UKUTA inafeli vibaya

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,836
Reaction score
1,845
Habari wakuu,

Ikiwa zimebaki siku 15 tu kuanza kwa ile oparesheni yetu maarufu ya UKUTA, mambo si shwari hapa Ufipa.

Mpaka sasa duru zinaonyesha hii kitu itashindwa vibaya hasa baada ya makamanda wenye ndoa kuingia mitini katika kuisupport operation hii. Zile juhudi za JOYCE KIRIA kuhamasisha wake na familia za makamanda kuwazuia kushiriki zimezua taharuki kubwa kwani zinaonekana kufanikiwa kwa kasi huku zikiungwa mkono pia kwa kasi kubwa na wake wa viongozi, ambao ni members wa BAWACHA.

Wake hao wamembana kooni mwenyekiti wao na kumzuia kutoa tamko lolote kuhusu UKUTA, ndo maana mpaka sasa BAWACHA wako kimyaa kama maji.

Kumekuwa na vikao vya dharura vya kutosha, vikilenga kuhakikisha CC inatafuta suluhisho au mwanya wa majadiriano na Mh Rais ili kuepusha "kikombe hiki" ambacho wamekitangaza lakini zimegonga mwamba hasa baada ya upande wa rumumba kukataa katakata.

Kwa kweli UKUTA mpaka sasa mustakabari wake haueleweki, kwani ilipangwa mwezi mzima wa nane utumike kuhamasisha kupitia MITANDAO YA KIJAMII, hatahivyo hili pia halijafanikiwa kwani JOYCE Kiria na team yake wameliwekea upinzani wa kutosha.

Ikumbukwe hata Mgeni wetu maarufu Ndugu EL hauingi mkono mkakati huu wa mwenyekiti,kwani amewahi kutangaza hadharani kuwa siasa za kiharakati na maandamano si STYLE yake. Kutokuungwa mkono na EL pia kunaacha pengo kubwa kwani timu ya vijana iliyo nyuma yake nayo imeamua kukaa kimya.

UKUTA unaelekea kuanguka kabla hata haujasimama, Ufipa hata vikao havikaliki huku. Ingawa mambo ni magumu ila tumeapa HATUNYWI SUMU WALA KUJINYONGA
 
Watu wenye dhamira hawasemi hadharani subiri Muda ufike uwaone barabarani, time will tell us
 
Walimcheka sana Dr Slaa na kusema amekaliwa na mama Josephine....ngoja wao tuone nani ana "final say"....
CC BAWACHA, Nifah
 
Ingekuwa inafail usingekuja kuandika huku!!!
 
ukuta unatangazwa mzee magu kwenye mikutano yake hivyo hakuna haja ya kuharibu pesa kwa ajiri ya matangazo...ndio maana nape amezuia vyombi vya habari visivungumzie ili serikali iwasaidie
 
ukuta unatangazwa mzee magu kwenye mikutano yake hivyo hakuna haja ya kuharibu pesa kwa ajiri ya matangazo...ndio maana nape amezuia vyombi vya habari visivungumzie ili serikali iwasaidie
Thibitisha kuwa Nape kazuia vyombo vya habari mkuu,
 
Unakuja kupima upepo ili uone mwitikio wa watu ukoje..we Subiri ujionee siku hiyo ndo mtashika vizuri viuno na huyo dada ako Joyce kwa mshangao
 
Hii miradi kwani mnalipwa bei gani? mbona ni substandard sana?inapangwa kizembe sana (as always)kwanza kwa kumtumia Joy kisha hiki ulichoandika
lakini kiukweli mambo si shwari huko kwenu na kila kitu kiko wazi kabisa...Ndugai mliyekuwa mmmemtenga ndie mnayemtegemea kwasasa awe mkombozi, bob kaacha majukumu ya kitaifa kavamia kazi za katibu mkuu na katibu mwenezi
 
Mkuu hii habari ni mpya, Kumbe Joyce anatumika?? kwaiyo ndugu yetu kamanda ...hayuko salama??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…