Jana polisi mkoani Arusha
walifanya maandamano mji
mzima wa Arusha na
viunga vyake bila kulindwa
na hatimae maandamano
yao yakaisha salama bila
vurugu.
Maandamano ya Polisi
yaliyofanyika jana bila
vurugu yamenikumbusha
maandamano ya CHADEMA
yanayofanyika huku
wakijilinda wenyewe!
Maandamano ya CHADEMA
huwa ya amani na
humalizika bila vurugu au
hata mende kuuwawa
wakifanya maandamano
kwa kujilinda wao
wenyewe.
Polisi kazi yao na wajibu
wao ni kulinda
maandamano na
kuhakikisha kuwa
yanakuwa ya amani huku
wakihakikisha azma ya
waandamanaji ina timia
bila amani kutoweka,
wanapaswa kulinda
maandamano na
kuyasindikiza huku
wakihakikisha usalama wa
raia na mali unakuwepo.
Maandamano ya jana ya
Polisi yalikuwa ya aina
yake! Waliandamana bila
kupata kibali kwa aliye
yatangaza, polisi hawaja
wahi kutangaza
maandamano na
kuandamana, jana
imekuwa mshangao! Aliye
tangaza maandamano ya
kupinga ubadhirifu unao
endelea Dodoma ni
Mbowe, maandamano ya
kupinga kinacho endelea
Dodoma bado hayaja anza
rasmi, kulikoni Polisi
waanze kuingia road?!
Na kama huwa wanajua
kuandamana bila vurugu
kwa nini huwa wanaingilia
maandamano ya CHADEMA
na kujeruhi waandamanaji
wasio na hatia?
Jana nimeona kwenye
taarifa ya Habari ya ITV eti
"Chadema wawapa polisi
wakati mgumu..." nimebaki
nashangaa, aliye jipa
wakati mgumu kwa
kuandamana kabla ya
muda na kuandamana bila
ridhaa ya aliyetoa agizo la
kupinga kinacho endelea
Dodoma ni nani?!