UKUTA HAUNA CHAMA
Na Mbusule C.Shillu,
Katika nchi yoyote ile kunapoibuka vimelea vya Udikteta, kila mwananchi anawajibika kuukemea kwa nguvu na akili zake zote maana athari zitakazojitokeza kama matokeo ya Udikteta huo zitawakumba wote bila kujali dini, kabila, kanda wala mrengo wa Kisiasa.
Kwa muda mfupi wa serikali ya awamu ya 5, kumekuwepo na dalili za dhahiri za vimelea hivyo hatari. Leo nitatolea mfano maeneo machache tu.
Utumbuaji majipu;baada ya kuingia kwa awamu ya 5,wimbo maarufu ulikuwa ni kutumbua majipu ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walitenguliwa uteuzi kwa tuhuma kuwa ni mafisadi. Hili lilifanyika bila kufuata sheria ya utumishi wa umma maana walitumbuliwa bila kupewa nafasi ya kujitetea wala kushirikisha vyombo vyao vya kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma. Mathalani, kutumbuliwa kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mzee Kabwe kulifanyika kwenye mkutano wa uzinduzi wa Daraja la Nyerere ambapo RC Makonda alitoa tuhuma dhidi ya Mkurugenzi huyo, Rais akatangaza kumtumbua palepale. Kutokana na Utumbuaji huu nchi imeongeza watumishi hewa wengi sana kwani inaelezwa kuwa waliotumbuliwa bado wanalipwa na serikali jambo ambalo ni mzigo kwa walipa kodi ambao ungeweza kuepukika km wangefuata utaratibu wa kuchukua hatua. Pia, Kama kweli tuhuma hizi ni za kweli,kwa nini wakurugenzi wa Halmashauri,DAS, wakuu wa Wilaya na Mikoa waliotumbuliwa hawajafikishwa mahakamani mpaka sasa? Maamuzi ya kutokuzingatia utaratibu hayana jina jingine zuri kuliko UDIKTETA.
Bei ya Sukari; Ilielezwa kuwa kuna wafanyabiashara wanaficha sukari, hivyo serikali ikaagiza watu hao kuuza sukari yao mara moja na atakayegundulika ameficha au anauza sukari zaidi ya bei elekezi ya Serikali, 1,800 atachukuliwa hatua ikiwemo kugawa sukari hiyo bure. Ikasemekana kuna shehena ya Sukari imekamatwa huko Mbagala na Tabata. Baada ya pale hatukusikia watu hao kufikishwa mahakamani wala sukari kugawiwa bure kokote. Serikali ikapiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje. ..baadaye tena km hali ya kujikanganya yenyewe ikaanza kuagiza sukari yenyewe,bei yake sasa ni kati ya 3000-4000. Maamuzi haya nayo yanaonekana hayakushirikisha wadau, UDIKTETA
Kodi kuongezeka kwenye utalii; hili nalo limesababisha watalii kupungua kwa kiwango kikubwa nchini. Matokeo yake vijana waliokuwa wanafanya kazi km Tour guide, porter, wasafirishaji wa watalii na mahotelia kupoteza ajira. Mathalani, Landmark Hotel kugeuka Hostel kunahusishwa na hili.
Kodi kubwa bandarini; nalo limekimbiza meli nyingi na matokeo yake Makampuni ya usafirishaji yanafungwa ama kufirisika. Bandari kavu nayo imekauka kwa mkumbo huu. Bidhaa sasa zinapitia Zambia na Mombasa. Matokeo yake gharama za Maisha kwa mtanzania wa kawaida zinazidi kupaa. Makampuni mbalimbali yamepunguza wafanyakazi kwa sababu ya kuongezeka kwa kodi na bidhaa kuadimika.
Kutokana na mlolongo huu mkubwa wa kodi pamoja na matamko ya kila uchwao, wawekezaji wamepungua kwa kiasi kikubwa nchini. Mazao ya shambani na malighafi sasa hazina soko tena. Mathalani: Mbaazi ilikuwa inanunuliwa 1800, sasa inauzwa 1100; wakulima walikuwa wanasukuma garish moja la mihogo kwa siku moja lakini kwa sasa inakaa bila mteja mpaka siku 3-4 na baadaye kuuzwa kwa bei ya kutupwa; matunda yalikuwa yananunuliwa na wakenya kwa oda maalum lakini sasa yanajiozea ama kuuzwa kwa bei ya kutupwa Buguruni. Kulima kumekuwa karaha. ...
Tozo zisizoeleweka kwa Mabodaboda; Sasa wanakamatwa hovyo na kulipishwa faini kila mahali. VAT imeongezeka mara dufu kwa wanaotarajia kununua pikipiki.Bodaboda si kimbilio tena kwa vijana. ..
Walimu; Kwa siku chache za utawala huu wamedhalilishwa vya kutosha. Mathalani; Kulazimisha kukesha kwenye Mwenge huko Sengerema na kusainishwa kwenye daftari saa nane usiku, kuamuliwa kulipa dawati likivunjika, kuhakiki watumishi hewa mstarini, kulazimishwa kuchangia Madawati na udhalilishaji mwingine mwingi.
Kupoka mamlaka ya Halmashauri ya kukusanya mapato. Ikumbukwe kuwa Halmashauri zote zipo chini ya TAMISEMI ambayo mara baada ya Utawala 5 kuingia ilitolewa ofisi ya waziri Mkuu na kupelekwa kwa Rais. Halmashauri za majiji ambako UKAWA walishinda kulikuwa na mizengwe mingi sana kwenye chaguzi za mameya. Kwingine km Jiji la Tanga uchaguzi ulifanyika kibabe kwa kumtangaza Meya wa CCM pamoja na ukweli kwamba hakushinda na ndiyo maana vikao vya baraza la madiwani havifanyiki huko. Mambo km hayo yalifanyika pia Halmashauri ya Kilombero. Kwa upande wa Dar es Salaam CCM katika kujiongezea idadi ya wajumbe ilileta mpaka wabunge kutoka Zanzibar kuja kupiga kura Bara kinyume kabisa na Katiba na Sheria za Serikali za Mtaa sababu TSMISEMI si jambo la Muungano lakini UKAWA wakasimama kidete kwa hoja na kutumia Mahakama wakashinda. Baada ya UKAWA kushinda, serikali ya CCM katika kuwakwamisha imewanyang'anya vyanzo vya mapato kama Property Tax ambayo ilikuwa inachangia kati ya 30-40% ya pato la Halmashauri hizo.Pia, Wamezuiwa kusafiri kwenda nje kutafuta wawekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo km ambavyo Halmashauri ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA toka 1995. Mathalani:Safari ya Uturuki ya Mameya wa Dar es Salaam iliyokuwa imefadhiliwa kila kitu na Serikali hiyo ilizuiliwa. Lengo ni kuwakwamisha ili baadaye waonekane hawakufanya kitu. Narudia TAMISEMI kwa sasa ipo chini ya Rais, connect the dots.
Machinga pia hawako salama maana kila uchwao serikali inatoa matamko ya kujikanganya kuhusu hatma yao mijini. Mathalani; Baada ya tamko la Rais huko Mwanza kuwa Machinga waendelee kufanya biashara mijini, Simbachawene akiwa Dar es Salaam alisema kuwa Rais alimaanisha Machinga wa Jiji la Mwanza tu. Ikumbukwe kuwa kwenye majiji yote 4 nchini, CCM kwa idadi ya Madiwani ilishinda Jiji la Mwanza tu. Hivyo, huu nao unaweza kutafriwa km mkakati kabambe wa kuzigombanisha Halmashauri zinazoongozwa na UKAWA kwa wananchi. Katika yote haya anayeumia si Meya wa upinzani ila Mwananchi mwenye chama na asiye na chama.
Siku nyingine nitagusia namna ambavyo kada zingine zilivyoathiriwa na utawala huu ndani ya muda wa miezi 9 ya madaraka.
UKAWA WANADAI DEMOKRASIA ILI HAYA YASEMWE KWA WAZI, SERIKALI IJISAHIHISHE KAMA AMBAVYO ILIKUWA IKIFANYIKA SIKU ZOTE KWA UPINZANI KUIBUA KASHFA NA WAHUSIKA KUWAJIBISHWA. ...
Nimechagua kusema Ukweli!