Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!
Kuna watu wanajiita UMEME JUA wapo karibu na DHL ofisi pale oposity na quality plaza Nyerer road Dar ndiyo wataalamu wazuri wa mambo haya. sina contacts zao, lakini ukienda maeneo niliyoelekeza utawaona tu...... Vile vile wana vifaa vyote vinavyohusu silar systems na ukubwa mbalimbali kutegemeana na wewe utakuwa na vifaa vya uwezo gani kiumeme.Ndugu zangu naomba walio na maarifa kuhusu teknolojia ya umeme wa jua wanipe elimu hivi yawezekana ukawa na umeme wa jua katika nyumba yako na ukatumia umeme kwa vyombo vyote ulivyo navyo kama tunavyofanya kwa umeme wa Tanesco na je gharama zake ni kama Sh ngapi za kibongo?
Nauliza hivi kwani kila siku nikisoma habari za umeme huu nakuta kazi yake ni kuwasha balbu, kuchaji simu na redio pekee.
Nimejenga kibanda changu mahala sasa umeme wa Tanesco nasikia watauleta baada ya miaka mitatu
asanteni. Nipeni desa wataalamu
Ndugu zangu naomba walio na maarifa kuhusu teknolojia ya umeme wa jua wanipe elimu hivi yawezekana ukawa na umeme wa jua katika nyumba yako na ukatumia umeme kwa vyombo vyote ulivyo navyo kama tunavyofanya kwa umeme wa Tanesco na je gharama zake ni kama Sh ngapi za kibongo?
Nauliza hivi kwani kila siku nikisoma habari za umeme huu nakuta kazi yake ni kuwasha balbu, kuchaji simu na redio pekee.
Nimejenga kibanda changu mahala sasa umeme wa Tanesco nasikia watauleta baada ya miaka mitatu
asanteni. Nipeni desa wataalamu
Tatizo ningependa kujua hizo batteries ni kama za gari zina kaa mwaka mmoja na inabidi ubadili au inakuaje , je kama unatumai batteries 7 inamaana ubadilishe zote? thanx
Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!
Asante kwa jibu zuri na dhani nitajiunga kutumia SolarHapana, hizi ni lead-acid batteries na zinadumu miaka mingi tu. Unatakiwa uzitunze kwa kujaza acid (electrolyte) kila baada ya muda kidogo.
Hizi zinaitwa deep-cycle batteries kidogo tofauti na battery za gari. Tofauti yake ni upana wa plates lakini zinatumia the same chemistry kufanya kazi.
¬K
Kwa kuanzia gharama yake yote ya hivyo vikorombwezo hadi umeme jua utumike nyumbani unatakiwa uwe na Tsh ngapi kwa hapa bongo?Ni kweli kwanza inabidi ujue watts ngapi unahitaji. Rahisi kukadiria hizi kwa sababu vifaa vyote vya umeme huandikwa watts zake (au Amps na Volts - Ohm's law itakupatia Watts)
Nyumba ndogo inahitaji kama 3KWatt (nakisia hapa inategeme vifaa). Kwa kweli ni gharama kubwa kujitegemea kiumeme. Bila ya grid (Tanesco ) inabidi uwe na mchanganyiko wa solar, windmill na stand-by generator ili likikosekana jua au upepo utategemea generator.
Tatizo kubwa la umeme wa solar (au wind) ni jinsi ya kuuhifadhi umeme wakati unatengenezwa ili siku za mawingu au usiku uchote umeme kutoka kwenye hifadhi yako. Njia rahisi inayotumika kuhifadhi umeme ni kutumia deep-cycle batteries . Kawaida hizo huwa na uwezo wa 12V. Unatakiwa kutengeneza Battery Bank kwa kuzipangilia battery kama 4 mpaka 8 in parallel or series kutokana na mahitaji ya vifaa vyako.
Kwa ufupi vitu unavyohitaji:
1. Solar Panels (ziko aina nyingi hizi - Tahadhari na wabongo wasikuuzie vioo vya kichina)
2. Charge controller (kwa sababu ya kurekebisha umeme unaotoka kwenye panel usizidi na kuharibu battery)
3. Invertor - Kubadilisha umeme wa jua DC kwenda kwenye umeme wa nyumbani AC. Hizi ziko ambazo unaweka ukutani kwenye plug na ina-supply kwenye circuit yako ya nyumbani.
4. Deep cycle batteries ( hizi ziko kama battery za magari )
Ushauri wangu binafsi ni upate kama solar panels 3 au 4 za 250Watts/each na circuit yako iwe inakunywa umeme kwa matumizi ya taa, fans na vifaa vidogo vidogo. Achana na vifaa vikubwa kama vile Oven.
Kwa kweli ukishapata vifaa hivyo (ukimpta mdau akakutolea China bei poa) kufunga ni rahisi sana unahitaji elimu ya darasa la saba tu. Uchawi wa umeme wa jua ukishavifunga vifaa vyote basi unacheka tu kwasababu hamna bili tena na hivi
vitu hudumu kama miaka 30 hivi. Angalia mchoro hapo chini.
¬K
Kwa kuanzia gharama yake yote ya hivyo vikorombwezo hadi umeme jua utumike nyumbani unatakiwa uwe na Tsh ngapi kwa hapa bongo?
Hata mimi pia ni mtumiaji wa umeme huu. Tatizo la umeme huu vifaa vyake ni ghari mno.Mheshimiwa naona umekata kiu ya wengi japo tulikuwa hatujauliza. Ninatumia solar pia kwa miaka miwili pia kwa taa, radio na tv. Mtaalamu aliniambia kuwa solar energy kwa sababu inaproduce current kidogo isingeweza kutumika kwa pasi au heater.
Je yawezekana habari hii kuwa kweli an fix? Nisaidie ili kama siyo nione uwezekano wa kuitumia kwa pasi pia.