comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na madaktari bingwa wa moyo kutoka European Society of Cardiology umetaja ukosefu wa ajira kuwa chanzo cha vifo kwa zaidi ya asilimia 50 ya wanaume hasa wanaougua maradhi ya moyo.
Utafiti huu ulionesha kutoka mwaka 1997 hadi kufikia mwaka 2012 zaidi ya watu 11 880 ambao ni sawa na asilimia 42 walikufa kutokana na magonjwa ya moyo baada ya kukosa ajira .Kwa mujibu wa Dr Roerth uhusiano uliopo kati ya ukosefu wa ajira na vifo unatokana na msongo wa mawazo ,watu kujiua na magonjwa ya shinikizo la damu.
Utafiti huu pia ulionesha zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivi vinatokea baada ya mtu kufukuzwa kazi au kukosa kazi huku ugonjwa wa moyo ukionekana kama sababu ya vifo vingi ukilinganisha na magonjwa kama kisukari na pressure.