Jerry slaa na mikakati yake ya kutafuta ubunge jimbo la ukonga 2015: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jerry slaa na mikakati yake ya kutafuta ubunge jimbo la ukonga 2015:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Brigedia, Jan 8, 2012.

 1. B

  Brigedia Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JERRY SLAA NA MIKAKATI YAKE YA KUTAFUTA UBUNGE JIMBO LA UKONGA 2015:
  Siku zote kiongozi bora wa uma ni yule anayekubali kukosolewa na kujisahisha pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa kazi yake. Jerry utake usitake kwenye hili lazima tukukosoe kwa facts, wewe umekuwa diwani katika kata ya ukonga kwa muda mrefu na hiki ni kipindi chako cha pili ambapo awamu ya kwanza ulikuwa naibu meya na sasa ni meya kamili lakini hakuna chochote kile cha maana ulichokifanya pamoja na mbunge wako wa awali Makongoro Mahanga na sasa Mama Eugene Mwaiposa ambaye amekuwa kama mbunge wa viti maalum na si wa jimbo. Sihitaji kuzungumzia takwimu ulizozitoa humu ndani because I know they have nothing to do na wananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisheni wewe na maswaiba zako, ambao ni mafisadi wakubwa. Hatuyafanyi haya kwa kukukomoa bali tunakukumbusha wajibu wako. Naomba niweke record sawa humu JF ili watanzania waelewe haya tunayoyazungumza wananchi wenzako wa Ukonga:

  Suala la huduma za serikali za mitaa Ukonga:
  Hii ni changamoto kubwa ya kwanza ambayo inakela sana wananchi wa Ukonga na maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala. Katika maeneo yote Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Ukonga ambao wote ni maswaiba wako wazuri unaowatumia kukupigia kampeni za kuusaka ubunge 2015, wamejifanya miungu watu na wanataka waabudiwe na wamekuwa wafujaji wazuri wa fedha za uma. Mathalani rafiki yako mkubwa ndugu Alfred Kipondya, mwenyekiti wa mtaa wa Madafu ambaye ni kinara wa kuwachangisha wanachi michango isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mmekuwa mkishirikiana nae kula pesa za miradi mbalimbali ya uma kama huu wa maji Mzambarauni kama ambavyo nimeelekeza hapo chini. Hali kadhalika unatueleza mmeongeza magari ya kuzoa taka ya municipal council ilihali wewe na Kipondya mnaendelea kuwachangisha wananchi kila kaya 3,000Tshs fedha ambazo zinaingia katika kampuni yenu binafsi, na hili ninakuombeni acheni mara moja mkija kwetu na wafungulia mbwa. Mbaya zaidi umekuwa ukiwashinikiza wenyeviti pamoja na watendaji wa serikaliza mitaa wakusanye 2,00Tshs kwa kila mtu anayekwenda kwa ajili ya kusainiwa document yoyote ile, ili muulize vizuri swaiba wako Kipondya hatokaa anisahau pale aliponiomba hela kwa ajili ya kunisainia document hukuakitaka kunipa risiti ya cash book yenye muhuli wa serikali ya mitaa. Wananchi huwa tunajiuliza Ilala Municipal Council kwenye hayo makusanyo mnayokusanya si kuna fedha mnazorudisha zitumike katika ofisi zetu za kata pamoja na serikali za mitaa, zinafanya kazi gani?? Jamani mbona hamtuonei huruma? Gharama za maisha zimepanda acheni kutunyonya sana.

  Suala la Mgogoro wa Ardhi Kinyerezi:
  Halmashauri ya Ilala imepitisha mpango wa upimaji wa viwanja kwenye maeneo ambayo watu wanaishi kule kinyerezi, ambapo mmewaambia wananchi wachangie gharama za upimaji ambapo katika kila square metre moja wanatakiwa kuchangia shilingi 1500. Ukishindwa kulipia gharama kwa ajili ya upimaji unanyangÂ’anywa eneo na unalipwa fidia. Na unajua fika kesi iko mahakamani ambapo wananchi wanapinga gharama ya uchangiaji na hali kadhalika mnajua fika kabisa hata kama mtu akishindwa kulipa gharama za upimaji, gharama za ufidiaji haziendani kabisa na gharama ahalisi za ardhi. Mwanasheria wako wa manispaa ya Ilala aliieleza mahakama kuu mbele ya Judge Shangwa kwamba fedha hizo mnazotaka kuwalipa wananchi mmezikopa bank. So mnataka hizo interest ndio wananchi wawasaidie kulipa?? Huu ni mradi ambao una harufu ya ufisadi na wewe unahusika moja kwa moja kwenye hili pamoja na maswaiba zako.


  Mradi wa maji Ukonga Mzambarauni:
  Mh mstaiki meya Jerry Slaa hili linaniuma sana kwani lina nigusa sana na watu wa Ukonga hawatokaa walisahau milele katika kipindi chao chote cha maisha yao hapa Duniani. Wananchi wote walichangishwa shilingi 5,000 Tshs kwa kila kaya kwa ajili ya mradi huu tena uchangiaji huo ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya kuondoa shida ya maji, na mkawaambia wananchi mtawasambazia mabomba kuanzia pale mzambarauini kwenda sehemu zingine mbalimbali kama Madafu,Mombasa, Gongo la Mboto, Mwisho wa Lami, mpaka Mazizini. Hivi huwa ukipita pale Mzambarauni roho huwa haikuumi kuona mmekula pesa za wananchi na huduma hakunailiyopatikana?? Muogopeni mwenyezi mungu tendeni haki panapostahili.

  Mkakati wako wa kuusaka Ubunge Jimbo La Ukonga-2015:
  Hongera sana kwa kushiriki kikamilifu kupigania kupatikana kwa jimbo la Ukonga ambalo linaongozwa na very weak candidate Mh Eugene Mwaiposa,ambaye anafahamu kuwa hiki ndiyo kipindi chake cha mwisho na hatorudi tena kwenye nafasi hiyo. Kwa hili naomba nikupongeze kwa kuona umuhimu wa kuwa na jimbo letu la Ukonga, dhana ambayo tuliamini itasaidia kutuletea maendeleo eneo letu la Ukonga, lakini hali imekuwa tofauti kabisa zaidi ya kuwa chaka la watu kuvuna pesa. Nashukuru umekili kuwa kama kugombea ungegombea 2010 kwani ulikuwa moja ya waasisi wa kupatikana kwa jimbo. Lakini ukweli wenyewe wa hili uko moyoni mwako, na ninajua dhamira yako inakusuta kwenye hili. Chanzo cha wewe kutogombea ubunge 2015 kinafahamika wazi kwa wale tunaofutailia. Mshauri wako mkubwa siku zote amekuwa ni mzee wetu mpendwa Balozi Patrick Tsere (Kipenzi cha vijana) ambaye ulifanya nae kazi akiwa kama DC wa Ilala na wewe ukiwa kama naibu Mstaiki meya. Unafahamu vizuri jinsi ambavyo walikuwa hawaelewani na mstaiki meya wa wakati huo na sababu kubwa ilikuwa ni uelewa pamoja na elimu ndogo aliyonayo mheshimiwa huyo kwa hiyo walikuwa wakipishana mzee Tsere muda wote. Hali iliyopelekea Mzee Tsere kukutumia wewe zaidi kwenye masuala mengi, hili unaweza ukabisha ila likowazi ulisafiri sana kwenda ziara za nje kwa sababu hiyo tu. Ili fika mahali mambo yakawa hayaendi kwa ajili ya mgogoro huo,ndipo Mh Rasi alipoona amsimamishe kazi Tsere na baadaye kumpangia nafasi ya ubalozi Malawi (rejea maneno ya Mh Raisi siku anamwapisha Tsere Ikulu). Na ni mzee Tsere aliyekushauri usubiri kwanza usiingie kwenye ubunge uongoze Ilala Municipal Council. Sasa mikakati yako ya kuusaka ubunge wa jimbo la Ukonga umeizindua katika ma Bar mbalimbali na kijiwe chako kikubwa cha kukusanya taarifa ni Mangi Bar (Tokyo) ,chini ya swaiba wako mkubwa na tapeli namba moja Saidi Dezo. Hutopata kula za Ukonga kwa kuwanywesha watu bia ndugu yetu, chapa kazi tukuvalue kwa uadilifu na uwajibikaji wako. Majuzi ulikuwa Kampala International University-KIU,kwa ajili ya mkakati huoo na umemwaga hela ukiamini vijana wanakupenda la hasha yawezekana hizo ni ndoto za buriani. Umri wako ulionao bado ni mdogo, weweni kijana mwenzetu cha kushangaza umekuwa na lugha za kejeli hali kadhalika dharau kubwa watu, hasa vijana unatuona tuko kijiweni. La hasha yawezekana sasa tukawa hatuna cha kukusaidia ila japo salamu tutakuona kiongozi wetu unatujali. Umediriki kuanza kuchangisha fedha kwenye mitandao na sehemu mbalimbali (ushaidi tunao) kwa ajili ya mambo mbalimbali ya Jimbo la Ukonga lakini badala ya kutimiza lengo la uchangishaji huo badala yake umekuwa ukiyafanya hayo mambo kisiasa. Haya yote yana mwisho wake ndugu yetu tunakuomba utimize wajibu wako kama ambavyo tulikupa ridhaa ya kutuwakilisha.

  Asante
  Brigedia
   
 2. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi huku JF hamna watu wa ukonga wachangie hii maneno?
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu hapati kura Ukonga.Yeye ni Meya lakini hakuna chochote alichofanya kwenye jimbo letu.Tuna shida kubwa ya barabara watu tunaoishi Kivule.Hali ni hiyo hiyo Kitunda,Mombasa,Machimbo nk.Kipindi kama hiki cha mvua nauli ya daladala ni shilingi elfu moja kwa safari moja.Yeye kama Meya amefanya nini kutusaidia watu wa huku? Ina maana anaona kunywesha watu beer kwenye mabar ndio dawa ya kupata kura? Anajidanganya sana.
   
 4. g

  gabatha Senior Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hyu kijana ni kambi ya EL na ni muuza sura tu hana jipya, 2015 ukonga ni mali ya chadema.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,901
  Trophy Points: 280
  mimi siyo mwana ukonga ila Jerry is my close friend, namshauri achape kazi.
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Huyu dogo jerry slaa kwa cycology 4 ze way nilvyomsoma kuwa yy anatumia karata ya ukijana ili kushinda na anatudhalilisha vijana wenzake, kwani maisha yake haypo kiutumishi kabisa na anatumia karata ya umeya kuuza sura town eti yy ni celebrety? Kazi kupiga picha na wadada wenye walovaa nusu uchi kwenye mabirthday ya kempsk, dah! Kweli mna kazi kweli kweli mnaochagua macelebrety badala ya viongzi watumishi majimboni kwenu.
   
 7. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mwaga bia mchizi wetu! Safari hii kwenye kura itabidi umtafute mchawi wako kama yanayolongwa ni kweli.
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Huyo Eugene Mwaiposa ni wa chama gani?Km ni CCM basi kummaliza ITAMAANISHA KITU TOFAUTI....
  !!!!?????!!!.Si kila mahali kuteuliwa naCCM kunamaanisha ushindi, kunaweza prove point za CDM.
   
 9. p

  pstar01884 Senior Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu sharobaro mpumbavu sana. Sasa aanze kuhesabu mwisho wake kisiasa kama haya yaliyonenwa ni ya kweli. Anasambaza bia aje kupata kura? What a shame pia ametudharau wanaukonga na watz kuwa tunanunulika kirahisi hivyo. Aanze kutambua kuwa kura ya kijana wa leo = ajira, huduma bora, maisha bora, haki na usawa, nk. Asipoyafanyia kazi haya kwa nafasi ya umeya aliyonayo sasa sio tu tutamkataa bali hata usalama wake wakt wa kuomba kura utakuwa rehani. Kiongozi gani kijana afu mpuuzi hv. Tumezoea hz tabia za kuhonga vitu vya ajabu ajabu kufanywa na hawa magamba mazee coz yamelelewa kwa rushwa, hadi huyu kijana karithi tabia hzo hzo? Tunamsubiri jimboni.
   
 10. M

  Mayunga96 Member

  #10
  Feb 26, 2014
  Joined: Oct 11, 2013
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siyo pandikizi wa kagame huyu jamaa...naomba mwenye details za URAIA wake atujuze tafadhali
   
Loading...