John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Ukweli Kuhusu Wachache au Wengi Kwenda Mbinguni Ukoje
Maandiko Katika Kitabu cha Luka
Kitabu cha Luka 13:23-28, kinasema: 23 "Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika MLANGO ULIO MWEMBAMBA, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje".
Maandiko Katika Kitabu cha Mathayo
Kitabu cha Mathayo 7:13-14, kinasema: 13 "Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache".
Maandiko hayo yanaeleza wazi kabisa, kwamba watakaokolewa ni WACHACHE, kwa sababu njia imesongwa sana.
Swali linakuja, je hii njia imesongwa na nini? Ni wazi kabisa imesongwa na mambo mengi ya kidunia, ambayo ni, anasa, upendaji fedha kupita kiasi, wivu, chuki, tamaa, uasherati ambao sasa upo mpaka kwenye mitandao, mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo.
Pia, kuna mitindo ya wanawake kutembea nusu uchi, burudani na miziki ya kidunia, ufisadi, n.k.
Zaidi ya yote ni kuongezeka kwa wimbi kubwa la manabii wa uongo. Wimbi hilo linasababisha ile njia ya kweli isitambulike kirahisi.
Hivyo, sababu imechanganyikana na njia nyingine nyingi za uongo. Na jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo ile njia ya ukweli inavyozidi kuwa nyembamba zaidi. Imefikia hatua ya kwamba katika baadhi ya maeneo, ukristo wa leo unapimwa kwa kiwango cha mafanikio ya kidunia aliyonayo mtu (kwa mfano utajiri), na siyo mafanikio ya kiroho (yaani utakatifu). Katika maeneo kama hayo, Neno la kweli limetupwa nje.
Bwana Yesu Kristo aliweka wazi, pale aliposema, kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu? Je, katika siku za Nuhu waliokoka watu wangapi? Kati ya mabilioni ya watu, waliokoka watu 8 tu.
Hii inaweza kuonekana hata katika kitabu cha 1Pet 3:20: "watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji". Tunaona kuwa waliokoka watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani wakati ule. Yaani, ni watu WACHACHE sana waliokoka.
Na tena alisema, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.
Luka 17:26-28, 30
26 Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. 27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. 28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma, kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni VIKAWAANGAMIZA WOTE.
30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
Kwa hiyo, kulingana na ushuhuda uliotolewa katika maandiko machache ya hapo juu, tunaona kabisa kuwa kati ya wengi, ni wachache tu watakwenda mbinguni.
Nini Kifanyike ili Wengi Waende Mbinguni.
Biblia inatuambia kila aliyemwamini mwana wa Mungu ni lazima awe na uhakika ya kuwa anao uzima wa milele ndani yake, na kwamba hata akifa leo atakuwa anaishi.
1Yohana 5:13 “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu”.
Turekebishe matendo yetu
Yohana 2:15: “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Unarekebisha matendo kwa kujitenga na mambo yote mabaya ya kidunia hii, kama vile ulevi, sigara, disko, anasa, matusi, miziki ya kidunia, rushwa, visasi, chuki, uasherati, utoaji mimba, vimini, mahereni, mawigi, suruali, lipsticks, wanja, n.k. unajitwika msalaba wako na kumfuata Yesu.
Je, watu wangapi wako tayari kujitenga na mambo hayo? Je, tuonavyo katika hali halisi, ni wengi au ni wachache?
Kujitenga na mambo yasiyofaa ndiyo MLANGO MWEMBAMBA aliosema Yesu Kristo, kupitia maandiko katika vitabu vya Luka na Mathayo.
Tujitenge na mambo hayo, tujitwike msalaba na kumfuata Yesu, ili tuwe miongoni mwa WACHACHE watakaokwenda mbinguni.