Kinachoitwa uwekezaji ndani ya pori la Ikorongo sasa imekuwa janga.Mwekezaji huyo au mmiliki huyo sasa amefunga njia ambayo ameikuta ikitumika kwa miaka mingi.Njia hiyo ambayo ilikuwa ikitumika na makambi ambayo yapo ndani ya Serengeti kwenda kupata huduma za zahanati na bidhaa imefungwa kabisa.
Je njia hiyo hata kama inapitia kidogo katika eneo la mwekezeji huyo TANAPA wameona ni sawa?Na kama ni sawa je siyo wakati muafaka sasa kuweka njia mbadala katika mpaka huo? Hakika watanzania nani katuloga?Tunauza halafu tunakuwa manamba katika nchi yetu.
Na sasa nasikia wanataka kununua kijiji cha Rubanda viongozi wa kijiji hicho wapo kwa mwekezaji huyo kila siku.Wanauza wenzao kwa mkate wa siku moja.Serikali hii ya hapa kazi tu isikubali kabisa.
Je mwekezaji huyo akinunua kijiji anataka kumiliki na njia ya kwenda Mugumu?Je hatatufungia pia na njia hiyo?Vijana wanaofanya kazi katika makambi yanayozunguka kijiji hicho na ambao kielimu hawakidhi viwango vya mnunuzi huyo wataenda wapi?