Ukweli kuhusu habari za Afisa wa Polisi aliyedaiwa kutelekeza familia

Status
Not open for further replies.

mwanjara

Member
Jul 17, 2016
21
6
Malalamiko=> Afisa huyu kalitia aibu Jeshi la Polisi

Afisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha ASP Amos Aron Mwakajoka aliyehamia Dodoma Central akitokea Kizuiani(OCS) katelekeza mke na watoto watatu line police NASACO block no.8. Hii ndio nidhamu mnayofundishwa?

Au yale maadili mnayoimba katika wimbo wenu "Nikiwa afisa wa police"?

Hili linatusikitisha sana sisi majirani raia tunaoishi nje ya kambi yenu tunapomuona huyu Mama mke wa afisa wa jeshi la police kugeuka ombaomba. Kibaya zaidi hadi watoto hawasomi tena!

Jamani michepuko sio dili bakini njia kuu! Mnawatesa malaika wasiokua na hatia, ndo mnapewaga sijui madawati ya jinsia sasa huyu askari anaweza kutoa huduma gani kwa raia akipatwa na matatizo yanayohusu kutelekeza watoto?

Muwe na aibu nyote wenye hizi tabia!


Majibu...

Habari hiyo ilikuwa na kichwa cha habari kinachosema "Afisa huyu alitia aibu jeshi la polisi" iliyotumwa na mtu anayejiita Mama Tuntufye.

Ukweli ni kwamba mwanamke huyo hajatelekezwa bali ameachwa... ambapo ndoa hiyo ilivunjwa na mahakama (ambapo hata hivyo walikuwa hawajafunga ndoa) tangu June 17 kwenye mahakama ya mwanzo Mbagala Kizuiani mwaka huu ambapo shauri la kwanza lilikuwa ni kuvunja ndoa, la pili lilikuwa ni huduma ya watoto na la tatu ni mgawanyo wa mali.

Baada ya kesi kusikilizwa hukumu iliyotolewa ni kwamba kwanza ndoa hiyo ilivunjwa pili iliamriwa n mahakama kuwa watoto wawe wanapewa sh 200,000 kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto na mgawanyo wa mali ambapo ulitakiwa ugawanywe pasu kwa pasu.

Pamoja na hayo yote watoto wote wana bima ya afya kwa ajili ya matibabu.
Na kuhusu suala suala la mwanamke huyo kuendelea kuishi pale line polisi Nasaco yeye mwenyewe aliomba aendelee kuishi pale hadi pale hati ya hukumu itakapotolewa Agosti mwaka huu ili apate haki zake zote alizoamriwa kupewa na mahakama ikiwemo kiasi cha sh milion moja ya fidia.

Lakini baada ya hukumu kutolewa na mahakama siku mbili alionekana kwenye kanisa la maji meupe lililopo Mbagala maji matitu akiomba msaada akiwa ameambatana na watoto akidai ametelekezwa na alipatiwa msaada.

Baada ya hapo alielekea pasipojulikana na kuwatelekeza watoto kwa dada yake kwa muda wa wiki mbili mpaka juzi julai 10 aliporudi na kuwachukua watoto na kudai kwamba hawana ada ya shule na wakati ada hiyo aliachiwa na mumewe tangu mwezi March pamoja na pesa za matengenezo ya gari yao kiasi cha sh milioni nne zilizokuwa benki.

Na kwa kipindi chote cha maisha yao ya ndoa tangu mwaka 2009 kadi ya benki, mshahara na posho vyote alikuwa anamiliki yeye mwanamke hadi June 7 ilipofungiwa akaunti hiyo.

Hata hivyo June 26 alitumiwa pesa za matumizi ya watoto kiasi cha sh 200,000 Kama ilivyoamuriwa na mahakama na katika kipindi chote hajawahi kukosa pesa kwa ajili ya huduma za watoto.

Baba yao alipowaomba watoto wake mbele ya mahakama ili aishi nao walimkatalia mpaka hapo watakapofikisha umri wa miaka 12.

Baba huyo hakuchoka alipeleka ombi la kuishi na watoto wake kwa ndugu wa mke aishiye Mikocheni ili waweze kuongea na ndugu yao aweze kuwaruhusu watoto wakaishi na baba yao lakini alikataa na kuwakana ndugu zake wote na kuwatukana mbele ya kikao hicho.

Chanzo cha kuachana kwao ni kukosa maelewano kati yao ikiwa ni pamoja na mwanamke kujilimbikizia pesa zote hali iliyomfanya mwanaume kukosa hata pesa za kujikimu kimaisha mahali anapoishi sasa.

Pia alikuwa anamgombanisha mume wake na ndugu zake kwa kumwita mama mkwe wake mchawi kwa madai kuwa anamroga mtoto wake wa pili pamoja na lugha za matusi alizokuwa anazitimia kwa mume wake na kwa familia ya mwanaume.

Tuhuma hizo zilileta vurugu ndani ya familia ambapo mwanaume huyo aliamua kuachana na mwanamke huyo na kuoa mke mwingine.

Hivyo ifahamike kwamba mwanamke huyo hajatelekezwa bali ameachwa na mume wake anaendelea kutoa huduma kwa watoto wake kama kawaida.

Inasikitisha sana kuona mama Ntuntufye anatumia mitandao ya kijamii kumdhalilisha afisa huyo wa polisi ili aonekane mbaya mbele ya jamii.

Hata hivyo hatua za sheria zitachukuliwa dhidi yake kwa kumdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii.

b68b81bf39f83c11a54a58c67bfcecc0.jpg
 
Haja telekezwa ameachwa baada ya kufunga ndoa na mke wangu mpya alienda kulalamika makao makuu ya Polisi hakuridhika akaja kwa kamanda wa Polisi mkoa akashauriwa afungue kesi mahakamani akafanya hivyo mahakama ilitoa maamuzi kwa vile tulizaa watoto hatukufunga ndoa,lakini kisheria kwa vile tulikaa muda mrefu ilisomeka kuwa ndoa hivyo ikaivunja ndoa hiyo na kuamuru matunzo ya watoto kila mwezi Tsh 200,000 laki mbili awali alikuwa
b68b81bf39f83c11a54a58c67bfcecc0.jpg
Kwa hiyo laki mbili zinatosha kulipia ada ya watoto wawili wanaosoma holy cross na mahitaji mengine?
 
Mtu mzima hovyo,wenzio wanawaza maendeleo wewe unawaza kuoa,ukipata mwingine zaidi ya huyo mpya nae utamtelekeza.
 
huyo mama aende tu ustawi wa jamii, hayo ya uongo na ukweli mnajua huko chumbani,
somesheni watoto muwape malezi bora,
hayo mengine ni juu yenu.
 
Alichokuwa ana lalamika yule dada ni kutelekezwa na kamanda na shemeji kugeuka omba omba ...kikubwa malafyale ni kumpatia fedha za kukidhi mahitaji ya watoto wako ambao bado wanahitaji malezi ya baba na mama ...kikubwa malizana na shemej yetu kiutu uzima ...acheni kuja huku kutudhalilisha wanakyusa bhana ...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom