Kutokana na hali ya utandawazi ulioweka wazi kila kitu hata kile ambacho hakikutakiwa kuwa wazi....matokeo yake vijana wanajikuta wamejiingiza kwenye mambo ambayo ukubwa wake yanaizidi akili yake ambayo ni changa.....
Hususani katika masuala ya mahusiano...haya ni moja ya masuala ambayo vijana hujikuta tu wamejitumbukiza huko kwa matakwa ya matamanio yao na wala sio kwa utashi wao.....na ndio maana humu haziishi nyuzi za malalamiko kuhusiana na hayo mambo.....
yao ya kingono....
Kimsingi ni kwamba vijana ni kama wameacha kabisa matumizi ya akili zao na wameamua kuenenda kama wendawazimu....kwa kuendekeza matakwa ya nafsi zao......
Na kibaya zaidi hawashauriki....kila utakalowaambia litakalopingana na matakwa yao....utapewa tusi ambalo pengine tangu kuzaliwa hujawahi kulisikia na kuitwa mmbeya kwa kufuatilia maisha ya watu......mambo yakiwa magumu huko chumbani kwao....anakuja tena huku huku kwa wambea na wanaomfuatilia maisha yake kuja kuomba ushauri.....hapo tena amekuwa mdogo kiasi kwamba unaweza hata kumpitisha kwenye tundu ya sindano..........na sisi kwa kuwa tunajua kulea vijana...tunajitahidi kuwashauri kwa kadri ya uwezo wetu......kwani kuishi kwingi ndio kuona mengi.....
Ujana ni maji ya moto......
Maisha ya ujana ni nusu ya uwendawazimu.....
Ukipiga picha vituko unavyovifanya kwenye ujana wako unaweza usiamini kuwa ni wewe uliyekuwa ukiyafanya hayo pindi uitwapo babu....