waterproof
JF-Expert Member
- Aug 14, 2020
- 388
- 352
Kuna minong'ono na maneno ya wazi kwamba kuna viumbe wa ajabu wamekimbilia katika dunia na kusababisha hofu na wasiwasi wa maisha ya binadamu wa kawaida, kwa mujibu wa mwanasayansi wa fizikia na nyuklia raia wa Canada Bwana Stanton Friedman aliwahi kunukuliwa akisema, "dunia imekua ikitembelewa sana na viumbe wa ajabu maarufu kama Aliens kwa lengo la kuangalia mienendo kadhaa ya kitekinolojia na maisha ya kawaida na muda sio mrefu wataweka makazi kabisa duniani, Hakuna doa la mashaka kwamba viumbe wa ajabu wenye akili nyingi sana wanafanya safari zao kuja duniani".
Bwana Friedman mwenye umri wa miaka 82 alikua akichunguza ajali ya chombo cha anga za juu hususani ajali ya mwaka 1947 iliohusu chombo cha anga kilichopata ajali mbaya katika anga za juu na kueleza kilipotezwa na kitu kisicho cha kawaida kabisa kilichokua na viumbe wa ajabu,
Aidha, aliwahi tena kunukuliwa akisema kuwa, faili lenye taarifa za siri sana za CIA juu ya uwepo wa viumbe hao ni moja ya ushahidi wa uwepo wa viumbe hao, nafikiri viumbe hao maarufu Aliens wanataka kulinda anga lao ambalo limekua likitembelewa sana na vyombo na binaadamu kutoka duniani.
Naye aliekua Waziri wa Ulinzi wa Canada Paul Hellyer aliwahi kunukuliwa akisema kuwa "dunia imekua ikitembelewa na viumbe hao kwa miongo kadhaa sasa, mwaka 1961 kulikua na vyombo vya anga vya ajabu 50 vilivyojulikana kama UFO na visivyo vya kawaida kabisa vikiruka kutoka kusini ya dunia vikielekea Urusi na Ulaya."
PIA,
Mtafiti wa masuala ya Aliens, Stewat Swardlow, na wengine wengi wamewahi kushuhudia kwa nyakati tofauti nyaraka za siri kutoka kwenye serikali tofauti tofauti kubwa duniani kama vile Marekani,China,Urusi,Japan,Ujerumani na nyingine zikionesha ukweli wa uwepo wa viumbe hawa.
Zifuatazo ni 4 kuu na kubwa za Aliens wanaopatikana kwenye mkanda wa Kuiper Belt...
1;Insectoid Aliens
2;Grey Aliens
3;Humanoid Aliens
4;Reptoid Aliens
Aina hizi ndizo ambazo serikali nyingi za dunia zimekubaliana na uwepo wake,lakini kwa siri kwa sababu ndiyo aina ya Aliens ambayo imewahi kuonekana hapa duniani. Lakini tujue kwamba,kama nilivyosema hapo juu ni kwamba wataalamu hawa wanasema kwamba kwenye mkanda wa Kuiper kuna mamia ya aina za Aliens lakini wanasema kwamba Aliens aina ya Insectoid ndiyo super power huko...
Insectoid, wanadaiwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuweza kuiongoza au kuirubuni akili ya kiumbe mwingine afikiri kama atakavyo yeye na hii ndiyo imefanya wakawa na nguvu sana eneo hilo ambalo limezua mjadala na vurugu sana baina ya wataalam wengi.Kwa maana hiyo Insectoid ndiyo aina bora zaidi ya Aliens inayopatikana eneo hilo.
Hawa viumbe ni hatari sana kwa maisha ya binadamu na karibia kila kundi la Aliens lina ajenda yake kuhusiana na binadamu na dunia hii. Kama nilivyosema kuwa kuna aina nyingi ya Aliens,hapa nitaeleza makundi machache ya Aliens na ajenda zao dhidi ya dunia na sisi wakazi wake....
#Mantids_Aliens.
Hawa wao wanadai kuwa dunia hii ni yao na waliishi hapa kwa miaka mingi kisha wakaondoka kwenda kutafuta maisha maeneo mengine na sasa wanahitaji kurudi.
#Lionestic_being_Aliens.
Hawa wanafanana sana na binadamu lakini pia wanafanana na Simba. Nimekosa picha ya kuonesha namna wanavyoonekana lakini inastaajabisha sana.Hawa lengo lao ni kuondoa mtindo wa kisiasa ulioko hapa duniani.Hawa wao watasubiri hadi tumeshamalizana sana na ndipo watakuja na kuondoa kabisa mtindo huu wa siasa ulioko hapa duniani....
#Humanoid_Aliens.
Hawa ni miongoni mwa Aliens wengi na wenye uwezo mkubwa sana na wa hatari. Inadaiwa kwamba miongoni mwa aina za hawa humanoid Aliens ipo aina ambayo inafanana kabisa na binadamu na unaweza kukaa naye kwenye kiti na usijue kama siyo binadamu. Hawa wanaamini kuwa dunia hii iko chini ya mamlaka yao na ni eneo lao. Wanataka kuisafisha dunia yote na kuhakikisha hakuna binadamu anabakia hapa. Wanaamini wana haki ya kufanya yote na chochote watakacho na ajenda yao kubwa ni kuwaondoa binadamu.