Ukulu: Viongozi wa dini si malaika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukulu: Viongozi wa dini si malaika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Jun 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SIKU moja baada ya viongozi wa dini kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina ya baadhi yao wanaojihusisha na biashara ya dawa za
  kulevya, Ikulu imeshindwa kutaja majina hayo, badala yake ikasema kauli hiyo haikutarajiwa kutoka kwa viongozi hao kwa kuwa nao si malaika ama watakatifu hapa duniani.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana na kusainiwa na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Bi. Premy Kibanga, kauli ya viongozi hao wa dini ni ya kusikitisha na haikutarajiwa kutoka kwao.


  "Viongozi wa dini ni watu wa kutumainiwa sana katika jamii yeyote, lakini ikizingatiwa kuwa wao sio malaika ama watakatifu hapa duniani, nao wanatumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa kabisa," ilisema taarifa hiyo.


  Badala ya kutaja majina ya wauza 'unga', taarifa hiyo ilieleza kuwa hivi karibuni wapo viongozi wa dini waliokamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili ya jamii na wapo ambao wamekamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, lakini wapo wanaochunguzwa hivyo kutokana na hayo viongozi hao hawakutakiwa kujitetea kwa kauli nyepesi kwa kumpa Rais saa 48."


  Ilisisitiza kuwa kiongozi anayejishuku ajisalimishe mwenyewe na anayeshukiwa na jamii afichuliwe ili afanyiwe uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake, lakini si kusubiri Rais awataje hadharani ndiyo viongozi hao waanze kuchukua hatua.


  Vyombo vya habari jana viliwakariri baadhi ya viongozi wa dini wakimpa Rais Kikwete muda wa saa 48 kuwataja viongozi aliowatuhumu kwa ujumla kuwa wanajihusisha na biashara hiyo haramu.


  Taarifa hiyo ilifafanua mambo aliyoyazungumza Rais Kikwete kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu John Ndimbo wa Jimbo la Mbinga ambapo Rais Kikwete alitoa ombi la kuwataka viongozi hao kujihusisha kikamilifu katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.


  "Ni tatizo linalozidi kukua pamoja na jitihada za Serikali kupitia vyombo vya usalama kuwabana, kuwawajibisha watumiaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Athari zake kwa jamii zinaeleweka, hivyo sihitaji kuzirudia...


  "Kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya na hiyo inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama, lakini inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu.


  "Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaostahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa, Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya," alisema.


  Taarifa hiyo iliongeza: "Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama kweli, ni wa rangi gani? Unatakiwa kushtuka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumwondoa nyumbani kwako hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako, hivyo Rais alikuwa na nia njema katika kulielezea jambo hili, na mwenye nia njema haumbuki," ilisema taarifa hiyo.


  Pia viongozi hao walitakiwa kuweka mikakati na vipaumbele vya kufanyia kazi changamoto hiyo na sio kuahirisha tatizo hili ambalo linazidi kuwa kubwa na kazi ya kupambana na dawa za kulevya haimhusu Rais peke yake bali inamhusu kila Mtanzania.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Premy?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ikulu nayo kiboko. Ikiambiwa itaje yenyewe inaanza tena siasa kwa kusema wanojishuku wajisalimishe. Kusema kuwa wanaojishuku wajisalimishe ni kusema kuwa ama hana majina au anaogopa kuwataja.
   
 4. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Aibu imewafika kutokana na rais wao bomu. Tumechoshwa na Rais ambaye kila kukicha analalamika tu na hachukui hatua yoyote. Nilitamani kuona mfano wa Kiongozi wa Dini ambaye amekamatwa katika biashara ya madini.

  Hii ikulu itakuwa kazi yake kukanusha na kupinga tu yanayosemwa. Marehemu Shehe Yahaya aliposema kuwa atatuma majini kumlinda JK, Ikulu ikajitokeza na kusema kuwa hana haja na hayo majini. Kwa nini asingesema mwenyewe.

  Hakuna kupinda kona, JK anapaswa kujibu hoja za Maaskofu vinginevyo nawashauri maaskofu wote na wachungaji na mashehe kuanzia Ijumaa wawaambie waumini wao udhaifu wa Rais wao na haja iliyopo ya kumwondoa kabla ya 2015
   
 5. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndiyo shida ya kuwa mropokaji jk sasa ivi yuko kama vuvuzela ye ni kuropoka tu ka mke wa mjumbe.
   
 6. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Inawezekana viongozi hao si malaika lakini je, mlio hapo ikulu mna usafi kiasi gani?
   
 7. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Inashangaza kwamba mkuu wa
  nchi ya Tanzania aliwausia
  viongozi wa dini zote yaani
  dini za Kiislam, Kibaha'i,
  Kihindu, Kiyahudi, Kishinto,
  Kikristo, Kibudha, n.k, kuacha
  kuuza/kununua "BHANGI"
  lakini walio react ni wa dini
  moja tu, sijui kwa nini ?
   
 8. K

  Kamura JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo lipo wapi Rais kuwataka viongozi wa dini kupambana na dawa za kulevya? Kumwita Rais wa nchi ya Vuvuzela ni utovu wa nidhamu hii inaonyesha hata baba yako unamwita hivyo kama akikwambia masuala ambayo unao si sawa. Kuwa na nidhamu, huu si uwanja wa matusi.
   
Loading...