Ukweli kuhusu vituo vya kulelea watoto yatima

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,444
25,358
Wakuu naomba nieleweshwe kuhusu mambo haya yanayohusu vituo vya kulelea watoto yatima

1)Utaratibu gani unafanyika ili mtoto apokelewe kwenye kituo cha kulelea watoto yatima

2)Je huyo mtoto analelewa mpaka lini ,kuna ukomo wowote wa kuishi katika hivyo vituo?

3)Je mtoto anasomeshwa mpaka ngazi gani ya elimu, je anasomeshwa mpaka anapopata kazi? Kama jibu ni ndiyo ,je akishapata kazi huyo mtoto atatakiwa naye alipe fadhila?

4)Je ikitokea amefeli kuna uwezekano wa kupelekwa shule za kulipia, vipi kwa wale wanaopata scholarship ya asilimia labda tufanye 50 ya kusoma nje ya nchi ,je gharama zingine zinalipwa na kituo?

5)Ikitokea mtoto ameonesha tabia mbovu zisizo rekebishika ,je watamfukuza?

6)Mtoto akifariki kuna utaratibu gani unaofuatwa?

7)Je wamiliki wa hivyo vituo wanapata faida gani?


8)Je kuna mtu yeyote ambaye amefanikiwa na kujulikana kupitia hivi vituo?

9)Ni taratibu gani zinafuatwa ili ufungue hivi vituo?

10)Kuna utaratibu gani wa kuwanunulia nguo? Je kuna ukomo wowote wa umri wa kununuliwa nguo?

11)Je mtoto akikataa kusoma kuna utaratibu gani wa ziada wanaomfanyia ili mradi hata aweze kutengeneza pesa?

12)Je nguo wanazozivaa zina kuwa zina fanana? Kama hazifanani je si kutakuwa na kaupendeleo hapo kwa maana kuna wengine watabahatika kupata nguo nzuri na za gharama kuliko wengine

13)Ikitokea watoto wanaoishi katika hivyo vituo wakabainika wanajihusisha na mapenzi nini kitatokea??

Embu nijibuni haya maswali
 
Mkuu kuna aina 3 za hivi vituo hivyo hata majibu uatakayopewa huwenda yakatofautiana.
1.VITUO VYA MASHIRIKA YA KIDINI
2.VITUO VYA SERIKALI (sijaviona siku za hivi karibuni)
3.VITUO VYA WATU BINAFSI
 
MAJIBU:
1. Katika vituo vya kidini watoto hawa huwa namavazi yanayo fanana
2.Huishi humo hadi pale wanapo hitimu elimu yao na huhudumiwa hadi wanapopata ajira au wanapokua tayari kujitegemea
3. Huko wanapo lelewa huwa na taratibu wanapo kuwa watu wazima na wao kusaidia wenzao 2 au zaidi kadri awezavyo hadi watakapo jitegemea kwa kusaidiana na mashirika hayo hili htofautiana kati ya imani na imani

N:B WATOTO HAWA HULINDWA NA JAMHURI CHINI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA AZIMIO LA UMOJA WA AFRIKA NA UMOJA WA MATAIFA LA HAKI ZA WATOTO
 
Hapa ni shida kuchangia mkuu,inaonekana kama umetunga mtihani japo majibu huna,hujafanya research yoyote halafu unataka tuku_spoon feed! Hii siyo haki.Anyway kila kituo kimesajiliwa kwa sera yake na havifanani hata umri wa kuingia na kutoka ni tofauti.Mengine katafute.
 
Hapa ni shida kuchangia mkuu,inaonekana kama umetunga mtihani japo majibu huna,hujafanya research yoyote halafu unataka tuku_spoon feed! Hii siyo haki.Anyway kila kituo kimesajiliwa kwa sera yake na havifanani hata umri wa kuingia na kutoka ni tofauti.Mengine katafute.
Haya kakojoe ukalale naona unalalamika lalamika tu
 
Hapa ni shida kuchangia mkuu,inaonekana kama umetunga mtihani japo majibu huna,hujafanya research yoyote halafu unataka tuku_spoon feed! Hii siyo haki.Anyway kila kituo kimesajiliwa kwa sera yake na havifanani hata umri wa kuingia na kutoka ni tofauti.Mengine katafute.
ILA YAPO YANAYO JIBIKA ILA ZAIDI AENDE IDARA YA USTAWI WA JAMII OFISI YA MKOA ALIPO ATAPATA MAJIBU YOOTE BILA TATIZO ILA SIO USTAWI MANISPAA
 
ILA YAPO YANAYO JIBIKA ILA ZAIDI AENDE IDARAVYA USTAWI WA JAMII OFISI YA MKOA ALIPO ATAPATA MSJIBU YOOPTEBBILA TATIZO SI MANISPAA
Ni kweli yanajibika ila ni mengi mno. Ni kama hajawahi hata kuviona anauliza mpaka nguo wanazovaa,ada,matibabu,which is not complex kama alishawahi kuviona.
 
Back
Top Bottom