tanzania unapoandikishwa la kwanza kazi ya mwalimu ni kufuta talent na ubunifu anaokuja nao mwanafunzi na kuanza kumkaririsha Kina kinjekitile Ngwale. Wakimaliza wote tunataka tufanane kabisa haitawezekana.

Tujiulize hawa wanaofeli kila mwaka kwa kushindwa kukariri je tumewaandaaje kutumia maarifa na Talents zao nyingine?

Picha ya Pili hapo ni ya Mjasiriamali wetu kijana kabisa wa hapa Nchini anaitwa Ruge Mutahaba.

Nataka kusema nn kuhusu Ruge?

Huyu ni mtu anayeguswa sana na uhaba wa ajira kwa vijana nchini, ndio maana katika matamasha yake ya Fiesta ana Package ya kufundisha vijana Fursa katika maeneo yao.

Ninachojiuliza ni kwa nn tumsubiri hadi mtu amalize chuo kikuu ndio tuje tunfundishe kuhusiana na Fursa na kwa nn Jukumu hili tumwachie Ruge? Ina maana Elimu yetu haiwezi kuzalisha watu ambao wanaona Fursa zinazotuzunguka?

Ni kwa nn hatufundishi utalii kuanzia huku chini primary, ni kwa nn hatufundishi kilimo, kwa nn hatufundishi ujasiriamali ni kwa nn hatufundishi namna bora ya ufugaji ?

Ukiniuliza kwa nn Kinjekitile tunamsoma kuanzia Msingi hadi Chuo kikuu sintoweza kukujibu. Kila ngazi tunarudia mambo yasiyokuwa na faida kwetu kabisa na ndio maana taifa hili kila mtu anakimbilia kwenye Siasa, au kuimba Bongo Fleva.

Kwa sasa hivi hakuna ngazi hata moja kuanzia msingi hadi wanaohitimu Chuo kikuu anayeweza kujiajiri.... Wote wanazunguka na bahasha kama hatafuti chuo anatafuta kazi.

Tumeshajiuliza baada ya miaka kumi ijayo tutakuwa na population ya watu wangapi? Je tutaweza kutuliza joto la vijana aasiokuwa na ajira huko mtaani? Unaniuliza ni kina nani wanaowaondoa watawala kwenye madaraka katika nchi nyingine? Jibu ni Ukosefu wa Ajira....

Kuna mahali tunakosea na hatutaki kupasahihisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi namuelewa sana huyu mzee!
wp-1465134676780.jpeg
 
Back
Top Bottom