Ukweli kuhusu mapenzi

Ukweli kuhusu mapenzi

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
335
1. Unaempenda kamwe hatokupenda bali atakudanganya.

2. Anaekupenda kweli utampotezea na utamkimbilia mwenye maumivu na mateso.

3. Ukihitaji furaha kutoka kwa unaempenda mara nyingi huishia maumivu.

4. Upendo wa kweli ni kujipenda mwenyeo maana hakuna atakae kuumiza.

5. Ni kweli mapenzi huwa matamu lkn mwanzoni kwasababu kila mmoja hujipamba na kila zuri.

6. Wanaopenda kweli kutoka ndani nyoyo zao huishia utumwani kwenye mapenzi.

7. Ukitaka kuonekana mjinga zaidi basi toa machozi na ulie kwa ajili ya mapenzi ingawa uko sahihi maana dalili ya moyo kuuma ni kilio.

8. Unapojaribu kuwa mwaminifu na mkweli kwenye mapenzi watu hukuona mshamba.

9. Ni kweli sisi binaadamu hutambua thamani ya kitu baada kutoweka. Lakini pia hutamani ambavyo havijatufikia.

10. Kulala na mwanamke ni kuridhisha matamanio, kukubali kuumia kwa ajili ya mtu ndio kupenda.

11. Binaadamu alivyokuwa si wa shukran akipendwa hufanya yanayochukiza, akipuuzwa hujipendekeza.

12. Ukiona watu wanakusifu kwasababu ya uzuri fahamu wanataka kusambaratisha furaha yako maana sisi watu tunapenda kuteketeza yaliyo jipamba.

13. Watu wa dunia ya sasa tunanunua mapenzi watu wa zamani walishibana kwa amani.

14. Usimuamini mwanamke hata kwa uchache maana akili zake ni matamanio.

15. Usimtese mwanamke kwasababu wana nyoyo za huruma kwa maana walitubeba miezi tisa bila ya kulalamika.

Written by @Travis Walker
 
Mapenzi!!?? Naona hili neno limepambwa na sifa zisizo zake.

Hakuna kitu mapenzi katika ubinadamu zaidi kila upendo wa kibinadamu una manufaa kwa anaeutekeleza. Maana yake ni kwamba kila anayempenda mtu kuna kitu ananufaika nacho au atanufaika nacho. That is the way of life.
 
Ni kweli ila siyo kila mwanamke anahuruma kwako ila ni huyo alokubeba tumboni kwake miezi tisa maana wengine ni kuumiza,
Kwahiyo hata wanaume wanateswa/Tunateswa sana na hao wanawake kikubwa ni KUPENDANA,KUTHAMINIANA,KUJALIANA,KUSHIRIKIANA ila siyo KUTAMANIANA
 
Usitochose na Mapenzi ulio experience Wewe...

Tuache tujioneee wenyewe...
 
Mapenzi!!?? Naona hili neno limepambwa na sifa zisizo zake.

Hakuna kitu mapenzi katika ubinadamu zaidi kila upendo wa kibinadamu una manufaa kwa anaeutekeleza. Maana yake ni kwamba kila anayempenda mtu kuna kitu ananufaika nacho au atanufaika nacho. That is the way of life.
Kabisa mkuu...watu walio erevuka wanao jua Mambo ...hutoa comment Konki

mzabzab come and get schooled.
 
Ni kweli ila siyo kila mwanamke anahuruma kwako ila ni huyo alokubeba tumboni kwake miezi tisa maana wengine ni kuumiza,
Kwahiyo hata wanaume wanateswa sana na hao wanawake kikubwa ni KUPENDANA,KUTHAMINIANA,KUJALIANA,KUSHIRIKIANA ila siyo KUTAMANIANA
Wazo pia
 
Mapenzi!!?? Naona hili neno limepambwa na sifa zisizo zake.

Hakuna kitu mapenzi katika ubinadamu zaidi kila upendo wa kibinadamu una manufaa kwa anaeutekeleza. Maana yake ni kwamba kila anayempenda mtu kuna kitu ananufaika nacho au atanufaika nacho. That is the way of life.

Expectation sio kanuni ya upendo tu. Mwanadamu chochote anachofanya huwa ana mategemeo na hio ndio kanuni ya maisha. Sio kwenye kupenda tu ila tunapozungumzia hisia tofauti tofauti basi mara kwa mara zinatupelekesha ili tufikie hamu ya kuridhika kwetu. Mapenzi ni hisia ila ni hisia yenye nguvu kutokea kuumbwa. Wengi tunashindwa kutofautisha kati ya hisia na matamanio
 
Mbona umeegemea kwenye negativity sana ina maana kwenye mapenzi hamna jema?
 
"Usimtese mwanamke kwa sababu wana nyoyo za huruma kwa maana walitubeba miezi tisa bila ya kulalamika"
 
16. Usimwamini mwanaume hata kwa uchache maana hujui ni lini atakugeuka hawa watu ni manyoka
 
Silaha ni shilingi beibii, kupendana zamani... ndo venye wanasemaga!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom