Ukweli kuhusu Okwi ni upi?

Ukweli kuhusu Okwi ni upi?

Tiger

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2007
Posts
1,747
Reaction score
387
Jamani kuna ndugu yangu(Simba damu) anakaribia kuchanganyikiwa huku.
Hebu nisaidieni habari za uhakika, Okwi ka-sign Yanga kweli? au kama ni uzushi, ukweli ni upi?
Heshima kwenu.
 
Mkuu mimi ni mwanasimba na nitakueleza yaliyosemwa na makamu m/kiti wa Simba jana wakati akiongea kwenye kipindi cha michezo cha magic radio, Kaburu alisema Okwi alifanya majaribio na timu ya Austria na ikaonekana amefanya vizuri na kilichobaki ni kwamba kama timu ile wataamua kumchukua watafanya mawasiliano na Simba na kama watafikia makubaliano Simba itamwachia aende zake Ulaya, wakati wote huo akisubiri dili kukamilika atakuwa na timu yake ya sasa ya Simba na kama dili halitakamilika ataendelea kuitumikia timu ya Simba mpaka mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa ligi msimu ujao.

Kuhusu kusaini Yanga bado watu wanaendeleza rumors na wengi wanasema yasije yakawa kama ya Waso tuliambiwa anaenda ubeligiji baadaye akaibukia jangwani.

Kwa maoni yangu kwa sasa tumwamini kwanza makamu m/kiti kwa kauli ambayo nimeieleza hapo juu na kama wanasimba tuacheni na tetesi za yeye kwenda Yanga lakini uhakika ni kwamba yeye bado ana mkataba na Simba hadi mwakani.
 
hata mm sielewi maana kila mtu anasema lake ngoja tusubiri maana mvumilivu ula mbivu
 
Heshima kwako mkuu,
maelezo yako yanaonesha kweli we ni simba damu kama ndugu yangu.
Mi si mshabiki sana wa football ila nikisoma btwn the lines naona hili swala limekugusa sana kama huyu ndugu yangu.
Imefikia hatua jama a anasema bora Okwi auzwe kokote lakini si Yanga.
Yani kavulugwa ile mbaya.
Hope hii taarifa itamtuliza kidogo.
Asante.
 
Mzee Akilimali ameshasema kuna mchezaji Yanga itamsajili watu watashtuka sana/hawataamini...wapo watakaochanganyikiwa kama ndugu yako na wapo watakaoingia kwenye siku zao kabla ya wakati wao kama Cras(...)
 
Mkuu umenifurahisha sana na wenye mimba lazima zitachomoka.tehe tehe
Mzee Akilimali ameshasema kuna mchezaji Yanga itamsajili watu watashtuka sana/hawataamini...wapo watakaochanganyikiwa kama ndugu yako na wapo watakaoingia kwenye siku zao kabla ya wakati wao kama Cras(...)
 
Hivi simba ni Okwi tu hakuna wachezaji wengine wa kuibeba timu, mtaaza visingizio kuwa tulikula tatu kutoka kwa azam kwa sababu Okwi hakuwepo, tumekosa kagame kwa sababu ya Okwi, ya nini kulazimisha mchezaji ambaye hana mahaba na simba
 
Okwi yuko Simba na bado ana mkataba nayo hadi june 2013. Watu wataongea na watatoka sana mapovu mwaka huu..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mzee Akilimali ameshasema kuna mchezaji Yanga itamsajili watu watashtuka sana/hawataamini...wapo watakaochanganyikiwa kama ndugu yako na wapo watakaoingia kwenye siku zao kabla ya wakati wao kama Cras(...)
ha ha ha ha ha vijana wangekuwa wana uwezo wangekuroga.. yaani wanisi kufa kufa kila wakifikiria okwi ndani ya uzi wa njano
 
Acheni kuishi kwa matumaini nyie.. Jana imetangazwa ktk mkutano Mkuu wa Simba kama Yanga wanamhitaji wakae mezani na uongozi wa simba. Bei poa tu dola Millioni 2 yan Tsh 3Bil. Bei imepunguzwa sana ukizingatia hali ya uchumi ya nchi yetu. Na pia hii inatokana kwamba bado yuko ktk mipango ya Prof Milovan. 3Bil nn bwana kwa Manji wenyewe wanamuita 'habari ya jiji'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi simba ni Okwi tu hakuna wachezaji wengine wa kuibeba timu, mtaaza visingizio kuwa tulikula tatu kutoka kwa azam kwa sababu Okwi hakuwepo, tumekosa kagame kwa sababu ya Okwi, ya nini kulazimisha mchezaji ambaye hana mahaba na simba
Kama Mrisho Ngassa?????!!!!
 
Back
Top Bottom